Mtoto akatwa uume wake wakati akitahiriwa- Muheza

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,266
33,039
MTOTO aliyetambulika kwa jina la Sumi Salim [10] amekatika uume wake wakati akitahiriwa kwa njia ya kienyeji huko Muheza mkoani Tanga Kutokana na maumivu makali aliyoyapata mtoto huyo wakati akijaribu kupewa tahiri hiyo mtoto huyo amelazwa kwa ajili ya matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Muheza mkoani humo. Tukio hilo lililothibishwa na jeshi la polisi lilidaiwa kutokea katika Kitongoji cha Paramba katika Kata ya Kicheba mkoani humo. Mama mdogo wa mtoto huyo ambaye alikuwa anamuuguza mtoto huyo hospitalini hapo alisema kuwa baba wa mtoto huyo alikataa ushauri aliopewa kutoka kwa mzazi mwenzake uliotaka mtoto huyo wamtahiri hospitalini. Alisema kuwa kutokana na ubishi wa baba huyo aliendelea kung’ang’ania kumtahiri kienyeji kwa kuwa alidai kutahiri kienyeji ni bei nafuu kuliko hospitali kwa kuwa hakuwa na hela. Hivyo kutokana na kauli yake hiyo alitafutwa mtaalamu wa mambo hayo na kumpeleka mtoto huyo kutahiriwa kwa njia hiyo. Alisema ngariba huyo wakati yupo katika zoezi lake hilo la tahiri kwa bahati mbaya alikosea na kujikuta akikata uume wa mtoto huyo na kumsabbishia maumivu makali sana. Kutokana na kukosea kwa ngariba huyo walifanya utaratibu wa kumkimbiza mtoto huyo hospitali na ndipo amelazwa katika hospitali hiyo wakiendelea na matibabu. Lakini ngariba huyo alipotafutwa kijijini hapo alikuwa ameishakimbia na hajulikani alipo hadi sasa na juhudi zinaendelea kumsaka ngariba huyo. http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=2461094&&Cat=1
 
Duuh poleni sana wanakwetu huko muheza.Jamani tubadilike haya mambo ya kwa ngariba ya kizamani sana..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom