Mtoto afichua siri ya baba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto afichua siri ya baba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, May 19, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MWANAUME aliyetambulika kwa jina la Bakari [36] mkazi wa jijini Dar es Salaam, amejikuta akipeleka hasira zake sehemu mbaya na kujikuta akimjeruhi mtoto wake wa kambo kwa kummwagia chai ya moto usoni.
  Imedaiwa kuwa, mwanaume huyo alikasirishwa na kitendo cha mtoto huyo kutoa siri kwa mama wakati wakipata kifungua kinywa mezani

  Chanzo cha habari hii kilidai kuwa, mtoto aliyetambulika kwa jina la Joyce [9] alimuumbua baba yake kwa kutoa siri kwa mama yake bila kutambua kuwa anafanya kosa kutoa siri hiyo.

  Imedaiwa kuwa, mwanaume huyo mfanyanyakazi wa wizara moja nyeti nchini alikuwa na tabia ya kumsaliti mkewe toka mke wake huyo alipoanza likizo ya uzazi

  Imedaiwa kuwa mwanaume huyo alikuwa akiondoka asubuhi nyumbani kwake akiwa ameongozana na mtoto wake huyo kwa lengo la kumpitisha shuleni anaposoma na kisha yeye kuendelea na safari yake ya kwenda kazini mara baada ya kumshusha mwanafunzi huyo shuleni

  Imedaiwa kuwa, majuma matatu nyuma baba huyo alikuwa akimpitia mwanamke mwingine nyumbani kwake na kumpakia kwenye gari hilo na kuondoka nae kila siku na mtoto huyo kuona hali hiyo.

  Imedaiwa kuwa, mwanzoni mwa wiki hii, baba huyo alikuwa akimuhimiza mtoto huyo kufanya haraka kunywa chai ili waondoke na kumsisitizia kuwa anasubiriwa na mtoto huyo bila kutambua alimuuliza baba yake huyo “kwani ameshakupigia simu Yule dada? Mwambie tunampitia sasa hivi?

  Mara baada ya kutamka maneno hayo mama wa mtoto huyo alikuwa akimuliza vizuri nani amempigie simu? bila ajizi mtoto huyo alianza kuelezea mkanda kuwa huwa wanampitia dada mmoja kila siku nyumbani kwake na kuondoka nae mjini

  Mama huyo wakati akiendelea kumuhoji mtoto huyo na mtoto huyo kujieleza bila hata kujua anafanya kosa kutoa siri hiyo, ndipo mwanaume huyo bila kutambua alichukua kikombe cha chai ya moto na kujikuta akimmwagia mtoto huyo usoni

  Hata hivyo imedaiwa kuwa, mwanaume huyo aliondoka kwa hasira baada ya kuona mtoto huyo amemvunjia adabu na mama huyo alichofanya ni kuomba jirani yake amsaidie kumpeleka zahanati mtoto huyo kwa kuwa yeye alishindwa kwa kuwa alikuwa ametoka kujifungua mwezi mmoja nyuma.

  Hata hivyo imedaiwa kuwa, mwanamke huyo ni miezi miwili sasa yuko nyumbani kwa ajili ya likizo ya uzazi

  Habari hii itaendelea
   
 2. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Huyo jamaa hana busara tu na wala hakutakiwa ku-panic kwani kama anampitia mwanamke mwingine asubuhi anapokwenda kazini kuna tatizo gani? anaweza kuwa mfanyakazi mwenzie...Yeye alitakiwa kuwa mtulivu tu na kumuelewesha mkewe. Sasa amemuumiza huyo mtoto bure....:mod:
   
 3. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  source.......
   
 4. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #4
  May 19, 2011
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Infidelity rules was not applied.... sasa cheki alivyoharibu kashindwa easy task namna hii????
   
 5. D

  Domo Zege JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Huyu mwanaume hana busara hata kidogo, maskini mtoto mdogo kama huyo kupewa adhabu kama hiyo.Wazazi tuwe na hekima kwa watoto zetu
   
 6. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #6
  May 19, 2011
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Source JF...
   
 7. L

  Leornado JF-Expert Member

  #7
  May 19, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hata kama jama angekuwa mpole, iko siku mtoto angetoa siri. Hakuna marefu yasio na ncha.

  Wanaume wengi huwa si waaminifu wakati wake zao wazazi.
   
 8. Mayasa

  Mayasa JF-Expert Member

  #8
  May 19, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 587
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Watoto wa siku hizi wanawahi sana kukua, huyo mtoto atakuwa kasema kwa makusudi kabisa...
   
 9. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #9
  May 19, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  za mwizi.....
   
 10. lono

  lono Senior Member

  #10
  May 19, 2011
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Excellent!!!!!!! ningebahatika kumuona huyu mtoto ningempatia bonge la zawadi.
   
 11. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #11
  May 19, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Uongo! Hajasema kwa makusudi, watoto hawana hulka za kishetani za kihivyo, yeye alisema alichoeksipiriensi, na ni kweli kabisa. Ndo maana hakuwahi kusema, alikisema konteksikale, pale alipohhimizwa aharakishe kifungua kinywa.
   
 12. S

  Sharo hiphop JF-Expert Member

  #12
  May 19, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 662
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Watu wengine wanaiba alafu hawajui kuiba.
   
 13. c

  chetuntu R I P

  #13
  May 19, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pole kwa mtoto.
   
 14. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #14
  May 19, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Hayo ndio mambo ya uzinifu. Hata mtoto hakuwa na huruma nae. Huyu mtu ana laana. Kama mimi nampeleka polisi kwa kuniumizia mwanangu, na nasikia ukifika keko wakisikia kosa kama hilo, ataipata.
   
 15. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #15
  May 19, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Unakula na kipofu halafu unamgusa mkono!
   
 16. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #16
  May 19, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,147
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  swali ni kwamba,ataacha kumpitia binti au ataacha kumpeleka mtoto shule?
   
 17. wapalepale

  wapalepale JF-Expert Member

  #17
  May 19, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 259
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 33

  haa mkubwa huyo bwana, miaka tisa kwa watoto wa siku hizi!!!!!!!
   
 18. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #18
  May 19, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  hasira hasara.angeuchuna kimya au ajitete kuwa ni mfanyakazi mwenzie hawezi kuacha kumpa lift
  lakn alivoreact lazima lipo jambo.Huyu bwana apelekwe fasta mahakamani hana adabu labda mtoto awe
  hajaungua usoni
  .agrr napata hasira ole wake angekutana na mm kwneye chumba cha upilato
   
Loading...