Mtoto adaiwa kufia mikononi mwa polisi Mwanza

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,300
5,434
kijana mtoto.jpg

Yahaya Aboubakar

Familia ya kijana Yahaya Aboubakar, aliyeuawa mikononi mwa polisi yaomba haki itendeke kwa waliohusika na mauaji hayo.

Kijana Yahaya Aboubakar mwenye umri wa miaka 15 anadaiwa kukamatwa na askari polisi nyumbani kwa bibi yake mtaa wa Juhudi, Kata ya Mabatini wilaya ya Nyamagana Septemba 2, 2022, akiwa mzima, kisha polisi hao waliondoka nae na kumfungia ndani bibi yake Yahaya ambapo baada ya kufanikiwa kutoka ndani alifanya jitihada za kumtafuta mjukuu wake katika vituo vya polisi na kumkosa.

"Wakasema wewe mama fungua nikawauliza nyie kina nani? mna kibali cha kuingia humu wakasema wao ni maaskari mbona hakuna mwenyekiti wala balozi wakasema ukigoma kufungua tunapiga mawe, baadae saa kumi na mbli marehemu akafika mjukuu wangu akawekewa mtutu huku na huku akaambiwa fungua mlango akafungua mlango wakamshika wakamuweka chini marehemu akalalamika akasema msinipige mimi sijabisha mnipeleke tu kama ni kituoni mimi nikamwambia mtoto huyo ni mgonjwa msimpige mpelekeni tu tutamfuatilia" ameeleza Bibi wa marehemu.

Mama mzazi wa Yahaya, Rehema Simba, amesema baada ya kuzunguka vituo vyote vya polisi kikiwemo kituo kikuu cha Nyamagana na kumkosa kijana wake ndipo akakutana na mkuu wa upelelezi akamwambia aende kwa RCO ili amueleze mtoto wake alipo.

"Baada ya kufika kwa RCO akasema shida nini nikamuelezea kwamba tumekuja ofisini kwako kuna kijana wangu amekamatwa tumeshazunguka vituo vyote vya polisi hatujampata akasema mtoto wako yupo Bugando Mochwari nikamuuliza mochwari amefuata nini? mbona mapolisi walimchukua nyumbani akiwa mzima? akaniambia kwamba baada ya kuchukuliwa na polisi alipelekwa eneo la mashiri na kupigwa na wananchi ndipo akafariki," ameeleza mama wa marehemu.

Ramadhan Ng’anzi ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, amesema bado uchunguzi unafanyika wa tukio hilo na atakayebainika kuhusika na mauaji hayo atachukuliwa hatua za kisheria.

Chanzo: EATV
 
Ramadhan Ng’anzi
RPC, this is rubbish, hamwezi kujichunguza mkamwajibisha your fellow police! Rais Samia tunasaema kiwepo chombo huru headed by a Respectable Judge (ingawa kwa Tanzania ni kazi ngumu kumpata) ku handle cases kama hizo maana polisi watampendelea mwenzao; Nature ya binadamu iko hivyo...
 
Ebo! inafikirisha kweli!!? Polisi wamtoe mtoto katika mikono salama wampeleke kwa wananchi, wenye uchungu mkali kwa tozo kila ukicha, wenye misongo ya mawazo akauawe huko Mashiri? Hakika damu yake haitowaacha salama kwa vyovyote vile wahusika

ZERO, STOP!
 
View attachment 2355206
Yahaya Aboubakar

Familia ya kijana Yahaya Aboubakar, aliyeuawa mikononi mwa polisi yaomba haki itendeke kwa waliohusika na mauaji hayo.

Kijana Yahaya Aboubakar mwenye umri wa miaka 15 anadaiwa kukamatwa na askari polisi nyumbani kwa bibi yake mtaa wa Juhudi, Kata ya Mabatini wilaya ya Nyamagana Septemba 2, 2022, akiwa mzima, kisha polisi hao waliondoka nae na kumfungia ndani bibi yake Yahaya ambapo baada ya kufanikiwa kutoka ndani alifanya jitihada za kumtafuta mjukuu wake katika vituo vya polisi na kumkosa.

"Wakasema wewe mama fungua nikawauliza nyie kina nani? mna kibali cha kuingia humu wakasema wao ni maaskari mbona hakuna mwenyekiti wala balozi wakasema ukigoma kufungua tunapiga mawe, baadae saa kumi na mbli marehemu akafika mjukuu wangu akawekewa mtutu huku na huku akaambiwa fungua mlango akafungua mlango wakamshika wakamuweka chini marehemu akalalamika akasema msinipige mimi sijabisha mnipeleke tu kama ni kituoni mimi nikamwambia mtoto huyo ni mgonjwa msimpige mpelekeni tu tutamfuatilia" ameeleza Bibi wa marehemu.

Mama mzazi wa Yahaya, Rehema Simba, amesema baada ya kuzunguka vituo vyote vya polisi kikiwemo kituo kikuu cha Nyamagana na kumkosa kijana wake ndipo akakutana na mkuu wa upelelezi akamwambia aende kwa RCO ili amueleze mtoto wake alipo.

"Baada ya kufika kwa RCO akasema shida nini nikamuelezea kwamba tumekuja ofisini kwako kuna kijana wangu amekamatwa tumeshazunguka vituo vyote vya polisi hatujampata akasema mtoto wako yupo Bugando Mochwari nikamuuliza mochwari amefuata nini? mbona mapolisi walimchukua nyumbani akiwa mzima? akaniambia kwamba baada ya kuchukuliwa na polisi alipelekwa eneo la mashiri na kupigwa na wananchi ndipo akafariki," ameeleza mama wa marehemu.

Ramadhan Ng’anzi ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, amesema bado uchunguzi unafanyika wa tukio hilo na atakayebainika kuhusika na mauaji hayo atachukuliwa hatua za kisheria.

Chanzo: EATV
Baada ya kuchukuliwa na polisi alipelekwa mashiri ndipo wananchi wakampiga.Hapo panahoja.
 
Nonsense..hivi hawa polisi wanajikuta ni akina nani?.yani wanampeleka mtuhumiwa kwa wananchi wanamuacha apate kipigo mpk kuf...?sasa kazi yao ni nini?.maana hapo hawajamlinda raia wameacha afe.
 
Lisikubalike Hili!.Watanzania Tupige Kelele! Yaani Polisi Wamchukue Kijana Nyumban Kwaoi Akiwa ni Mzima Halafu Wampeleke Mitaani Akapigwe na Wananchi Hadi Kuuawa!
Hili Linaleta Ukakasi. Lichunguzwe Vyema....
 
Kweli, pande zote mbili zisikilizwe! Ingawa kuua ni kosa ila dogo labda aliwasumbua sana. Ukizingatia kalelewa na bibi!
Wapo watu wengi tu wanakaa na bibi zao,mama zao ila wanakuwaga na historia chafu yaani bad#
Kuna ile kitu unachokwa na jamii kwq sababu ya matukio yako
Hata mkienda polisi wenyewe wanakuambieni nyie mkikamata malizana nao,sisi tutakuja kubeba mwili tu
Swali je huyo dogo alikuwa na rekodi chafu?

Ova
 
Back
Top Bottom