Mtoto afungwa mnyororo mguuni kwa siku tatu na wazazi wake

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Mtoto wa darasa la nne, Nelson Nansisi wa shule ya msingi ya Bwawani wilayani Ilala, Dar es salaam amefungwa mnyororo mguuni kwa siku tatu na wazazi wake, kwa madai ya tabia ya kuzurura hadi usiku wa manane na utoro shuleni

Tukio hilo lilifichuliwa juzi na Wasamaria wema wa maeneo ya Daimasoko Kiwalani, jambo lililoshangaza majirani ambao waliamua kutoa taarifa Polisi na kwenye gazeti hili

Licha ya kutoa taarifa polisi, walieleza kusikitishwa na tukio hilo huku baadhi wakidai mtoto huyo anafanyiwa hivyo, kwa sababu anaishi na mama wa kambo

Mwenyekiti wa Serikali za mtaa wa Minazi Mirefu Daimasoko, Ubaya Chuma alithibitisha kupokea taarifa hizo na kuzifikisha polisi ambao walifika na kukosa ushirikiano wa wananchi kukamata wahusika wa ukatili huo

"Sisi tulifanya jitihada kuwaita polisi ambao walifika wakiwa na magari mawili, lakini mama wa mtoto akakataa kufungua mlango na majirani hawakuonesha ushirikiano kwa Serikali za Mtaa wala polisi ili kubaini tatizo, mwishoni tuliondoka."alisema

Baba mzazi wa Mwanafunzi huyo, Nansisi Rashid alikiri kitendo hicho kwa kudai ni mtoto wake kuzidi utukutu na kuwasumbua jambo lililowakosesha njia mbadala ya kumwonya

"Hivi sasa nimemwandalia fomu ya kumhamishia shule moja ya Temeke ili abadilishe mazingira, anaondoka hapa nyumbani anakwenda kucheza, si kwamba anakatazwa ila kurudi kwake ni saa sita usiku, ukienda kumtafuta kwenye mabanda ya video humpati, ikafika kipindi nikasema siendi tena, ila mama yake akawa anasisitiza niende kumtafuta."alisema na kufafanua

"Juzi mjumbe alimkuta mtaani saa sita usiku, mimi nakuja kufungua mlango saa saba usiku namkuta amelala nje, jambo hilo ni hatari, kwani watu wanaweza hata kumchukua na kumpeleka kusikojulikana."

Alisema baada ya kufikia hatua hiyo, aliamua kumfunga mnyororo mguuni na kwenye kiti ili hata anapotaka kwenda kucheza aondoke na kiti chake

"Nikasema namfunga atakayekuja aniulize mimi, ndio maana hata polisi walikuja juzi na hawakuona kuwa ni tukio la kushangaza kwa sababu hakufungwa shingo,"alisema

Aliongeza kuwa mtoto wake huaga anakwenda shule, lakini hafiki, na hata shule ambazo alikuwa akisoma masomo ya ziada jioni waliamua kumfukuza

Alisema suala hilo limeshafika hadi kwenye vyombo vya habari na polisi na kwamba atashirikiana na polisi mtoto huyo atakapotoka nje na kwenda kuzurura waje kumkamata na kumpeleka mahabusu ya watoto.

Chanzo :JamboLeo
 
Huyu dogo ni mzururaji wala mama wa kambo hana kosa hapo.. Wazazi wakishindwa kumlea vixuri huyu mtoto ndio mwanzo wa kujiunga na vikundi vya kina panya road.

Baba alifanya njia nzuri sana kumzuia kwa mtindo huo jamii huwa inatafsiri tukio bila kuangalia mwanzo ulikuwaje . Wangeenda kuulizia hao wajumbe wanamuona mtoto huyo nje ya nyumba yao mpaka saa sita za usiku.
 
Nadhani mzazi ndiye aliyekosea kwa kushindwa kumjengea mwanae misingi mizuri ya malezi tangu akiwa mdogo.

Pia nina wasiwasi na akili za huyo baba kumuhamisha mtoto shule au kumfunga hizo kamba sidhani kama ndio solution.
 
Nadhani mzazi ndiye aliyekosea kwa kushindwa kumjengea mwanae misingi mizuri ya malezi tangu akiwa mdogo.

Pia nina wasiwasi na akili za huyo baba kumuhamisha mtoto shule au kumfunga hizo kamba sidhani kama ndio solution.
Mleavyo ndivyo atakavyokuwa... bila shaka mtoto kuna kitu anakikosa katika malezi, huyu baba aangalie upya ulezi wake..!
 
upload_2016-12-6_9-51-55.jpeg

71Mvf32BiPL._SL1500_.jpg

Tatizo watu wameona mnyororo ndio wanawaka ila kuna watoto bila kuwafunga hutafanya kazi yoyote nyumbani, tena wanaweza kujidhuru wenyewe. Sasa huyo mtoto gani anaenda kucheza hata hakumbuki kurudi nyumbani? Wangemfungia milango tu.
 
Mleavyo ndivyo atakavyokuwa... bila shaka mtoto kuna kitu anakikosa katika malezi, huyu baba aangalie upya ulezi wake..!
Kweli kabisa mkuu. Pia tukiangalia bado huyo mtoto ni mdogo kiumri hivyo akiamua kumbadilisha bado ana nafasi ya kubadilika.
 
Kweli kabisa mkuu. Pia tukiangalia bado huyo mtoto ni mdogo kiumri hivyo akiamua kumbadilisha bado ana nafasi ya kubadilika.
Inashangaza sana kusikia mzazi kuwa mtoto huyu amenishinda, mtoto ni darasa la nne anakushinda kwa namna gani..!
 
Hamjakutana na watoto watukutu. Hapa wengi watalalamika kwa sababu imeonekana sio mama yake mzazi. Ila hakuna mzazi atakaefurahia kuona mwanae mdogo anazurula hadi saa sita usiku asichukue hatua.
 
Back
Top Bottom