Mtoto huyu ni malaika, anahitaji msaada wetu, na amekataa kwenda Loliondo

COMPLICATOR2011

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
253
35
Mtoto Cecilia Edward (14) (pichani), mkazi wa Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani, ambaye kwa sasa anaishi na mlezi wake, Mbagala jijini Dar es Salaam, bado anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo na amekuwa akihudhuria kliniki na hajapata mabadiliko.

Kwa mujibu wa mlezi huyo, Cecilia anasumbuliwa na ugonjwa huo, hali iliyosababisha tumbo kujaa maji mara kwa mara.

Imeelezwa na mlezi wake huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwamba tatizo hilo lilimuanza Cecilia baada ya wazazi wake wote kufariki dunia akiwa na umri wa miaka minne.

Hata hivyo, mlezi wake huyo alisema mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam kuwa hana niya ya kwenda kutibiwa Loliondo kama ilivyoripotiwa na gazeti hili siku za nyuma.

“Sina mpango wa kumpeleka mtoto huyu Loliondo na anaendelea na kliniki,” alisema.
Awali gazeti hili katika toleo namba 687 la Mei 31 liliandika kimakosa kuwa jina lake ni Khadija Ally na kuwa mtoto huyo anaomba msaada wa kwenda kutibiwa Loliondo kwa Babu.
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.
 
Dah pole sana dada!!Upate nafuu mapema. msiende kwa Babu nasisitiza tena, msiende loliondo.
 
Je Waziri wa Afya hajamuona mtoto huyo??? Hebu wale waliokaribu na Waziri au Naibu Waziri mama Nkya awafamishe kuhusu huyu mtoto.
 
Hakika wana'JF tumchangie huyu mtt na mungu atakulipa. Pia nasisitza Loliondo kwnye kiini macho wasimpeleke.
 
Nashauri source impeleke bungeni live uso kwa uso na mzee wa kulialia, amezoea kuliia posho je hili
 
Pole sana dada,nashauri apelekwe aende THT kwa Dr ferdinand anaweza kumsaidia.please ucende kwa babu.
 
Lions club na Motie Mengi institutions hizi si zinasaidia watu kwenda india kwa matibabu ya moyo? sasa sijui kama mlezi anataarifa hizi, na hiyo clinic anayo hudhuria ni ya wapi ambayo haiwezi kumshauri mgonjwa.
 
Kwa kweli nimesikitishwa sana na hali ya huyo mdogo wetu. Napendekeza kuwa wapewe taarifa waziri wa afya na ustawi wa jamii, waziri wa jinsia na watoto na mbunge wa jimbo analotoka. Wenye uwezo wa kumfikisha kwa hao waheshimiwa wajitahidi ikiwezekana wote wajulishwe ili mhusika mkuu apatikane kati ya hao waheshimiwa. Pole sana mdogo wangu!
 
halafu hapa wabunge wa magamba na ccj wanadai cdm na nccr ni wanafiki kukataa posho wakati huohuo kuna watu kama hawa nchini ambapo gharama ya kumtibia nje ni posho ya mwezi mmoja ya mbunge mmoja. CCM ONENI AIBU duniani tunapita tu...
 
Pole sana dada. Nashauri wahusika wampeleke ITV WAMTANGAZE NADHANI WATU WANAWEZA KUJITOKEZA ZAIDI KUSAIDIA AU HOSPITALI YA CRBT. Waweza pia kumsaidia af hapa jf naona pole tu, nashauri mtoa mada uweke mawasiliano ya kumpata mlezi direct ili watakao guswa wawasiliane nae fasta
 
Back
Top Bottom