Mtoto kai-format simu yangu. Narudishaje data?

Simu yangu mtoto kai-format yote, je in njia gan au app gani nayoweza kuitumia kurudisha vyote alivyovifuta?
Simu haina password mpaka mtoto anachokonoa settings mpaka kipengele cha Factory Reset?
 
kuna watu mnadekeza sana watoto duh mpaka anafikia kuformat simu aiseee
 
Kabla ya ku-format ulikua na Google akaunti? Na uli-log in kwenye simu yako?

Kama jibu ni ndio, basi kuna 70% ukarudisha vitu vyako.

Fanya hivi, nenda kwenye Settings
Add google account (weka akaunti yako ya Google uliyoweka kabla ya simu yako ku-formatiwa),


Ukishafanya hivyo, Sync akaunti yako ya Google
(Option hii ya ku-sync inategemea na simu unayotumia)

Kama unataka picha zako na video basi download App ya Google photos toka Playstore

Kisha Log in kwenye Google Photos, hapa watakuletea picha zako zote.

NB: Kurudisha picha au video inategemea sana kama uliziback up kabla ya simu ku-formatiwa.

Kila la kheri!
 
Back
Top Bottom