Mtoto anusulika kuliwa na Simba bahari zoo Dar es Salaam

kwan mkuu mbona kajieleza vizur kuwa kutokana na mishe mishe zilizokuwapo hakufanikiwa kupata picture.......jamaa hana professional ya uandish wa habar coz angekuwa nayo inamaana angeacha pia mawe simba na angekuwa anakomaa tu na camera yake na hatimaye pengine jiwe lake ndo limemwwondoa simba bila yeye pengine mtoto angeliwa kabisa!!!
 
Habari wakuu,
leo nimeshuhidia tukio la kutisha na kusikitisha ambapo mtoto mwenye umri upatao miaka sita hivi amedakwa na simba wakati akiwa zoo.

inaonekana mtoto huyo alipenya kwenye fensi ndogo na kujikuta akiwa karibu kabisa na fensi kubwa yenye matundu makubwa na hatimaye kudakwa. kilichofuata hapo ni sisi kuanza kuwashambulia simba hao kwa mawe na hatimaye walimuachia mtoto huyo huku uso ukiwa umejaa damu na nyama za mapaja zikiwa zinaning'inia.

SOURCE: mimi mwenyewe, ninaishi karibu kabisa na eneo hilo.

Simba hao hapo pichani ndio waliotaka kukatisha maisha ya kiumbe huyo, sikuweza kupata picha ya tukio hilo kutokana na mshituko niliokuwa nao (lakini picha hii imepigwa mara baada ya tukio). Mama mtoto alizimia kwa muda, mtoto amechukuliwa kupelekwa hospitali.
Good job for saving a Life,God bless you.
 
sasa huyo mama alikuwa mjinga kiasi gani hata asimwangalie mtoto wake anafanya nini? NIngekuwepo ningemkata vibao mamake wa huyo mtoto.
Tatizo sio Mama mtoto peke yake. Haiwezekani viewers wawe na access mpaka kugusa hiyo fencing ya cage. Hiyo zoo/hoteli tayari ina safety issues. Kwanza wanashindwa hata kuwatunza hao wanyama, Simba wana starvishwa mpaka vimekuwa kama vi mbwa koko vya uswahilini vinavyojitegemea? Simba gani hao wamedaka mtu halafu eti wakapigwa jiwe na mleta mada wakamtema mtoto!? Give me a break. Simba kakung'ang'ania umpige jiwe akuchunie, kawa mbwa?

attachment.php
 
Umesomeka Kamanda! Ila ungeweka picha ya mtoto ingeboresha thread hii.

Jamani! Picha ya mtoto aliyeraruliwa na simba ina raha gani kuwekwa hapa? Hata hivyo mleta thread kajieleza vya kutosha kwamba muda aliokuwa nao aliutumia kumwokoa mtoto na si kupiga picha. Hongera Lukansola kwa kumwokoa mtoto badala ya kupiga picha.
 
Uli mudesi bee
Habari wakuu,
leo nimeshuhidia tukio la kutisha na kusikitisha ambapo mtoto mwenye umri upatao miaka sita hivi amedakwa na simba wakati akiwa zoo.

inaonekana mtoto huyo alipenya kwenye fensi ndogo na kujikuta akiwa karibu kabisa na fensi kubwa yenye matundu makubwa na hatimaye kudakwa. kilichofuata hapo ni sisi kuanza kuwashambulia simba hao kwa mawe na hatimaye walimuachia mtoto huyo huku uso ukiwa umejaa damu na nyama za mapaja zikiwa zinaning'inia.

SOURCE: mimi mwenyewe, ninaishi karibu kabisa na eneo hilo.

Simba hao hapo pichani ndio waliotaka kukatisha maisha ya kiumbe huyo, sikuweza kupata picha ya tukio hilo kutokana na mshituko niliokuwa nao (lakini picha hii imepigwa mara baada ya tukio). Mama mtoto alizimia kwa muda, mtoto amechukuliwa kupelekwa hospitali.
 
Nimeona Jana kwenye TV Kama kuna Mtu anabisha shauri lake. Kuna vitu vingi vya muhimu tunapuuzia, unaenda na mtoto zoo halafu anaachwa unattended. Na zoo nayo kwa Nini eneo ambalo kuna simba wanaliacha bila mfanyakazi wao, kulinda both simba na binadamu wazembe Kama huyo mama.

Kwa Nini simba aliweza kumyakua mtoto aliyekuwa hajaingia kwenye cage?

Tunachukulia kila kitu kirahihirahisi tu sisi ni watu wa namna gani jamani.
 
Hakuna kitu ninachochukia kama hili neno bahati au angekufa tungesema Mungu kampenda zaidi. Huu ni uzembe wa zoo na huyo mama. Ingekuwa nchi za wenzetu mwenye zoo maisha yangekuwa magumu kwake kwa kupelekwa mahakani na kulipa fidia
 
ndugu watoto wa siku hizi hawatabiriki kirahisi,dakika moja tu ,inamtosha kukutoroka!watoto wa siku hizi wadadisi sana.
Kuna haja ya watu kupata elimu ya namna ya kutembelea hizo Zoo, sasa huyo mama alikuwa mjinga kiasi gani hata asimwangalie mtoto wake anafanya nini? NIngekuwepo ningemkata vibao mamake wa huyo mtoto.
 
pole sana kwa mtoto aliyejeruhiwa,na pole sana kwa mama mtoto,tunamuombea kwa mungu mtoto apone haraka.na pia hongereni wale wote mlioshiriki kuokoa maisha ya huyo mtoto!mtoto wa mwenzio ni wako!
 
Back
Top Bottom