Mtoto huyu alinifanya nitokwe na machozi, tupunguze ngono zembe

Captain A

Member
Dec 25, 2016
65
161
Wadau hii ni story ya kweli ilinitokea nilipenda pia kuwa hadithia wenzangu huenda kuna jambo tunaweza kujifunza hapa.

Ilikuwa ni siku ya alhamisi nikiwa natoka katika mihangaiko yangu ya kila siku, wakati tupo njiani na dereva tunaludi ofisini mbele yetu kulikuwa na wanafunzi wawili wa shule ya msingi kwa kukadilia wenye miaka 8 au 9 walikuwa wakiongozana, mara ghafla mmoja kati ya wale Wanafunzi alidondoka akiwa akilia kwa uchungu sana huku ameshikilia upande wa moyo wake,

baada ya kuona hali ile nilimwambia dereva asimamishe gari ili twende tukaone nini kimemtokea mwanafunzi yule, baada ya kufika eneo la tukio haraka nikaanza kumhoji yule mwanafunzi aliyedondoka vipi moyo unakuuma maana alikuwa akilia kwa uchungu sana huku ameshikilia upande wa moyo wake,

yule mwanafunzi kutokana na uchungu aliokuwa nao alishindwa ata kuzungumza alipatwa na kigugumizi ikabidi nianze kumbembeleza kwanza ili japo aweze kuongea, yule mwenzake alianza kukimbia kuondoka eneo hilo, baada ya muda wa dakika 2 yule alianza kuongea kwa kwikwi kwamba yule mwenzake alimwambia baba yake alikufa kwa Ukimwi hivyo na yeye pia ana Ukimwi na kwamba atakufa kwa Ukimwi,

kiukweli ghafla nilitokwa na machozi, nikajikuta baada ya kumsaidia yule mtoto, naanza na mimi kulia huku nikivuta taswira ya watoto wangu endapo ikitokea nimepata HIV au kufa na HIV. Ilinibidi nimchukue yule mtoto kwenye gari akatuelekeza tukampeleka mpaka kwao huku nikiwa namfariji na maneno,

ni kweli kwamba mtoto yule baba yake alikufa na HIV, na yeye alizaliwa akiwa na maambukizo ya HIV, swali ambalo limebaki kichwani kwangu mtoto yule ataendelea kuishi na hali hiyo ya uchungu kwa kipindi gani?

Ataendelea na kusoma huku akitaniwa na wenzake na hali ile na jinsi nilivyomuona akilia kwa uchungu sipati picha akiwa shuleni atakuwa analia kiasi gani, mwisho nawaomba sana ndugu zangu wenye watoto tutulie na familia zetu, Ukimwi upo na watoto wetu wanateseka sana kuwa yatima.

Tupunguze ngono zembe kwani hizo ni starehe za muda mfupi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dohhh,unakosa ht la kusema Mungu atamsaidia maana ni ngumu kwakweli
 
Kikubwa kumuomba Mungu azidi kukuepusha na ugonjwa huo maana hata ukijilinda miaka kadhaa ipo siku tu utaingiwa na tamaa za kimwili maana binadam tumeumbwa na hisia basi siku utakayo iona salama kwako ndio siku ya kwenda kupata huo ugonjwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom