Mtoto Doreen aruhusiwa kutoka hospitali

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Marekani. Mtoto Doreen Mshana, manusura wa ajali ya Lucky Vincent, ameruhusiwa kutoka Hospitali na sasa ameungana na wenzake wawili katika nyumba maalum wanamoishi, Marekani, jimbo la Iowa.

Awali, wanafunzi wengine waliokuwa wakitibiwa katika Hospitali ya Mercy Hospital, Sioux City, Saidia Awadh na Wilson Tarimo, waliruhusiwa kutoka hospitali walimokuwa wakitibiwa.

Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, ameandika katika ukurasa wake wa facebook na kueleza kuwa sasa Doreen, ameungana na wenzake baada ya hali yake kuimarika.

Doreen, alibaki hospitali hapo kutokana na majereha makubwa aliyopata na hivyo kulazimika kufanyiwa upasuaji mkubwa wa uti wa mgongo.

Wanafunzi hao walinusurika katika ajali ya basi la shule ya msingi ya Lucky Vincent, iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva, Mei 6 mwaka huu, Karatu, Arusha.

Chanzo: Mwananchi
 
I am exceedingly glad to hear this fellow and namesake of my wife is doing better and has been discharged from the hospital today. May God heal them all.
 
Mkono wa Bwana uendelee kuwa juu yao na nguvu ya uponyaji iendelee kumiminika juu yao.
 
Back
Top Bottom