Mtoto amefia tumboni akiwa na miezi saba, je haya maelezo niliyo pewa hospital ni sahihi na ni bora kwa afya!?

Poleni Sana.
Inaonekana sheria zinatofautiana, maana kama nchi nyingine wanaweka maslahi ya mzazi/mama mbele zaidi.

Nikuvumilia tu, ila anahitaji uangalifu wa karibu kutoka kwa mume na ndugu....

Asije kukutana na wasiojua wakamuuliza....eehh naona tumbo linazidi kukua, hongera lini unatuletea mtoto?
Hii kauli inaumiza na anaweza kukosa jibu lakumpa mtu inategemea mko na ukaribu upi.

Mungu amtangulie amalize hiyo safari salama na ampe nguvu na afya ya kujaribu tena kubeba ujauzito.
Hawakutoa Option, maelezo niliyo toa ndio tuliyopewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaogopesha kama hospitali ndani ya nchi Moja...zinakuwa na utaratibu tofauti juu ya afya ya mgonjwa....
Najua ni utaratibu ulikuwepo mda, ila baadhi ya nchi umeanza kubadilisha hizi taratibu, kama sikosei Israeli ni mojawapo...

Ni bora mama angekuwa hajui ikamtokea akipata uchungu akajifungua nakugundua hivyo kuliko kumwacha aendelee kuteseka kiakili na baadae aanze upya kuugulia maumivu baada ya maziko...

Nikwavile sio jambo linalotokeaaga kila mara ndio maana hatusikii wanawake/familia wakilalamika.
Huo labda ni utaratibu wa hospital za serikali nchini tu!
Kwa hospitali za binafsi mara tu baada ya kujua hali hiyo wangemshauri wakitoe mara moja!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kimsingi kiumbe tumboni huwa hakiozi haraka na hizo 14 inawezekana ila kama itashindikana itabid wamuongeze uxhumgu kwa njia ya dawa ila pia wanaweza mfanyia c section yote kunusuru hari ya mama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Poleni Sana.
Inaonekana sheria zinatofautiana, maana kama nchi nyingine wanaweka maslahi ya mzazi/mama mbele zaidi.

Nikuvumilia tu, ila anahitaji uangalifu wa karibu kutoka kwa mume na ndugu....

Asije kukutana na wasiojua wakamuuliza....eehh naona tumbo linazidi kukua, hongera lini unatuletea mtoto?
Hii kauli inaumiza na anaweza kukosa jibu lakumpa mtu inategemea mko na ukaribu upi.

Mungu amtangulie amalize hiyo safari salama na ampe nguvu na afya ya kujaribu tena kubeba ujauzito.
Amina

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmm ni kumtesa tuu..
Kunabndugu yangu mkewe ilitokea kama huyuhuyu walipogundua mumewe na baadhi ya ndugu waliambiwa yule mjamzito alichomwa sindano hata nusu saa haijaisha uchungu ulimjaa akazaa na tukaenda kuzika siku ile ile.
 
Watu humu wanaona ushauri huu kwa hisia umetoka hospitali ya serikali kwa nadharia ya kwamba hawajali.

Ila kuna vitu vingi vinafanyika hospitali za binafsi si kwa maslahi ya mgonjwa bali kwa maslahi ya hospitali.

Na kwa sababu wengi tunaaminishwa hivyo tunaamini huko ndiko salama, si kweli.

Hilo jambo la kawaida kusubiri.
Kwa sababu akianzishiwa uchungu ikaleta shida inabidi azalishwe kwa operation kitu ambacho ni shida kubwa katika sura zote.

Ukianza wenyewe chance za kujifungua bila shida ni kubwa zaidi ingawaje vyote vinawezekana.

Wewe ungekuwa mama ungejisikiaje kubebelea kiumbe mfu kwa wiki mbili?
Binafsi nisingeweza

Hospital wangempa options zikiambatana na sababu za kila option
Mama atachagua mwenyewe!

Kwa hiyo hospital ikishakuwa ni ya serikali basi daktari ndiye msemaji wa mwisho
 
Fanya fasta wakaichomoe kabla mama mjamzito hajapata infections, fasta yaani. Huyo doctor inabidi achukuliwe hatua kwa kuhatarisha maisha ya mama mjamzito, yaani mtoto aendelee kuoza tu huku mama akisubiri.
Habari za Mda huu wakuu wote humu ndani,

Ni matarajio yangu weekend inaenda swadacta na mapumziko yapo sawa sawia

Naomba msaada juu ya swala lililo mtokea Shemeji yangu (Mke wa kaka yangu),

Shemeji yangu huyu yeye ni mjamzito na ujauzito wake ulifikia miezi saba,alihisi mtoto apigi tena tumboni na akawa anahisi maumivu ya kichomi tumboni na hata akifanya shughuli za kuinama ( kama kufagia,kuosha vyombo n.k) alikua anahisi maumivu makali sana, Hivyo akapata wasiwas na kuamua kwenda hospitali kwa ajiri ya kufanya Ultra sound,

Bahati baya zaidi majibu yakatoka kuwa mtoto amefariki, kwasababu alienda ktk zahanati tuu, akashauriwa aende cliniki aliyokuwa ameanza kwenda ili akapewe rufaa ya kwenda hospital kubwa kwaajiri ya kwenda kuzalishwa na mambo kama hayo,

Kweli alipewa rufaa na kwenda huko hospital kubwa, baada ya kufika huko waliziona zile documents zote na kuthibitisha hilo, lakini sasa waka mwambia, madhari mtoto amefariki tumboni, hivyo uchungu huwa unakuja wenyewe automatic,

Hivyo wamempa siku 14 na kumwambia endapo zikamaliza hizo siku kumi na nne kama hajapata uchungu aende wakamzalishe, leo ni siku ya tano hana dalili zozote za uchungu, sasa nilikuwa naomba msaada kwa nyinyi wataalamu,

Je hii ya Mama mjamzito kukaa na kiumbe kilichokufa tumboni zaidi ya wiki sasa haitaleta madhara ya kiafya kwake baadae!? kama vile kuoza kwa mtoto na baadae kuoza kwa kizazi n.k

Lkn pia Je ni kweli lazima apewe hizi siku kumi na nne kwanza? ili apate uchungu mwenyewe!?

Mwisho kabisa Je kunauwezekano wa njia nyingine kutumia zaidi ya kusubiri hizi siku 14!?

Natanguliza shukrani za dhati.
Ahsante.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ungekuwa mama ungejisikiaje kubebelea kiumbe mfu kwa wiki mbili?
Binafsi nisingeweza

Hospital wangempa options zikiambatana na sababu za kila option
Mama atachagua mwenyewe!

Kwa hiyo hospital ikishakuwa ni ya serikali basi daktari ndiye msemaji wa mwisho
Ni kweli kupewa option ni jambo muhimu. Mara nyingi nafasi ipo. Lakini si mara zote huleta matokeo chanya.
Nawajua wengi walokufa kwa kukataa ushauri wa daktari. Nawajua wengi ambao walienda fanya ndivyo sivyo baadaye. Nawajua pia waliopotoshwa.

Humu kuna wengi professional wameshauri kuwa asubirie. Maana yake utaratibu huu ni bora zaidi kwa mama kwa ujumla wake kitiba. Madhara ya kisaikolojia na kimwili huzingatiwa wakati hizi taratibu zinakubaliwa. Pia hali ya mama, ukubwa na umri wa kiumbe unazingatiwa.
Inawezekana baadaye liwe jambo la ajabu lakini kwa sasa kwa mazingira yetu ya tiba ni salama zaidi.

Kuhusu kuweza, nikuhakikishie tu ni wengi wanaweza kuliko wanaoshindwa. Hata hivyo huambiwa wakiona hali tofauti warudi hospitali. Milango iko wazi kama anajisikia tofauti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom