Mtoto afariki kwa kukosa matibabu, wazazi waliamini maombi pekee

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
2,954
8,093
Tukio hilo lilitokea Machi 17 baada ya mtoto huyo kuugua kwa siku tatu huku akiwa anafungiwa ndani na baba yake Cossam Sikapita, akidai kuwa hawataki aende hospitali kupatiwa matibabu kwani kwa kufanya hivyo angekuwa ametenda dhambi kwani dini hairuhusu kutibiwa na dawa za hospitali.

Mwanafunzi wa darasa la saba Shule ya Msingi Laela A, Ruti Sikapitaamefariki dunia baada ya wazazi wake kukataa kumpeleka hospitali kwamadai kuwa imani ya dhehebu lao haliruhusu waumini wake kutibiwa hospitali.

Tukio hilo lilitokea Machi 17 baada ya mtoto huyo kuugua kwa siku tatu huku akiwa anafungiwa ndani na baba yake Cossam Sikapita, akidai kuwa hawataki aende hospitali kupatiwa matibabu kwani kwa kufanya hivyo angekuwa ametenda dhambi kwani dini hairuhusu kutibiwa na dawa za hospitali.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Laela, Didas Simtengui,alisema kuwa mtoto huyo alikuwa anaumwa kwa siku tatu na hawakumpeleka hospitali badala yake walikuwa wanazidisha maombi wakiamini kuwa atapona.

Mmoja wa majirani, Musa Mwanakulya alisema kuwa wao walikuwa hawamuoni
mtoto huyo akienda shuleni na wenzake na walijua anaumwa na ametibiwa
isipo kuwa maombi ni kitu cha kawaida na walikuwa wakisikia wanaomba
kila siku katika nyumba hiyo.

‘’tulikuwa tunasikia wakisali sana huku wakiwa wamejifungia ndani, tulipo uliza walidai kuwa wanamuombea Ruti anaumwa lakini hawataki kumpeleka hospitali wakidai kuwa mafundisho ya dini yao haya ruhusu kutibiwa hospitali….waliendelea kumuombea mpaka akafariki dunia’’…alisema.

Majirani walipopata taarifa kuwa mtoto huyo amefariki kutokana na wazazi wake kugoma kumpeleka hospitali, walikwenda kuvamia katika nyumba hiyo wakitaka wawakamate wazazi hao ili nao wawaue.

Kutokana na vurugu kubwa kuibuka ililazimu polisi wa kituo cha Laela wafike katika eneo hilo na kuwatawanya watu waliokuwa na hasira kali na kuuchukua mwili wa marehemu kwenda kuuhifadhi katika chumba cha kuhifadhia maiti kilichopo katika kituo cha afya cha Laela na wazazi wa mtoto huyo kuwaweka rumande ili kuwaokoa na wananchi wenye hasira kali.


Chanzo: Mwananchi


My take: Tuwe makini sana wadau na hizi imani, zisitupeleke katika umauti.
 
Back
Top Bottom