Mtoto huyo kavutwa kope na mwalimu(Adhabu!) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto huyo kavutwa kope na mwalimu(Adhabu!)

Discussion in 'Jamii Photos' started by KakaKiiza, Mar 3, 2011.

 1. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,273
  Trophy Points: 280
  Mtoto.JPG Mtoto2.JPG
  Mtoto yupo darasa la tatu tu.Kisa chenyewe hana daftari?????!!!!

  Mtoto unamuona katika picha ni mwanafunzi wa shule ya msingi Buguruni anasoma darasa la tatu siku yanamkuta haya alikuwa na kosa la kutokuwa na daftari mwalimu anaeitwa Ms.Haule ni mdada tu akampiga na kumfinya kwa kumvuta ngozi ya macho na hicho ndio kilichotokea.Mtoto nyama ya macho ikamtoka nje,macho yakawa mekundu yanatoa tu machozi mtoto akawa kama kapoteza fahamu hata kusikia akawa hasikii.Jamani nimesikitika sana kila nikiangalia picha hii machozi yananitoka siwezi kuitazama.Mtoto anaendelea na matibabu katika hospital ya CCBRT ambako baba yake amempeleka.Baba wa mtoto anasikitika sana hana hakika kama mtoto wake atakuwa sawa!!Hivi ninavyoandika mwalimu kakimbia haijulikani alipo na polisi wanamtafuta.Kwa nini lakini mwalimu umefanya hivyo haukuwa na kitu kingine cha kumuadhibu huyo mtoto mpaka macho yake uyavute??Poor kid nahisi anasikia maumivu makali sana na huyu mtoto lazima hata kisaikolojia hayupo sawa.Wewe mwalimu huko uliko hata kama umejificha ila hutajificha milele hata kama si mkono wa sheria kukuangukia ila mwenyewezi Mungu atakuonyesha nguvu yake!!!
   
 2. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  KakaKiiza nilisikia hii kitu redioni siku lakini sikuwa kwenye utulivu kuipata sawasawa.
  Hiyo picha inaliza kama nini, huwezi itazama mara mbili.

  Mtoto wangu (class 4) amewahi kupigwa ngumi na mwalimu wake kisa amesahau daftari la history nyumbani, nilikomaa nao mpaka wakamsimamisha. Niliwaambia sipingi mtoto kupewa adhabu stahili lakini napinga mtoto kufundishwa ubondia.

  Walimu wanatoka na machungu yao nyumbani kisha wanaenda ku-explode kwa watoto wetu.
  Tunaanza kujenga taifa la watoto wenye hasira na kisirani. Adhabu zisizofaa huzalisha uasi ndani ya watoto na sijui kama walimu hasa shule za msingi wamefunzwa saikolojia ya ku-deal na watoto.

  Shule husika isaidie huyu mwalimu apatikane na sheria ichukue mkondo wake. Huyu mtoto anatia huruma sasa, unapata kilema kwa kosa la dogo kama hilo. Inasikitisha sana.
   
 3. Averos

  Averos JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 648
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  Haya ndo matokeo ya kutofuata taratibu katika utekelezaji wa adhabu, mwalimu haruhusiwi kumpiga mtt apendavyo yeye bali kwa kufuata minogozo iliyopo, imagine angekuwa ni mtoto wake ndie aliyefanywa hivyo angekubali?
   
 4. g

  geophysics JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 904
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Duu sitaki niamini hili kama ni kweli.... Natamani nigharimie matibabu ya mtoto huyu ili awe salama.... Walio karibu watufahamishe imetokea lini hili...Mtoto na mzazi wa mtoto pole....
   
 5. Chitemo

  Chitemo JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,293
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Huyo mwalimu ni mseng* na nahisi ana mtindio wa ubongo na hyo taalamu ya ualm kaingia kwa magumashi tu. Dont she know teaching is a noble proffessional? Ualimu ni wito jaman tena watoka kwa mungu. Alaaniwe hata huko alikokmbilia. Puuuuumbav* zake, sina shaka huyo mwalm ni tasa..!!?
   
 6. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #6
  Mar 3, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Dah!! Hawa walimu wetu bwana....
   
 7. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2011
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145

  Ndio matatizo ya kuajiri form four failures kwenye taaluma ya ualimu wa shule za msingi, wengi (hasa hawa wa kizazi kipya) wana mtindio wa ubongo!
   
 8. s

  shosti JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  mhh tunasafari ndefu kweli,ila tutegemee makubwa zaidi hivi hizi jeuri za kugusa watoto wasio wetu tunazitoa wapi:rain:
   
 9. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280

  yaani mimi siku mwalimu anampiga gaude wangu...duuuh shule itageuka uwanja wa vita...yaani ntatembeza karate acha kabisa
   
 10. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #10
  Mar 3, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kwanza nitoe pole kwa mtoo na wazazi wake,namuombea mtoto nafuu na Mungu atamsaidia na kupona.
  Zamani taaluma hii ya ualimu ilikuwa ni wito na watu waliipenda tofauti na sasa ambapo imeingiliwa na mdudu mbaya uitwao mamluki ambao hawana kitu cha kufanya na huamua kuingia sehemu hii ya ualimu ili kuweza kujikimu na maisha magumu na ndio maana tunaona vitendo vibaya kama hivi kwa watoto wetu.
   
 11. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #11
  Mar 3, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Tafadhali naomba mawasiliano na Baba wa huyu kijana. (ni PM)
   
 12. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #12
  Mar 3, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Huyo Mwalimu ni mchawi kabsaaa!!
   
 13. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #13
  Mar 3, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Imeandikwa, "Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa. Msilaumu, nanyi hamtalaumiwa. Sameheni, nanyi mtasamehewa"
   
 14. J

  Just i am Member

  #14
  Mar 4, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mh susy hayo yote uluyo ya sema ni sawa ila kwa hili kwa mtoto kama hyu hapana..tena aliyelitenda kalitenda kwa makusudi akiwa na akili zke timamu
   
 15. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #15
  Mar 4, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  OMG!!!

  [​IMG]

  Consequences of internecine violence. Teachers on one side and the government on the other. Pupils/students are the victims. Low wages, poor living conditions, unpredictable future...etc. All these accumulated rage befall to these kids
   
 16. hundukad

  hundukad Member

  #16
  Mar 4, 2011
  Joined: Jun 26, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza nampa pole huyu kijana....habari nilizonazo kutoka kwa walimu wa shule hiyo ni kwamba huyu mwanafunzi alichapwa viboko matakoni, lakini inasemekana ana matatizo ya figo...baada ya kuchapwa akaanza kuumwa na kuzidiwa ambapo alipelekwa hospitali ya Amana ambako alipewa dawa zilizosababisha reaction na hali yake kuzidi kuwa mbaya na kuvimba macho....baada ya hapo alipelekwa ccbrt ambako ametibiwa hivi sasa ni mzima....ningependa kuwaasa ndugu zangu tusiwe tunarukia maneno tuambiwayo na kuyaamini, na kuhukumu kisha kufanya kazi ya magereza....ndiko tulikofika sasa...shame
   
 17. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #17
  Mar 4, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli inasikitisha sana. Tatizo walimu wengi wamechanganyikiwa na maisha hivyo hasira zao nyingi wanaenda kuzimalizia kwa watoto kama hawa. Ugua pole mdogo wangu.
   
 18. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #18
  Mar 4, 2011
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  huyo si mwalimu, ukimwangalia huyo mtoto vizuri utagundu kuwa yule mwalimu ni jini akiwa kazini balijini katika umbo la mwili wa mwanadamu
  so its better to have a say, to our ALMIGHTY GOD for this kid
   
 19. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #19
  Mar 5, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  au mwalimu alikuwa na mimba changa?
   
 20. kisute

  kisute Member

  #20
  Mar 5, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii inadhihirisha kiasi gani walimu wanakosa maadili waliopewa kuelimisha jamii.
  Kama ukifuatilia kiundani huenda utakuta ni miongoni mwa wale waliajiriwa kipindi cha crush programe ili mradi kukidhi uhaba wa walimu nchini. Walimu wa enzi zetu walilelewa kimaadili na wlikuwa watiifu sana. Mi binafsi sipendezwi wa watu wenye mioyo mibaya, wakatili kiasi hicho waendelee kuiadhibu jamii yetu. Naomba vyombo husika kumfuatilia huyo mwalimu kwa kila hali hadi apatikane na sheria ichukue mkondo wake. Wananchi mnaomfahamu huyo mwalimu mfichueni kokote alikojificha.
   
Loading...