mtoto apewa adhabu ya kuning’inizwa mtini miguu juu kichwa chini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mtoto apewa adhabu ya kuning’inizwa mtini miguu juu kichwa chini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Mar 31, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MWANAFUNZI wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Dukamba, amepewa adhabu ya kuning’inizwa mtini miguu juu kichwa chini, huku amefungwa miguu na mikono.

  Inadaiwa mtoto huyo mkazi wa kijiji na kata ya Kharumwa wilayani hapa, Dickson Mjarifu (8), alipewa adhabu hiyo kwa karibu wiki moja na mama yake wa kufikia, Dafroza Masilu (25) kwa kushirikiana na baba yake mzazi, Hezron Mjarifu (35) huku akionywa kuwa angesema angeuawa.

  Akisimulia kisa hicho mwanzoni mwa wiki hii katika mahojiano maalumu na gazeti hili, mwalimu wa darasa analosoma mwanafunzi huyo, Agnes Boniphace, alidai kuwa Alhamisi iliyopita asubuhi, wanafunzi wenzake walitoa taarifa shuleni kuhusu mateso aliyokuwa akipata mwenzao.

  Kwa mujibu wa Mwalimu Agnes, ambaye sasa anaishi na Dickson, wanafunzi hao walipokuwa wakipita njiani karibu na nyumba anayoishi mtoto huyo, Dickson aliwaita kuwaomba msaada.

  Mwalimu Agnes alidai kuwa wanafunzi hao waliposogea karibu na nyumba hiyo, walimkuta mwenzao amening’inia mtini huku akiomba wasaidie kumnasua kutoka katika mti huo.

  “Baada ya kuwaita, wenzake walikwenda na kumwona, wakakimbia hadi shuleni na kutoa taarifa kwa Mwalimu Mkuu, ambaye alituchukua sisi baadhi ya walimu na wanafunzi hao na kwenda kwenye eneo la tukio.

  “Tulimkuta Dickson ananing’inia huku amefungwa kamba mikono yote na miguu huku kichwa kikielekezwa chini mfano wa popo.

  “Tulipoona hali hiyo, ilitulazimu kutoa taarifa kwa uongozi wa Kijiji ambapo Ofisa Mtendaji wa Kijiji alifika na kushuhudia, tukamfungua akateremshwa na kwenda naye shuleni akatusimulia kila kitu, yakiwamo mateso ambayo amekuwa akifanyiwa na mama huyo wa kambo,’’ alidai Mwalimu Agnes.

  Walipofika shuleni, walimvua mtoto huyo nguo na kushuhudia makovu sehemu mbalimbali za mwili na hasa mgongoni, makalioni na kifuani, huku akionesha alama za fimbo.

  Kutokana na hali ya makovu na alama za fimbo, uongozi wa Shule ulimwita mama huyo na kumhoji juu ya hali ya mtoto huyo.

  “Cha ajabu, mama alipofika na kuhojiwa, alisema anayehusika na kipigo cha mtoto huyo ni baba yake mzazi, Hezron Mjarifu, ambaye ni mkulima katika kijiji hicho.

  “Tuliamua kuwaita polisi ambao walimkamata mtuhumiwa na kumpeleka kituoni na kumpatia mtoto fomu namba tatu ya matibabu,’’ alifafanua.

  Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Kharumwa, Dk. Leonard Mugema, aliyempa matibabu mtoto huyo alisema baada ya uchunguzi wa kina, alibaini mambo mengi yaliyosababishwa na kipigo hicho.

  Dk. Mugema alisema walibaini majeraha ya ndani yaliyosababisha damu kuvilia mwilini.

  “Hali ya mtoto si nzuri ana makovu mwili mzima akikuvulia nguo kama una roho nyepesi unaweza kumkimbia bila kumpa matibabu ... lakini nashukuru manesi wangu wamejitahidi kumsafisha vidonda vizuri.

  “Tulitaka tumlaze, lakini yeye akaomba akae kwa mwalimu wake wa darasa ambaye amekuwa akimleta asubuhi na jioni hapa hospitalini kwa matibabu,” alisema Dk. Mugema.

  Dk. Mugema aliongeza kuwa baada ya kumfanyia vipimo vya kina mtoto huyo, walibaini anakabiliwa pia na utapiamlo uliosababishwa na kukosa chakula mara kwa mara.

  Akizungumza na gazeti hili, Dickson alidai amekuwa akipigwa kwa mwezi na wiki tatu kila siku na mama yake alimwekea ‘dozi’ ya kuchapwa viboko kila siku asubuhi na jioni.

  Alidai pia mara nyingi amekuwa akinyimwa chakula na kufanyishwa kazi nyingi na ngumu, ikiwa ni pamoja na kusomba maji kutoka kisimani na kwenda kusenya kuni porini.

  Mtoto huyo alibainisha kwamba alionywa na mama yake huyo kwamba endapo atatoa siri atamwua, hali iliyosababisha akae kimya siku zote hizo, hadi siku hiyo alipoomba msaada kwa wanafunzi wenzake.

  Alidai kuwa aliamua kuomba msaada, kwa kuwa mama huyo hakuwapo, kwani alikwenda shambani na kumwacha akining’inia mtini.
   
 2. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Tabia zetu siku hizi zinaashiria kabisa kuwa mwisho wa dunia umekaribia,wazazi hawa wanatakiwa kupewa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine ambao wana tabia kama hizi.
   
 3. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hawa wachukuliwe hatua kali kabisa mke na mume ni makatili na wauaji wakubwa.

  watoto wanfanyiwa ukatili hivi?
  Ki ukweli inauma sana.
   
 4. Chitemo

  Chitemo JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,293
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  tuweke wazi ni mkoa ama wilaya gan huu unyama umetokea, coz hvyo vjj ni ngumu kutambua! Ila sheria must take its action. Pole sana victim wa huo utesaji mungu atakuwa nawe.
   
 5. a

  arinaswi Senior Member

  #5
  Mar 31, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 183
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ndugu, Kharumwa iko mkoa wa mwanza wilaya ya geita.
   
 6. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #6
  Mar 31, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ni kweli binadamu tumekua kama wanyama!hii yote ni sababu mtoto ni wa kambo kwa mama na huyu jamaa anaonekana katawaliwa na mkewe kiasi cha kuachia mwanawe ateswe huku na yeye akishiriki!
   
 7. k

  kisukari JF-Expert Member

  #7
  Mar 31, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,754
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  kwa kweli inasikitisha,halafu baadae mtoto atarudishwa kwa huyo huyo mama,maisha haya,hujui umlalamikie nani au ukimbilie wapi.wamama wakiwa na roho mbaya,huwa na roho mbaya haswa.ingekuwa mtoto wake angemfanyia hivyo kweli.na hao wababa nao,aaah inasikitisha
   
Loading...