mtoto aliyeuawa, njaa,umasikini na frustration ndo chanzo.

Mwana wa Mungu

JF-Expert Member
Aug 14, 2008
1,003
83
Jamani, mtoto aliyepigwa na baba yake kule Musoma hadi kufa kwasababu ameiba mayai ya shs.300, ni kitendo cha ajabu. wengi wamerespond kwenye hii kitu kuwa, ni kwasababu wakurya ndio tabia yao kupiga. Mimi nimekuja na jicho la tofauti, MTOTO YULE ALIIBA KWASABABU ALIKUWA NA NJAA. Baba yake si ajabu alikuwa na frustration za maisha magumu.

maisha bora kwa kila mtanzania lini? Kama at least hao wananchi vijijini wangesaidiwa kwa pesa za fisadi mmoja tu, wangefuga kuku wengi wa mayai, baba angemwekea mtoto yule trei kibao ale mayai hadi achoke. KWENYE NYUMBA ZA MAFISADI PAPA, kuna kila kitu(kwa hela za watz), kuna mayai, kuna majuis, manyama, mapochopocho kila kitu. hela hizi zingekuwa kwenye mgawanyo sahihi, kwakweli mtoto yule asingeuawa kwa kuiba mayai nyumba ya pili, angekuwa amekula mayai hadi ameridhika nyumbani. nilishawai kuishi kijijini, wakati mwingine unarudi toka skuli unakuta wazazi wameenda shamba hawajaweka msosi, upige deshi hadi jioni. msosi hamna. ndio maana watoto huwa wanaiba kwasababu wanaona njaaa. vita dhidi ya mafisadi pekee ndio itakayoondoa rushwa na ubadhilifu tz ili at least mwananchi wa kawaida apate chakula cha kutosha, watoto wetu wasiwe na njaa hadi kufikia kuiba mayai. wazazi wamekuwa na frustration za ugumu wa maisha, kina mama wanafariki mahospitalini wakati wa kujifungua, barabara hazijengwi, matatizo kibao. wakati huohuo mafisadi wanajenga mijengo dubai na souzi na ulaya na marekani. hivi watz tutafunguka macho lini, HAWA JAMAA CHINI YA KUMI TU NDO WAMETUZIDI NGUVU, yaani tufisadi tuchache hivi ndo tumeshikilia nchi, watz tumeenda wapi? wametuchukua akili nini? ati, kina rostam, manji na wenzao wametuchukua akili? sasa mbona hata wakati mengi na wengine wamejitoa muhanga sisi bado tunatoa mimacho tu? tuandamane hawa jamaa kama sio waaminifu waadibishwe. huku mtaani watu njaa na matatizo yamewazidi kwasababu yao. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
tehetehee, topic za leo mwana wa mungu mbona unanivunja mbavu. Kusema ukweli, hiyo ilikuwa ni njaa. si ajabu mtoto alirudi home akakuta hamna msoso kama ulivyosema. ni kweli watoto wa kijijini wakati mwingine huwa wanakula mlo mmoja tu. ndio pengine aliamua kwenda vichakani kukagua kama kuna kuku yoyote alitaga mayai. akaamua kupika na kula...njaa jamani, umasikini tz umezidi sasa. mkombozi wetu ni nani? ni JK anayechukua hela Kwa Sumaiya kwaajili ya UVC?
 
siyo njaa pekee iliyomfanya aibe, inawezekana ni hamu tu ya yai. Si unajua taratibu zetu za kibongo saa zingine, hata kama mayai yapo ni ya baba tu ama watu wazima!

Tukiacha hayo, swala la kupigana tu mi silependi, iwe kwa mtoto ama mkubwa. Na inapofikia mtu anapiga mpaka mtoto anakufa akili yangu inashikwa na ganzi ya wogo na moyo unajaa simanzi. Kwa kuwa nia yangu ni kutafuta ubinadamu nabaki kujiuliza maswali, JE alikusudia kuua? Ama ndio ule upigaji wetu wa popote tu uchape watoto? Kama nia ya huyu jamaa hakuwa kuua ndio napata woga zaidi, maana watu wengi hawaelewi athari za kupiga unapokuwa na hasira maana mkono wako unaangukia popote na unaweza kuua. Jamani wale wapigaji makonde watoto, nadhani mnaona athari zake.

Kupiga mtoto si kwamba sio sahihi tu, ila unaweza ua.
 
hakukusudia kuua, ilikuwa hasira tu. yaani ile hasira na machungu ya maisha, yalikuja kuishia kwenye kumwadhibu mtoto. si yeye ila hasira ya maisha magumu. najua kwasasa yule mzazi atakuwa anajilaumu, si kwasababu anaenda jela, ila kwasababu amempoteza mtoto wake aliyemlea, akampeleka na shule kwa miaka yote hii.

watz wako frustrated na maisha magumu, kila kukicha mambo magumu. sisi wengine tunaweza kuona maisha mazuri kwasababu tunacho chakula, wengine wanatia huruma jamani, vibaka wanaongezeka kila siku. watu wanaumia.

umenifurahisha unaposema ilikuwa ni hamu, ni kwasababu hajala muda. angekuwa na uwezo kidogo,babake angemnunulia mayai ale hadi hamu iishe, kama watoto wa Rostam azizi, manji na yale mapapa, wanavyokula vizuri, wanaenda weekend bagamoyo kwenye beach, kwenda kusoma ulaya nk. Mungu saidia tanzanial.
 
mafisadi wanaumiza mioyo ya watz. watu wana hasira hadi wanaua watoto wao bila kujipendea.
 
Hivi hamjui kuwa miaka ya hivi karibuni watanzania wamekuwa na HASIRA sana mioyoni mwao?? kama unabisha angalia watu wanavyomshambulia kibaka ambapo hata hawaulizi nani kaibiwa na alichoiba kiko wapi. wakimaliza kazi yao (kuua) kila mmoja anasambaa kivyake akijisifu alivyochangia kupunguza vibaka mjini ila hawana taswira ya aliyeibiwa na kama amepata mali yake....
Tumuombe Mungu maana haya ndiyo matayarisho ya ghasia zisizokoma kwani hata shetani huwa anaandaa mazingira kwa project zake ziwe endelevu.
 
Back
Top Bottom