Mtoto kapotea akapatikana baada ya siku 10 Manzese, je huu ni ushirikina au?

beco

JF-Expert Member
May 7, 2013
1,339
782


Kuna mtoto mmoja alikuwa amekuja likizo kutokea iringa kaja Dar maeneo ya tandika Davis corner.Huku Dar ndipo wazazi wanaishi, tarehe 28 ya mwezi wa 12 2017 mida ya saa 4 usiku alikurupuka kama anaota akawa anatoka nje anakimbia kuna mpangaji mwenzao akatoka na kumkimbilia alipomkamata akawa mbishi anadai anamkimbilia mama yake wakati mama yake alikuwa ndani kalala watu wakachukulia poa wakajua ni usingizi wakamrudisha ndani.

Siku ya pili tarehe 29 dogo (miaka 8) akapotea tu bila ya kujulikana kaenda wapi, wametafuta kila sehemu wakaripoti na polisi walivyoona mda unazidi kwenda.

Siku ya pili na ya tatu wakaamua kwenda kukesha kwenye maombi mambo yakagoma.

Kuna mdada mmoja akamshika sikio akamwambia utahangaika bure hebu fanya plan B ndo akaanza kuhangaika kwa waganga kama watatu wote wakawa wanampa jibu moja kuwa mtoto yupo hajadhurika bado ila hatuwezi fanya chochote kwa kuwa aliefanya yupo ndani kwenu na yuko vizuri.

Baadae akiwa amekata tamaa kuna mtu akampa namba ya simu ya mtu yupo Sumbawanga akamwmbia mpigie simu alipompigia jamaa akamwmbia kazi ndogo tuma elfu 20 jamaa akatuma akaambiwa kesho utampata mwanao mchana.

Siku ya pili jamaa mchana akawa anampigia simu jamaa bila ya mafanikio simu ilikuwa haipatikani jamaa akajua kapigwa.

Ilipofika mida ya saa8 akapokea simu inamwambia aende Manzese kituoni akishuka asivuke bara bara atembee mita 200 na asimame atapokea simu nyingine akafanya kama alivyoagizwa baada ya mita 200 kweli alipigiwa akaambiwa mtoto kapatikana atume elfu 30
Karakata kwenye bonde na aliyehusika na huo mchezo ni shemeji yake kabisa mume wa dada yake na jamaa kakiri kuwa kweli kafanya ni masharti alopewa na mganga ili.

Awe tajiri yaani huku kimenuka aliyepotelewa anasema hawezi msamehe Jumamosi anaenda kwao akateketeze ukoo mzima.

Swali langu je kumtumia mtu kama huyu (mganga) kama umepatwa na tatizo ili umpate mtoto wako aliyepotea, ni ushirikina au?
 
Ha ha ha watu wamestuka aisee, hebu weka namber ya mganga wa Sumbawanga nimpe mchongo jombaa...
 
Ni true story sitaki mvutia yeyote na hata namba ya mganga sina ,kama una mpango na namba sina na mnaofuata pm mtoke wenyewe
 
ramli chonganishi ni marufuku kwa mujibu wa jamuhuri ya muungano wa watu wa zanzibar na tanganyika...
 
Back
Top Bottom