Mtoto afariki dunia baada ya kukeketwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto afariki dunia baada ya kukeketwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MaxShimba, Oct 22, 2009.

 1. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  BABA MZAZI wa mtoto Debora Daniel [4] aliyetambulika kwa jina la Daniel Shauri [37] anashikiliwa na polisi mkoani Manyara kwa kosa la kutoa idnini binti yake akeketwe na kumsababishia kifo.
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Parmena Sumary alisema kuwa tukio hilo lilitokea siku hiyo saa 10.00 jioni katika Kijiji cha Imbilili Wilayani Babati.

  Mtoto huyo alikeketwa mnamo Oktoba 11, mwaka huu huko Manyara na baada ya zoezi hilo alivuja damu nyingi sehemu za siri hadi kufikia mauti yake Oktoba 18, mwaka huu kutokana na mkasa huo.

  Kamanda alisema kabla ya kifo chake, mtoto huyo alikuwa akiishi na mtuhumiwa baada ya mama yake mzazi, Bi. Chatherine Daniel (29) kupata kichaa na kumtelekeza akiwa mdogo.

  Alisema Kutokana na hali hiyo ya mtoto huyo kukosa malezi ya mama yake ilimpelekea akose afya na kupata na homa za mara kwa mara kwa sababu ya kukosa maziwa halisi ya mama.

  Alisema kutokana na hali hiyo ya mtoto huyo kuumwa mara kwa mara ilipelekea na kusababisha wazazi wa mtuhumiwa kushauri kuwa mtoto huyo akeketwe ili kuondokana na matatizo hayo ya maradhi.

  Kamanda alisema kuwa mtuhumiwa alitekeleza ushauri potofu wa wazazi wake ambao aliuamini moja kwa moja, lakini alishangazwa na hali ya mtoto huyo kuendelea kuwa mbaya hadi alipofariki dunia kwa kupoteza damu nyingi.

  Baada ya kifo hicho kutokea, mtuhumiwa alitaka kuuzika mwili wa mtoto huyo bila ya watu kujua lakini wasamaria wema walitoa taarifa kwa Mtendaji wa Kijiji hicho, Patizumu Jeseph ambaye alifika nyumbani kwa mtuhumiwa na kukuta maandalizi ya mazishi na kuwaamuru kusimamisha shughuli hiyo hadi hatua za kisheria zitakapofuatwa.

  Baada ya amri hiyo mwili huo ulichukuliwa hadi Hospitali ya Wilaya ya Babati kwa uchunguzi zaidi na ndipo iligundulika kuwa marehemu alipatwa na mauti hayo baada ya kukeketwa na kuvuja damu nyingi.

  Kamanda huyo alisema kuwa ngariba aliyehusika kumkeketa mtoto huyoa aliyetambulika kwa jina la Mama Mangiza, alitoroka baada ya hali ya mtoto kuzidi kuwa mbaya na polisi wanaendelea kumsaka kujibu shtaka hilo.

  Imedaiwa kuwa mtuhumiwa yuko chini ya ulinzi wa polisi na kumtafuta mtuhumiwa namba mbili ngariba ili wote kwa pamoja wakajibu shitaka hilo mahakamani.
   
 2. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Waakamtwe wote na watupwe jela.
   
 3. k

  kabwa Member

  #3
  Oct 23, 2009
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwahiyo sikuhizi daktari akimfanyia operesheni mgonjwa akifa daktari anashtakiwa?
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Hawa wanatakiwa wafinywe na kupewa displini ili liwe ni funzo

  kwa wote wenye ushenzi huo wa kizamani...They are living in

  the past and they force to the Earth to spin anticlockwise!...Shiit!
   
 5. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #5
  Oct 23, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Ni bora wa'officialize' hii practice ya ukeketaji ili ifanyike kitaalamu kwa wanawake kama wanataka kama ilivyo kutairiwa kwa wanamme. Ni utamaduni wa watu na nadhani dola & NGOs hazitashinda vita hii
   
 6. M

  Mwambashi Member

  #6
  Oct 23, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukeketaji ni kinyume na haki za binadamu. Wote wana makosa ambayo ni ukeketaji na la pili ni kusababisha mauti.
  Kwani ndugu yangu kikwenu ukeketaji unaruhusiwa?????
   
 7. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #7
  Oct 23, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Hivi upo dunia ya wapi ndugu?
   
 8. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #8
  Oct 23, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  [ame]http://www.youtube.com/watch?v=kOfmvhJ7tdg&feature=related[/ame]
   
 9. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #9
  Oct 24, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
Loading...