Mtoto haramu katika familia

Boeing 747

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
3,510
9,349
Heshima kwa kila mmoja

Inafahamika wazi mama ndiye anayejua baba halisi wa mtoto..

Kutokana na uhalisia huo, watu wengi wamekuwa na maswali yasiyo na majibu ya moja kwa moja..mfano

1. Unaweza ukakuta familia ina watoto 5, wamesoma na wana kazi nzuri tu..ila Kuna mmoja haendani kabisaa na wenzake...yeye ana tabia za kipekee..hamtii mzee wake wala mama yake, wala ndugu zake....yaani ni pasua kichwa..

Hapa nina maanisha unaweza ukakuta watoto 4 ni wapole, wasikivu na wanasikilizana ila huyo mmoja ni pasua kichwa....hawa 4 wanabaki na maswali, Je inakuwa ndugu yetu hafanani na sisi kitabia..?

2.Mnaweza mkawa kwenye kikao cha famili, huyu ndugu mmoja hawaachi mfikie muafaka mzuri lazima atawavuruga tu....si kosa lake...mama anajua siri.

3.Baba anaweza akawa anaumwa, kalazwa hospitali ndugu wote mpo bega kwa bega kumuuguza baba, huyu ndugu mmoja yeye hana time....tena wakati mwingine msishangae kusikia akiwaambia mzee kashazeeka...inatakiwa arest in peace atuachie mali...mnajiuliza huyu kalogwa, hampati majibu...

4.Huyu ndugu mmoja pamoja na ukorofi na tabia zake mbaya , unakuta mama anampenda sana na anamtetea sana haswa kwenye swala la kupewa mali...mnajiuliza mbona sisi tunajitoa hivi lakini mama hatukingii kifua namna hii..?

%%%%%% Majibu ya haya maswali 4 ni marahisi...Mara nyingi mtoto wa namna hiyo huwa ni mtoto haramu katika familia...yaani si damu moja na ndugu zake..

Kuna Mila na desturi za makabila fulani fulani hapa nchi mwanamke anafundwa vilivyo.

Wanawake hao huwa wanafundishwa kuwa akiingia kwenye ndoa, asizae watoto wote na mume mmoja.. mtoto mmoja au wawili anafundishwa azae na baba mwingine.

Lengo na mafundisho haya lilikuwa ni kama ifuatavyo.

1. endapo ukoo wa mume wa ndoa una laana fulani, asili ya wizi, magonjwa ya kurithi kama kifafa, kuna uwezekano mkubwa watoto wa baba huyo wakarithi matataizo hayo.

Hivyo mama hutafuta mwanaune mwingine kwa siri kubwa, anazaa naye ili kupata mtoto mmoja wa kukomboa wenzake endapo matatizo niliyoyaeleza yatatokea..

Jambo hili hufanyika kwa siri kubwa na wamama wafundaji wanajua wazi kuwa mtoto wa 3 kuzaliwa si wafulani..

Wanawake huwa hawana desturi ya kutunza siri, lakini kwa hili, hata umchome na mshale wa moto jichoni, hatasema siri hii....yupo radhi afe.

Lakini yale maswali 4 ya mwanzo yanaweza yakaja kinyume, watoto wakazaliwa 5 , watoto 4 wakawa na tabia mbaya zisizovumilika, wizi, ugomvi, ulevi, umalaya, hawataki kazi wao ni kumtesa mzee awape pesa za kula bata, ila huyu mtoto mmoja akawa smart, mpole, msikivu, mchapakazi, yaani baba ndiyo akawa anamtegemea hata kumrithisha biashara zake...maskini kumbe si damu yake..

Lakini ukweli ni kwamba hapa tunasema mama aliona ameolewa na zuzu, mume ambaye dish lineyumba, hivyo akatafuta mwanaune wa kweli, akazaa naye kwa siri ,....baba ukalea ukijua ni mwanao...kumbe ni damu ya ukoo mwingine..

Mama atajitahidi sana kumsihi mzee amwandikie mtoto huyu mali nyingi zaidi...coz mama anajua siri.

Mtoto wa namna hii ndiyo hawa tunawaita watoto haramu katika familia, ...anaweza akawa mbaya au akawa mzuri.....il hatafanana na wenzake hata kidogo...

Mwisho....usijeukashangaa kwenu kuna ndugu mmoja anawatesa balaa, rangi hata hamfanani...baba ameshamchoka ila mama uenu haachi kuwasihi, msimchukie ndugu yenu.....Kachukua tabia za mjomba wake wa Sumbawanga....hakuna cha Sumbawanga..baba ni wa mtaa wa pili hapo....trust me.

NB...wanaume tuamke hawa wanawake wanatuzidi kete






IMG_20190814_121517_010.jpeg
 
umesahau ngoja nikukumbushe kitanda hakizai haramu
Huo ni msemo waliotumia wahenga kuwapooza wanaume waliochapiwa...

Sasa hivi tunasema mke akichepuka akazaa, hapo kitanda kimezaa haramu.
 
Sikubaliani na wewe katika hili, unataka kusema kuwa ikiwa familia ina watoto watano halafu mmoja akawa na ulemavu wa ngozi (zeruzeru/ albino) huyo nae atakuwa mwanaharamu?

Kumbuka kuwa kuna mtoto anaweza akarithi tabia ya babu wa baba yake ambaye pengine wazazi wake hawakuwahi kumuona.
 
Sikubaliani na wewe katika hili, unataka kusema kuwa ikiwa familia ina watoto watano halafu mmoja akawa na ulemavu wa ngozi (zeruzeru/ albino) huyo nae atakuwa mwanaharamu?

Kumbuka kuwa kuna mtoto anaweza akarithi tabia ya babu wa baba yake ambaye pengine wazazi wake hawakuwahi kumuona.
Sijazubgumzia ulemavu hapa...nimezungumzia tabia...

Karibu sana...
 
Mimi mwenyewe sijui kama ni mtoto wa dingi wangu
Nadhani nitakua tofauti, mali na vyote vinabaki hufi navyo cha msingi kama kusomesha kumpa mali etc mpe uache alama duniani.
Familia zimebeba mambo mengi sana yanayohuzunisha hasa linapokuja swala la mtoto. Rejea watoto wa mitaani, ukiamua kufanya simple observation wana mengi ya kusimulia na kusikitisha.
 
Hoja yangu ni kuwa mtoto anaweza akarithi tabia za vizazi vilivyotangulia hivyo akaonekana tofauti na wazazi/ndugu zake
Watoto wa damu moja kuna tabia mbili tatu ambazo ni common watafanana....hata iweje....mfano kuonge, kucheka, kutembea, kukasirika kwao n.k.
Kwa hiyo bado hujanishawishi..
 
Mimi mwenyewe sijui kama ni mtoto wa dingi wangu
Nadhani nitakua tofauti, mali na vyote vinabaki hufi navyo cha msingi kama kusomesha kumpa mali etc mpe uache alama duniani.
Familia zimebeba mambo mengi sana yanayohuzunisha hasa linapokuja swala la mtoto. Rejea watoto wa mitaani, ukiamua kufanya simple observation wana mengi ya kusimulia na kusikitisha.
Fact....ila wamama wanajua ukweli wote...hata hao watoto wa mtaani wengine wana mama zao wapo hai na wamekana kuwatajia wanao baba zao.
 
Back
Top Bottom