Mtoto ana mwaka 1 na miezi 4, mama yake ana ujauzito wa mwezi 1

Mbavu za Mbwa

JF-Expert Member
Jan 2, 2011
303
154
Wadau habari zenu mke wangu ana mtoto wa mwaka mmoja na miezi minne (miezi 16), tena alijifungua kwa operesheni na sasa amepata tena ujauzito.

Nisaidieni
*Je, kuna madhara yoyote anayoweza kuyapata mtoto huyu mwenye mwaka na miezi minne anayoweza kuyapata? Maana bado ananyonya.

*Nifanyaje ili mke huyu, mtoto wangu na kiumbe kilichopo tumboni waweze kuwa imara (Healthy)?

Tafadhali, wadau wenye uzoefu na utaalamu
 
Wote mama na mtoto wapate lishe bora na muda wa kupumzika. Tenga muda wa kucheza na mtoto kuanzia sasa na hata mdogo wake akizaliwa.

Kuna cases nyingi za emotional neglect zina affect watoto katika makuzi na wazazi wanazifanya bila wao wenyewe kufahamu.
 
Asante sana kwa ushauri
 
wala usimwachishe mkuu kunyonya sijui hizi myth watu wanaziibua wapi !mie nilipata mimba ya 2 mtoto mdogo ananyonya dk wa watoto akaniambia nile vizuri na ninyponyeshe had mimba ikifika miez 7 ! nikahis nitamuua mwanangu jaman monthly mtoto akawa anapanda kgs clinic !na hakudhurika chchte kile !we mletee mkeo vyakula hasa matunda na mamboga mboga ale tu aendelee kunyonyesha !marufuku machips !
 
Mama mtoto ale vizuri, asiache kumnyonyesha mtoto, na atakua vizur tu! Bora yako ww, mtoto mkubwa kabisa huyo!!
 
Huku nilipo watu wanabeba mimba hata mtoto akiwa na mwezi mmoja, within one year mwanamke anazaa mara 2.
Wangu alibeba mimba mtoto wa kwanza akiwa 4 months.
 
Wadau habari zenu.
Mke wangu ana mtoto wa mwaka mmoja na miezi minne (miezi 16), tena alijifungua kwa operesheni na sasa amepata tena ujauzito.

Nisaidieni
*Je, kuna madhara yoyote anayoweza kuyapata mtoto huyu mwenye mwaka na miezi minne anayoweza kuyapata? Maana bado ananyonya.

*Nifanyaje ili mke huyu, mtoto wangu na kiumbe kilichopo tumboni waweze kuwa imara (Healthy)?

Tafadhali, wadau wenye uzoefu na utaalamu
Amepata umempa mkuu??
 
Mke inabidi awe kwa uangalizi wa karibu na dr

Ila ulishindwa kabisa kumwaga nje au kutumia condom?
Mbona hamuwahurumii hao wake zenu????
 
Iko hivi naona wengi mmechangia upande wa mtoto tu. Kwa mama wa operation angalau angekuwa na miaka miwili ama 3 ,nilishuhudia Dada mmoja baada ya kujifungua! kwa operation mtt wa kwanza akabeba mimba mtt akiwa na mwaka na nusu, ile mimba alivyofikisha miezi mitano uzito wa mtt tumboni ukawa unasababisha anaumwa sana kwenye jeraha la operation iliyopita akawekwa bed rest miezi saba wakatoa mtoto kabla ya siku za mtoto maana mama alikuwa anapata maumivu makali mno, kidonda kilichopita kikawa na dalili za kuchanika kwa ndani..mtoto alitolewa kwa kisu tena,, hiyo nilishuhudia,

Siombei baya limkute ila aende hosp kubwa kwa ushauri zaidi na check up za mara kwa mara.

Angalizo: wakati mwingine ni vyema kuwa na Huruma na mkeo, operation ni nusu ya kifo..vyema kusubiria angalau miaka 3 kisha unajaza tena.

Mungu awatie nguvu nyote.
 
Wote mama na mtoto wapate lishe bora na muda wa kupumzika. Tenga muda wa kucheza na mtoto kuanzia sasa na hata mdogo wake akizaliwa.

Kuna cases nyingi za emotional neglect zina affect watoto katika makuzi na wazazi wanazifanya bila wao wenyewe kufahamu.
Ni kweli kabisa
 
Ni sawa tu.
Mshukuru Mungu usikwazike kabisa kuwa na furaha.. kuna wanaobeba hata watoto wana miezi kadhaa na hakuna tabu. Aache kunyonyesha kama bado anafanya hivyo.
 
Mtafutie mtoto maziwa mbadala, ili mama aelee hiyo mimba vizuri, jamani tutumieni njia za uzazi wa mpango, nando mana zipo kuzuia vitu kama hivyo.
 
Back
Top Bottom