Mtoto aliyekuwa akiishi na utumbo nje ya tumbo lake afariki dunia mkoani mbeya. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto aliyekuwa akiishi na utumbo nje ya tumbo lake afariki dunia mkoani mbeya.

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Nov 9, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 9, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  MTOTO ALIYEKUWA AKIISHI NA UTUMBO NJE YA TUMBO LAKE AFARIKI DUNIA MKOANI MBEYA.  [​IMG]
  Mtoto Mpeli Mathias pichani aliyekuwa akiishi na utumbo wake nje ya tumbo baada ya kuzaliwa bila sehemu ya haja kubwa amefariki dunia mkoani Mbeya.
  [​IMG]

  Mama Mzazi wa Marehemu Mpeli (Memory) Mathias, Mpeli Mwakyusa akiwa amembeba mwanae wakati wa uhai wake akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhumbili hivi karibuni.  Taarifa kutoka kwa Mama mzazi wa mtoto huyo Mpeli Mwakyusa (26) amesema mwanae huyo alifariki dunia akiwa wilayani Rungwe mkoani Mbeya na mazishi kufanyika wilayani humo juzi.

  ''Mtoto ametutoka Memory wangu, Mungu awasaidie kwa msaada wenu mwendelee kwa wengine kuwasaidia, asante'' alisema Mama mzazi wa mtoto huyo kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi alipowasiliana na mmiliki wa mtandao huu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la Tanzania Community Media Organization (TACOMO) linalojishughulisha na masuala ya kijamii.

  Amesema anawashukuru wale wote waliomsaidia kipindi cha uhai wa mtoto wake ili kuokoa maisha yake lakini Mungu ndiye mwamuzi.

  Mtoto huyo aliweza kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Peramio na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kupata michango kutoka kwa wasamalia wema akiwemo Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi.

  Taarifa ambazo zimeufikia mtandao huu wa KALULUNGA COMMUNITY MEDIA TANZANIA ni kwamba mtoto huyo alizaliwa bila utumbo mpana hivyo alikuwa akiishi kwa majaliwa ya Mungu.

  Mtandao huu unaungana na watanzania wote kutoa pole kwa ndugu jamaa na familia ya Marehemu, Mungu alitoa na sasa ametwa jina lake Lihimidiwe.

  Chanzo:
  CHIMBUKO LETU: MTOTO ALIYEKUWA AKIISHI NA UTUMBO NJE YA TUMBO LAKE AFARIKI DUNIA MKOANI MBEYA.
   
 2. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #2
  Nov 9, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Pole nyingi kwa wafiwa!! Kukosa utumbo mbana ni tatizo kubwa ..hata hivyo mtoto alijitahidi sana kupigania maisha yake!! Lakini mwishoni yote ni mapenzi ya Mungu!! RIP!!
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Nov 9, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Mwenyeezi Mungu amalaze pema peponi ameen
   
 4. ALLEX

  ALLEX JF-Expert Member

  #4
  Nov 9, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 2,046
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  poleni ndugu na jamaa pamoja na watanzania wote mliokuwa mkitoa misaada kwa kijana huyu ...
   
 5. Tausi.

  Tausi. Senior Member

  #5
  Nov 9, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pole sana mama, yote ni mipango ya MUNGU,
  kwani yeye ndiye ametoa na yeye ndiye ametwaa.
  Ni matumaini yangu kuwa MUNGU atakuzawadia kingine
  kilicho kizuri, na utasahau yale yote kwani yote ni Mitihani.
  R.I.P Baby Mpeli.
   
 6. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #6
  Nov 9, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  mungu amlaze mahali pema peponi. AMEN
   
 7. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #7
  Nov 9, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Angalau amepumzika na mateso... better to die than maisha yale.
   
 8. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #8
  Nov 9, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Pole sana Mama Mpeli!

  Sijui watawala wanapata funzo gani kwenye hili? jamii yetu imejifunza nini?

  RIP Baby Mpeli!
   
 9. H

  HERBERGONER Member

  #9
  Nov 9, 2011
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mungu amtie nguvu huyo mama memory apumzike kwa amani..............amina
   
 10. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #10
  Nov 9, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Mambo mengine unashindwa hata kuongea... Hapa ndo mtu unatambua kua you are at a better position kuliko wengine No matter how terrible you situation you think you are in.... Sad. May the angel rest in peace ....
   
Loading...