Mtoto Anapoteswa namna hii Na wewe unarekodi tu Video Yako. Unaakili wewe!?

BabaTina

JF-Expert Member
Aug 29, 2008
429
574
ad0cc97c4f25f4538d8e4294879d934a.jpg


Wanajamii kuna video inaenda viral huko Facebook ya mama mmoja akionekana kumnyanyasa mtoto mdogo mwenye umri wa kati ya miaka2-3.

Katika video hiyo jimama moja lenye roho ya kutu kushinda shetani limekalia siti huku likionekana kumsimamisha mtoto yule ashike Bomba wakati lenyewe limestarehe.

Mbaya zaidi mtoto yule akawa anashikwa na usingizi hivo mtoto akawa anajaribu kumuegemea jimama hill ambalo bila chembe ya huruma likawa linamsukumiza mtoto yule ili asisinzie.

Ni hakika mtoto yule kapata mateso makubwa sana sana!

Lakini pia najiuliza huyu mtu aliyekuwa unarekodi alishindwa vp kuchukua hatua wakati mtoto yule akipata mateso Yale. Binafsi nimeona kijana huyu ambaye kaposti hiyo video hapo kwenye ukurasa wake wa FB naye pia anaroho mbaya kama ya jibibi lile. Alipaswa kumuokoa huyo mtoto.

Kwa wanaojua kutumia teknolojia plz naomba muichote hiyo video muiweke hapa jukwaani ili kila mtu ajionee ushetani ule na Habari hii iwafikie maafisa wote wa usalama wa RAIA na haki za watoto popote pale walipo huyu jibibi awekwe nyuma ya nondo

Hii ni screen shot ya video na jina linaloonekana ni la muhusika aliyepost hiyo video wanaoweza kuichota waichote Tafadhali ije jukwaani

fe75c414467a438ac210d6d7a8653a72.jpg
 
Tulipo fikia sasahivi hata mtu akikukuta unazama au unapatwa na balaa lolote badala yakukuokoa yeye anakurekodi ili apate cha kupost huu ni zaidi ya ujinga wa mwendo kasi
 
Back
Top Bottom