Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,339
- 51,882
MTOTO ANAHAKI YA KUIJUA ASILI YAKE.
Anaandika Robert Heriel.
Hakuna sababu yoyote inayozuia na kumnyima Haki mtoto kuijua Asili yake.
Mtoto lazima amjue Baba yake mzazi,
Mtoto lazima ajulishwe mama yake Mzazi.
Hiyo ni Haki ya Mtoto.
Mtu ili ajitambue lazima atambue asili yake. Mtu ambaye haijui asili yake kamwe hawezi kujitambua, atajitambuaje Kama hajui alipotoka, kumaanisha hajui alipo na Kule anapoenda.
Wazazi hasa wa kike waliofunzwa wakafunzika, wenye maadili na wenye ukike kiasili kamwe hawawezi kumficha mtoto Baba yake hata Kama wangefarakana vipi na Baba Mtoto.
Inawezekana kabisa Mama anaweza kuogopa kumwambia mtoto Bab yake halisi Kwa sababu kadha WA kadhaa, mathalani;
1. Kubakwa
2. Kujamiiana na Ndugu wa karibu, au Baba mzazi au Baba Mkwe.
3. Kufanya umalaya na wanaume wengi Kwa mara moja.
4. Mwanamke kufanyiwa mambo mabaya na Baba Mtoto, hivyo kujenga chuki. Miongoni mwa sababu zingine.
Kimsingi sababu hizo hapo juu na zingine hazimzuii Mama kumuambia Mwanaye Asili yake, asili ya kuzaliwa kwake, mama lazima amwambie mtoto asili yake ikiwa anampenda Kwa dhati yote.
Ingawaje lazima mzazi/Mama aangalie umri sahihi wa kumwambia mtoto wake ili isije ikamuathiri kiakili, kiroho na kihisia.
Mtoto akishakuwa mkubwa mwenye umri wa kutaka kuoa, kuanzisha familia ndio umri sahihi wa kumwambia mtoto Baba yake halisi, ili kuiweka historia yake Sawa pindi aanzishapo ukoo wake.
Umri huo ni umri mkubwa kabisa, mtoto mwenye miaka 25 kuendelea anajielewa, anajua mambo mazuri na mabaya ya Dunia, hivyo kumuambia mtoto asili yake ni ipi hata Kama inaumiza itamsaidia zaidi kuliko kumficha ambapo sio tuu itamuumiza yeye Bali utaumiza mpaka watoto wake(wajukuu zako) na kizazi chake chote.
Mtoto ndio ataamua aendelee na majina yako(upande wa mama) au afuatane na ukoo wa Baba.
Hakuna ubaya mtoto kujua asili yake ni matokeo ya kubakwa Mama yake(zingatia umri wa mtoto hasa akiwa mtu mzima) hakuna ubaya wowote mtoto kujua yaliyotokea.
Ni kweli yanaumiza lakini tuufiche ukweli?
Ukweli haufichwi,
Ukweli ukifichwa unatabia ya kuumiza na kudhalilisha huko mbeleni, ukweli unatabia ya kuumbua watu.
Pesa inanguvu zake lakini kamwe pesa haishindi asili.
Kumsomesha mtoto hakukufanyi mtoto awe wako
Narudia, hakuna sababu yoyote ya kumzuia Mama kumnyima mtoto wake kujua asili yake.
Hapo ni ishu ya Umri tuu WA Mtoto, akishakuwa mtu mzima mtoto aambiwe ukweli hata Kama unaumiza kiasi gani. Huo ndio utuuzima wenyewe