Mtoto chini ya miaka 14 haruhusiwi kufanya kazi/ kuajiriwa

Status
Not open for further replies.

Rahma Salum

Member
Sep 7, 2020
30
59
Kwa mujibu wa sheria ya Mtoto (2009), Watoto wana ruhusa ya kufanya kazi baada ya kutimiza umri wa miaka 14. Kazi haipaswi kumzuia mtoto kuhudhuria masomo au kupata muda wa kujisomea na kupumzika.

Watoto wasiajiriwe kufanya kazi nyakati za usiku. Yeyote anayewafanyisha kazi watoto kupita kiasi, au asiyewalipa ujira unaostahili, basi anavunja sheria hii.
 
mimi nina wafanyakazi wa shamba wana 13 yrs watatu... niliwapa mtihani mmoja ana akili sana nataka kumsomesha sec..wale wenzake ni shamba mwanzo mwisho. Kinachoniuma hela zote nawalipa wazazi wao zote as if wao ndiyo wanafanya kazi - maisha haya jamani.

Kuhusu hiyo sheria, Africa haiwezi kufanya kazi ndugu, maisha ya watu walio wengi ni duni mno.
 
Kwanini unawalipa wazazi wakati wanaofanya kazi ni watoto? Halafu unadiriki kabisa kusema inakuuma?

Jitafakari mkuu kuna mahali unakosea.
 
Nilitafuta mfanyakazi wa ndani nikaletewa binti wa miaka 12. Nikawaza sana baadae nikaona hata nikimrejesha kwao atapelekwa kwingine nikaamua nikae nae acheze na watoto.

Alikua bright sanaaa baada ya mwaka nikampeleka shule form one, akawa anaongoza darasani.

Form two akaanza utukutu nikafuatilia shuleni nikiwa na maamuzi ya kupata msaada wa walimu ili atoe maamuzi ya kuendelea na na shule au kuacha shule... akasema anataka shule tena kwa machozi

Form three akakimbilia kwa mume muuza urembo, akaishi nae miezi nane wakaachana na sasa amerudi kijijini kwao

Nimejifunza sana hapa
 
Kwanini unawalipa wazazi wakati wanaofanya kazi ni watoto? Halafu unadiriki kabisa kusema inakuuma?

Jitafakari mkuu kuna mahali unakosea.
yaani masharti toka wanakuja toka makwao ni kwamba lazima hela niwalipe wazazi wao - yaani ni tatizo!! Kuna muda niliacha kuwapelekea makusudi kama miezi 3 hivi - wale vijana wakaniambia nipeleke sababu babu yao anataka kuezeka nyumba !! nikatuma.
 
mimi nina wafanyakazi wa shamba wana 13 yrs watatu... niliwapa mtihani mmoja ana akili sana nataka kumsomesha sec..wale wenzake ni shamba mwanzo mwisho. Kinachoniuma hela zote nawalipa wazazi wao zote as if wao ndiyo wanafanya kazi - maisha haya jamani.

Kuhusu hiyo sheria, Africa haiwezi kufanya kazi ndugu, maisha ya watu walio wengi ni duni mno.

Wewe vipi? Unamlipaje mtu ambae hajakufanyia kazi???
 
it was part of agreement kabla hawajaletwa kwangu !! inakuwa tatizo kidogo ku-reverse ingawa huwa najaribu lakini mara zote nakwama sababu watoto nao wanataka hela itumwe!! hawanipi ushirikiano.
 
Jaribu kuliangalia hilo kwa umakini mkuu...

Siku hao watoto wakisema umewatumikisha bila kuwalipa na wazazi wakasema pesa ulizokua unawapa sio mshahara wa watoto wao ila ni makubaliano yako na wao utapata tabu sana
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom