Mtoto ambaye hakunyonya maziwa ya mama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto ambaye hakunyonya maziwa ya mama

Discussion in 'JF Doctor' started by MAKALA, Oct 6, 2010.

 1. M

  MAKALA Member

  #1
  Oct 6, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 45
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Habari
  naomba kujua ikitokea kua una mtoto ambaye hakunyonya kabisa maziwa ya mama, yaani ambaye anakulia kwa kutumia maziwa ya kopo, ni aina gani ya lishe? (chakula) inashauriwa kumpa ili kumuimarisha zaidi kiafya ukiacha hayo maziwa ya kopo anayotumia.mtoto umri wake ni miezi sita.
  ahsante.
   
 2. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwa umri wa miezi6 unaweza kumwanzishia uji wa lishe lakini kwa kuanza na mchanganyiko wa vitu vichache kadri anavyozoea unaongeza ingredients nyingine. unaweza kupata unga uliotengenezwa tayari kwa watoto madukani au kuandaa vitu na kwenda kusaga mashine.
  Vitu vinavyochanganywa kwenye unga wa lishe ni mahindi yasiyokobolewa, ulezi, karanga, ngano, mchele, soya na dagaa ukipenda ( wapo ambao hutumia uwele/mtama badala ya ulezi) Hii ni kwa moni yangu tu ndugu waweza pata maoni tofauti, kila la kheri!
   
 3. P

  Paul S.S Verified User

  #3
  Oct 9, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  kwa kuanzia wiki2 za mwanzo mpe uji mwepesi sana na ulio iva sana wa sembe changanya na maziwa ya ngombe au yakopo
  baadae mpe uji dona na maziwa. kisha kila mwezi ongeza kimojawapo kama mchangiaji wa juu alivyo vitaja.
  kumbuka kutengeneza uji mwepesi sana na uliopikwa mda mrefu kusaidia mmeng'enyo tumboni.
  chuja unga kupata unga laini sana kabla ya kpika
   
 4. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #4
  Oct 9, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  kule kijijini mtoto wa miezi 6 wanakandamiza na ugali................... ukilicheki toto limenenepa utashangaa
   
Loading...