Mtoto Amuuwa Mwenzake Kwa Jiwe Pemba: Ni Katika Ugomvi Wa Soka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto Amuuwa Mwenzake Kwa Jiwe Pemba: Ni Katika Ugomvi Wa Soka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Junius, Oct 6, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  MTOTO wa umri wa miaka 14 Samir Faraj Kheir anashilikiwa na Jeshi la Polisi kutokana na kumuuwa mwenzake Khalfan Zaidi Abadi (14) kwa kumlenga jiwe la kichogo na kumsababishia kifo hapo hapo.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Yahya Rashid Hemed (Bugi) amelithibitishia Mwananchi Jumapili kwamba ni kweli mtoto huyo amefariki jana majira ya saa 8 mchana baada ya kupigwa jiwe na mwenzake baada ya kutokea mabishano ya mchezo wa mpira wa miguu.

  “Hawa watoto walikuwa wakicheza mpira lakini nadhani timu moja ilifungwa kwa hiyo timu ya pili ikaona imechezewa faulu ndio wakaaza kurushiana mawe na huyu mmoja akampiga ndipo lilipompata na kufariki hapo hapo kwa sababu alipigwa eneo la nyuma cha kichwa yaani kichogoni na alipotez adamu nyingi” alisema Kamanda Bugi.

  Amesema wakati watoto hao ambao wote ni wanafunzi wa shule ya msingi wakicheza mpira kuna timu moja ilifunga time nyenzake na ndipo mtoto timu moja ilianza kubishana na timu nyengine na kuanza kusababisha ugomvi wa kurushiana mawe ambapo Samir alirusha jiwe na kumrushia Khalfan ambapo lilimpata jiwe la kichogo na sehemu iliyotoboka ilikuwa ni ndogo lakini ametoka damu nyingi kichwani.

  Kamanda Bugi alisema baada ya kurushiwa jiwe la kichogo mtoto huyo alianguka chini ya kutoka damu na kuzimia hapo hapo na kukimbizwa hospitali ya Wete lakini alipofika alikuwa ameshafariki dunia.

  “Tunasema ameguswa katika pressure point maan akuna sehemu hizo zikiguswa tu mara unaweza kupiteza fahamu au kufa kabisa nay eye hilo jiwe limempata katika sehemu hiyo na ndipo alipomalizika kwa sababu wakati daktari anamuangalia ameseme ameshafariki zamani” alisema Kamanda Bugi.

  Watoto hao wote ni wakaazi wa Bopwe Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba ambapo hadi sasa Samir anashikiliwa na jeshi la polisi wakati Khalfan amezikwa leo mchana kijijini kwao Wete.

  Kamanda Bugi amesema wanamshilia kwa sababu za kiusalama kwa kuwa hivi sasa bado kuna joto kutokana na kifo cha mtoto mwenzake hivyo kama jeshi la polisi lazima lilinde usalama wa mtoto huyo na wanatarajiwa kumfikisha katika mahakama za watoto jumatatu au jumanne baada ya kumamilika kwa uchunguzi wa kina.

  “Sisi tunamshikilia hapa kituoni kwetu kwa ajili ya uslalama wake lakini huyo hapa na tumeshampa chai amekunywa tu vizuri lakini tunasema ameuwa bila ya kukusudia maana kwa kuwa walikuwa wanacheza na keshi yake itapelekwa katika mahakama za watoto nadani jumatatu” alisema Kamanda.

  Amesema hivi sasa mtoto huyo baada ya kuelezwa kwamba mwenzake aliyempiga jiwe amefariki amekuwa akilia sana na kugoma kuongea kutokana na huzuni alizokuwa nazo.


  SOURCE: ZANZIBAR YETU WEB BLOG.
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Du, inasikitisha kweli.
   
 3. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2009
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Hivi sheria inasemaje kutaja jina la mtuhumiwa chini na miaka18??? Jamni waandishi wa habari hebu nifafanulieni juu ya hili..
  Pole kwa wafiwa nafikiri ni kosa la kuua bila kutegemea!!
   
 4. S

  Semjato JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2009
  Joined: Jun 26, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  maskini..inahuzunisha!
   
 5. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  mhh jamani yani cjui nisemeje....inauma sana!
   
 6. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,364
  Likes Received: 3,129
  Trophy Points: 280
  asalamaleiku walahi.....amembonyeza kizenji mwenzake?
   
Loading...