Mtoto Ahukumiwa Kunyongwa hadi Kufa!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto Ahukumiwa Kunyongwa hadi Kufa!!

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Bushbaby, May 22, 2012.

 1. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  MAHAKAMA KUU ya Tanzania Kanda ya Tabora imemuhukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa Juma Mayala (23) kwa kosa la kumuua baba yake mzazi  Hukumu hiyo ilitolewa jana na Jaji Simon Lukelewa huku upande wa Mashitaka uliongozwa na Wakili wa Serikali, Magreth Ndaweka

  Jaji Lukelewa alisema kuwa, alitoa adhabu hiyo kwa kuwa mshitakiwa alipatikana na hatia ya kuumua baba yeke mzazi na nkuridhishwa na ushahidi wa hali ya juu kuhusiana nna hilo

  Ilidaiwa Mei 5, 2004 mshitakiwa alimuua baba yake Mayala Ngamba kwa kumkata kwa shoka mara tatu kichwani hali iliyopelekea kifo chake papo hapo.

  Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa,mara baada ya kufanya mauaji hayo mshitakiwa aliufukia mwili huo katika choo kisichotumika na kisha kufunika kwa mawe juu ambapo mwili huo uligundulika baada ya siku tatu.

  Awali imedaiwa kuwa mshitakiwa alifanya mauaji hayo kutokana na kuchukizwa na hali ya kunyimwa chakula na mzazi wake huyo mara kadhaa hali iliyofanya ajichukulie maamuzi mikononi kinyume na sheria

  Mayala mkazi wa kijiji cha Maskati, Wilaya ya Shinyanga

  Source: Nifahamishe

  Mytake:
  Kama kosa alilifanya mwaka 2004, mtuhumiwa alikuwa na miaka 15, je hii kesi ilisikilizwa mahakama ya watoto?


  Hawa watu wa Haki za watoto kesi hii waliisikia? au huwa wanasikia tu kesi za watoto ambao ni Ma-star?

   
 2. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  Ama hakika kisasi ni haki, anaeua na yeye auliwe, so ni haki yake kuuliwa , HAKUNA MJADALA! akiwa na miaka 15 kwani alikuwa hana akili timam? muuwaji ni muuwaji na khasa anapokuwa na akili timam na yeye lazima auliwe ! full stop!
   
 3. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2012
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Hii kesi inaleta picha gani kwa wazazi wa Lulu kung'angania kuwa lulu ni serengeti boy?
   
 4. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #4
  May 22, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Nasubiri jaji wa kesi ya Lulu atumie kesi hii kama reference kwenye kutoa hukumu......:smash::smash:
   
 5. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #5
  May 22, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,600
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  Miaka kumi na tano anaruhusiwa kuua?? utoto unaishia miaka mingapi?
   
 6. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Kamuua babaye?


  Tena anyongwe mara moja tena amecheleweshwa sana!
   
 7. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #7
  May 22, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Swahiba ....acha munkari!!! alitenda kosa hilo akiwa na miaka mingapi??
   
 8. m

  makumvi Member

  #8
  May 22, 2012
  Joined: Mar 26, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Huyu kijana alikosa busara, kwa umri wa miaka 15 aliwezaje kupata ujasili wa kumwua babaye na kumfukia kwenye shimo la choo jamani ? kweli hastahili msamaha katika hili nadhan shelia imechukua mkondo wake hapa
   
 9. Achahasira

  Achahasira JF-Expert Member

  #9
  May 22, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  navyojua mimi mwanaume anapata akili akiwa amesha balehe.naamini huyo unaye mwita mtoto alibalehe kabla hata ya kumua babake.

  na mtu anaye balehe ni mtu mzima.

  kuto fikisha miaka kumi na nane isiwe ndo sababu.
   
 10. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #10
  May 22, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,512
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  mtoto wa kiume akiwa na miaka 10 akili yake ipo poa na anajua baya na zuri na anajua kosa la kuua ..

  my take asinge hukumiwa kunyongwa ila kifungo cha maisha
   
 11. H

  Hume JF-Expert Member

  #11
  May 22, 2012
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 338
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Mleta hoja ana issue ya msingi hapa ya kujadili. Wengi naona wanatoa maoni yao kutokana na hasira ya kilichofanyika.
  Ni kweli kuwa kijana alifanya kosa kubwa sana kumuua baba yake.

  Lakini JE? suala la umri wake wa utoto wa miaka 15 lilizingatiwa wakati wa mwenendo wa kesi hadi hukumu? Jaji alizingatia umri wa mtenda kosa wakati kosa linafanyika au amezingatia umri wakati wa hukumu?

  Wanasheria watoe msaada hapa!!
   
 12. H

  Hume JF-Expert Member

  #12
  May 22, 2012
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 338
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Hiki siyo kigezo cha utoto na utu uzima. Vinginevyo zinazoitwa mimba za utotoni zisingekuwepo.
   
 13. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #13
  May 22, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Nyongelea mbali huyo :hatari::hatari:
   
 14. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #14
  May 22, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  kwani ccm wamefanya nini hapa unapotezea au
   
 15. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #15
  May 22, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Sheria inasemaje?
   
 16. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #16
  May 22, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Tatizo watu wanaanzisha thread kutaka kujadili mambo ya kisheria badala ya kuweka thread kwenye forum ya sheria wanaweka huku halafu wanaomba msaada wa kisheria. Pelekeni forum ya sheria kama mnataka msaada wa kisheria.

  Waulize wanasheria kwenye forum ya sheria.
   
 17. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #17
  May 22, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Waberoya Kuna kesi zipo mahakamani...na watetezi wa kesi wanataka Favor kisa mtuhumiwa eti ni mtoto...siwezi kujibu swali lako kwamba utoto unaishia miaka mingapi!! labda unisaidie....
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #18
  May 22, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  EMT hata hapo umechangia pia!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #19
  May 22, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Nimechangia kwa wewe kuuliza mambo ya kisheria kwenye forum habari na hoja mchanganiko?
   
 20. S

  Starn JF-Expert Member

  #20
  May 22, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 400
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Haya ndo yanayomsubiri LULU wanasubiri atakapofikisha miaka 18+ ndio watamuhukumu
   
Loading...