Mtoto ana haki, lakini pia ana wajibu. Je, wajibu wa Mtoto ni upi?

Status
Not open for further replies.

Rahma Salum

Member
Sep 7, 2020
30
59
Pamoja na haki za kulinda ustawi wa mtoto, kwa mujibu wa sheria ya mtoto ya 2009 mtoto atakuwa na wajibu na jukumu la;

(a) Kufanya kazi kwa ajili ya mshikamano wa familia.

(b) Kuwaheshimu wazazi, walezi, wakubwa wake na watu wazima muda wote na atawasaidia pale inapohitajika.

(c) Kuhudumia jamii yake na taifa lake kwa uwezo wake wote kimwili na kiakili kadiri ya umri na uwezo wake.

(d) Kutunza na kuimarisha mshikamano wa jamii na Taifa.

(e) Kutunza na kuimarisha mambo mema katika utamaduni wa jamii na Taifa kwa ujumla katika uhusiano na wanajamii au taifa
 
Mitoto mingi ya siku hizi ni mivivu na inapenda starehe wakati hela haina..!!

Toto limemaliza form four linalala hadi saa tano, linaamka linakunywa chai linaoga linakwenda kuzururaa kwa washikaji zake, hata kukata majani kutunza garden haliwezi..afu linawabana wazazi litafutiwe shule ng'ambo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom