Mtoto aliyepanda ndege kwenda Zanzibar bila kuonekana ametoweka tena

Update:
Mtoto ameonakana jana usiku akiwa bandarini akijiandaa na safari ya boti kurudi znz,kwa sasa yupo kituo cha polisi cha kati(Central) akipewa hifadhi.

Source:Sam Mahela_Nipashe_Radio1
 
Kwa nini mama yake hakuacha amemfunga kamba wakati anaenda kuwapokea waandishi?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Wachungaji jitokezeni,hiyo ndio nafasi ya kutuonesha hizo karama mlizopewa na Muumba.

Nashangaa mpaka leo kina Mzee wa upako, Gwajima, Lwakatare, Kakobe, Efatha n.k wapo tu badala ya kuonesha cheche zao ili tuwaamini vizuri. Wao huponya wale wagonjwa fake tu wanaokuwa wamewaandaa!!! Wamponye na huyu mtoto anateseka ili tujue kama kweli wanafanya kazi
 
Awahi kwenye makanisa ya kiroho yaliyo na mungu wa kweli, naamini mungu atafanya bila kusita
 
Haya tusubiri ataibukia wapi.... Nahisu safari hii ataibukia Ferry

Ni mgonjwa wa akili tu huyo ndio maana anatoweka toweka. Halafu na watu wa airport wazembe yaani mtoto anapita check 5 za airport na ya 6 ya ndani ya ndege bila kumgundua.

Na huyo mama yake kashindwa malezi ndio maana mtoto anamtoroka toroka halafu yeye anasema anapotea.
Ni shiiiiida
 
Huyu mtoto inabidi aombewe lakini kinachonishangaza kwanini baba yake hajishughulishi na hii issue, mama mzazi wa happy alisema babake happy yupo lakini hajishughulishi na chochote kuhusu matatizo ya mtoto au huyu baba anajua kinachomsumbua mtoto na pengine anahusika na hili suala
 
Usijali ndugu yangu. Tuombe Mungu tu awe nasisi maana hapa ulimwenguni yako mengi tusiyoyaona kwa macho. Tumwombe Mungu atuokoe na yule mwovu.

Mchana mwema.

Samahani sana but huyu gwajima anasemaga vitu vikubwa sana so ulimi umeniteleza i
 
huyu mtoto atakuwa anatumiwa na wachawi na baba anaijua hiyo siri haiwezekani mtoto amepotea baba yake yupo kimya hata hangaiki hata siku ya kwenda kumchukua kule zanzibar baba yake hakwenda alienda mama yake tuu kuna siri nzito hapo baba ahojiwe na polisi ukweli utajulikana tuu
 
apigwe tu! Wakikaona viboko vihusike ni kukachapa hasa c kanajitoa ufamu
 
Kikombe cha babu,homa ya dengua,ebola,sasa huyo binti. Tanzania bwana mambo hayaishi haya na la katiba nalo bado. Sijui masiku yanayokuja tutambiwa nini? Yetu masikio na macho.
 
Kituko hiki cha binti huyu, kinatupa nafasi ya kutafakari upya;Usalama na ulinzi katika taifa letu !
 
Kongosho mambo ?
Msalimie EMT na kaka yako Nyani Ngabu maana sijawaona pande hizi.

Mie mzima. Za wikienda? Habari zilizopo ndani ya Dar ni kwamba kuna wizi wa watoto na wakubwa pia

Hutumika udanganyifu mkubwa kwa kuwapa lift za magari. Pia watoto hudanganywa kwa biskuti, pipi, nk.

Wanawake hutongozwa au huambiwa wawapeleke hao watu sehemu fulani wakidai kuwa wao wamepotea au kwa kutaka mashamba, viwanja na nyumba.

Ukikibali tuu kupanda gari yao umeliwa. Kivipi? Well, sijui.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom