Mtoto amefia tumboni akiwa na miezi saba, je haya maelezo niliyo pewa hospital ni sahihi na ni bora kwa afya!?

Jemedal_bin_chichi

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
539
574
Habari za Mda huu wakuu wote humu ndani,

Ni matarajio yangu weekend inaenda swadacta na mapumziko yapo sawa sawia

Naomba msaada juu ya swala lililo mtokea Shemeji yangu (Mke wa kaka yangu),

Shemeji yangu huyu yeye ni mjamzito na ujauzito wake ulifikia miezi saba,alihisi mtoto apigi tena tumboni na akawa anahisi maumivu ya kichomi tumboni na hata akifanya shughuli za kuinama ( kama kufagia,kuosha vyombo n.k) alikua anahisi maumivu makali sana, Hivyo akapata wasiwas na kuamua kwenda hospitali kwa ajiri ya kufanya Ultra sound,

Bahati baya zaidi majibu yakatoka kuwa mtoto amefariki, kwasababu alienda ktk zahanati tuu, akashauriwa aende cliniki aliyokuwa ameanza kwenda ili akapewe rufaa ya kwenda hospital kubwa kwaajiri ya kwenda kuzalishwa na mambo kama hayo,

Kweli alipewa rufaa na kwenda huko hospital kubwa, baada ya kufika huko waliziona zile documents zote na kuthibitisha hilo, lakini sasa waka mwambia, madhari mtoto amefariki tumboni, hivyo uchungu huwa unakuja wenyewe automatic,

Hivyo wamempa siku 14 na kumwambia endapo zikamaliza hizo siku kumi na nne kama hajapata uchungu aende wakamzalishe, leo ni siku ya tano hana dalili zozote za uchungu, sasa nilikuwa naomba msaada kwa nyinyi wataalamu,

Je hii ya Mama mjamzito kukaa na kiumbe kilichokufa tumboni zaidi ya wiki sasa haitaleta madhara ya kiafya kwake baadae!? kama vile kuoza kwa mtoto na baadae kuoza kwa kizazi n.k

Lkn pia Je ni kweli lazima apewe hizi siku kumi na nne kwanza? ili apate uchungu mwenyewe!?

Mwisho kabisa Je kunauwezekano wa njia nyingine kutumia zaidi ya kusubiri hizi siku 14!?

Natanguliza shukrani za dhati.
Ahsante.

YALIYOJIRI HOSPITALI (UPDATES)

Kwanza awali ya yote nitoe shukrani na dhati kabisa kwa wote mliokuwa mmechangia ktk uzi huu, ushauri wenu niliupokea kwa mikono miwili, mlitoa ushauri nikaupokea kisha nikajiridhisha ni nini cha kufanya kulingana na ushauri husika,

Nisema tuu kwanza ile niliyo andika uzi nilisema ilikua siku ya 5, hii sikuwa sahihi,ile ilikua ni siku ya 8 na siku 14 ilitimia jana, Niseme tuu niliufata ule ushauri kuwa nisubiri mpaka hizo siku 14 zitimie kama tulivyo elekezwa ndio niende tena,

Jana JUMAMOSI ndio ilikua siku ya 14 hivyo tulienda tena hospital, baada ya kuwapa maelezo kuwa tumesubiri kwa siku 14 mlizo tupa lkn uchungu haujaja hivyo tumeruka kama mlivyo tuelekeza,

TULIAMBIWA TWENDE TENA NYUMBANI TUKASUBIRI SIKU 14 ZINGINE MPAKA UCHUKU UJE WENYEWE( kwa ujumla wake zingelikua siku 28)

Tuliona sasa hii hali si hali ya kawaida, tuliamua kuondoka na kwenda hospitali binafsi, kufika kule tukaeleza hali halisi toka mwanzo kabisa mpaka kufika tulipo fikia, Dactari yule wa ile hospital binafsi alionesha masikitiko ya hali ya juu, hivyo akasema Mgonjwa wetu atapatiwa huduma na kwa uwezo wa Mungu atakua salama,

Kwanza ilibidi afanyiwe tena Ultra sound ndipo shughuli zingine ziendelee, alifanyiwa Ultra Sound na kubaini kuwa kiumbe kile mule tumboni kimepoteza miezi miwili, yaani mwanzo kilikua na miezi 7 lkn jana kikakutwa na miez 5 na pia kilikua kimeanza kuharibika ngozi, Dactari alituambia kupungua kwa miezi kwa kiumbe hicho ni suala la kawaida kama kimefia tumboni, Hivyo alipewa kitanda na masuala ya utabibu yalianza

Ilimchukua masaa 7 mpaka 8 akajifungua kwa njia ya kawaida.

Kama Hospital binafsi suala linawezekana kwanini hizi hospitali za serikal, ambazo ndio kimbilio la wengi kulingana na vipato linashindikana!??

SERIKAL HII INAHITAJI KUJALI WATU WAKE,SIO KUWEKA TARATIBU ZA HOVYO KWENYE MASUALA YA AFYA YA WATU WAKE.

Ahsanten sana na niwashukuru wote kwa pamoja.
 
Aisee poleni sana ila mi nnavofaham kama kiumbe kimefia tumboni mama hupewa dawa ya kuongeza uchungu haraka ili aweze kukitoa nje. Sasa swala la kwamba uchungu utakuja wenyew sijuwi kwa kweli.Kwanza Mama itamuathili ki saikolojia kukaa na kiumbe tumboni ambacho anajua hakina roho tena.Ila wajuzi watakuja zaid mi so mtaalam

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usikute kuna Watu wenye Mamlaka Wizara ya Afya wanafungua Uzi wanafunga na kwenda Jukwaa lingine....

Ningekua nna Mamlaka ningehakikisha namtumbua huyu Doctor/Nesi aliyetoa Maelekezo tajwa hapo juu!

Wameua watu wengi bila kujari kuwa Mishahara yao inatokana na Kodi za wakiwemo Wajawazito na Wagonjwa.....

Shenzi zao wenye Mamlaka!
 
Aisee mpaka nimesisimkwa na mwili wote, ndugu yangu kwa kifupi rudini hospital kiumbe kikatolewe.
Nilichoshuhudia mwaka jana kupoteza mtu kwa ushaur kama uliopewa nimetokea kuogopa hata kumuangalia mjamzito wa aina yoyote.
Nenda hospital kubwa zaid huyo dada akasaidiwe hicho kiumbe kitoke, msikubali kusubir siku 14(sina uhakika kama kitaalam ni sahihi)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee mpaka nimesisimkwa na mwili wote, ndugu yangu kwa kifupi rudini hospital kiumbe kikatolewe.
Nilichoshuhudia mwaka jana kupoteza mtu kwa ushaur kama uliopewa nimetokea kuogopa hata kumuangalia mjamzito wa aina yoyote.
Nenda hospital kubwa zaid huyo dada akasaidiwe hicho kiumbe kitoke, msikubali kusubir siku 14(sina uhakika kama kitaalam ni sahihi)

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu yangu wee, Ahsante sana na ndio sababu nikakimbilia kuja kupata ushauri

Lkn cha kuzingatia ni kuwa Hospital tulioenda ndio hospital kubwa hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ni kweli kabisa na utaratibu ni huo huo. Madhara yataweza kutokea kama kisipotoka kwa hizo wiki 2.
Aendelee kusubiri.
 
Usikute kuna Watu wenye Mamlaka Wizara ya Afya wanafungua Uzi wanafunga na kwenda Jukwaa lingine....

Ningekua nna Mamlaka ningehakikisha namtumbua huyu Doctor/Nesi aliyetoa Maelekezo tajwa hapo juu!

Wameua watu wengi bila kujari kuwa Mishahara yao inatokana na Kodi za wakiwemo Wajawazito na Wagonjwa.....

Shenzi zao wenye Mamlaka!
Wewe unafahamu SOP za missed abortion?
 
Kama inawezekana kumzalisha baada ya siku 14, ni nn kinasababisha asizalishwe kabla?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndo utaratibu ulivyo.
Kila kitu kina umuhimu wake, siku 14 zijipita kama ilishindikana ataenda hosp, then utaratibu wa kuzalisha utaanza, ukishindikana utaenda utaratibu mwingine.
Sasa unaporuka step moja, shida ikitokea ama ikishindikana next step ni way forward na ni more aggresive than previous.
Thats all I have to say.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom