BabaTina
JF-Expert Member
- Aug 29, 2008
- 429
- 574
Wanajamii kuna video inaenda viral huko Facebook ya mama mmoja akionekana kumnyanyasa mtoto mdogo mwenye umri wa kati ya miaka2-3.
Katika video hiyo jimama moja lenye roho ya kutu kushinda shetani limekalia siti huku likionekana kumsimamisha mtoto yule ashike Bomba wakati lenyewe limestarehe.
Mbaya zaidi mtoto yule akawa anashikwa na usingizi hivo mtoto akawa anajaribu kumuegemea jimama hill ambalo bila chembe ya huruma likawa linamsukumiza mtoto yule ili asisinzie.
Ni hakika mtoto yule kapata mateso makubwa sana sana!
Lakini pia najiuliza huyu mtu aliyekuwa unarekodi alishindwa vp kuchukua hatua wakati mtoto yule akipata mateso Yale. Binafsi nimeona kijana huyu ambaye kaposti hiyo video hapo kwenye ukurasa wake wa FB naye pia anaroho mbaya kama ya jibibi lile. Alipaswa kumuokoa huyo mtoto.
Kwa wanaojua kutumia teknolojia plz naomba muichote hiyo video muiweke hapa jukwaani ili kila mtu ajionee ushetani ule na Habari hii iwafikie maafisa wote wa usalama wa RAIA na haki za watoto popote pale walipo huyu jibibi awekwe nyuma ya nondo
Hii ni screen shot ya video na jina linaloonekana ni la muhusika aliyepost hiyo video wanaoweza kuichota waichote Tafadhali ije jukwaani