Mtoto aandika barua kuomba hela kwa Mungu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto aandika barua kuomba hela kwa Mungu

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by SWADO, Jan 11, 2011.

 1. S

  SWADO Member

  #1
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JOKE.

  Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 9 alikuwa anahitaji sana shilingi 100,000 (laki moja). Akamuuliza mama yake ni jinsi gani anaweza kupata pesa hizo. Mama yake akamwambia "muombe Mungu atakupatia. Mtoto alianza kuomba kila siku na kila mara lakini hakupata hiyo pesa toka kwa Mungu. Hatimaye akafikia uamuzi wa kumuandikia barua Mungu ili asome maombi yake. Kisha akai-post barua ile. Wakati wafanyakazi wa posta wakichambua barua kwa ajili ya kuzipeleka sehemu husika, walishangazwa kuona bahasha iliyoandikwa "Kwa Mwenyezi Mungu" na wakashindwa kuelewa mahali
  pa kuipeleka, Wakaamua kuifungua.

  Barua ilisomeka hivi:

  "Mpendwa Mungu,

  Jina langu ni EMMANUELEY, nina umri wa miaka 9 na ninasoma darasa la
  tatu katika jiji la Dar es salaam ambalo liko katika nchi ya Tanzania ,
  bara la Africa .

  Nimeamua kukuandikia barua hii kukuomba kiasi cha shilingi laki moja
  baada ya kuomba bila kupata majibu toka kwako.
  Naomba sana unisaidie kwani mimi ni mtoto mdogo na sina uwezo wa kufanya kazi na kupata pesa. Pia wazazi wangu hawana uwezo kwani hata nchi yetu
  ni maskini sana .

  Natanguliza shukrani.

  Wako mtiifu,


  EMMA."


  Wafanyakazi wa posta walifurahishwa sana na barua hiyo na kisha wakaamua
  waipeleke kwa Rais KIKWETE. Rais KIKWETE naye alipoipokea ilimfurahisha
  sana na kisha akamwambia Secretary wake achukue sh. 2000 amtumie mtoto
  huyo akidhani kuwa pesa hizo ataziona kuwa nyingi sana .

  Mtoto huyo alipopokea hizo shilingi 2000 alijibu hivi:

  "Mpendwa Mungu wangu,

  Nashukuru sana kwa kusikiliza maombi yangu na kunitumia pesa nilizokuomba. Lakini nimebaini kuwa uliamua kuzituma kupitia serikali yetu ya Tanzania . Kama ilivyo kawaida yao hao wezi, wamekata kiasi cha sh. 98,000 kwa ajili ya kodi , kwa hiyo wameniletea Sh. 2000 tu
   
 2. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #2
  Jan 12, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha!
  Wangempa hata elf 50 jaman.
   
 3. fundiaminy

  fundiaminy JF-Expert Member

  #3
  Jan 12, 2011
  Joined: Jun 4, 2009
  Messages: 358
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Duh! Hahahaha..hii imeanzisha cku yangu poa.
   
 4. S

  Simeon Member

  #4
  Jan 12, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 61
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  duuu...!mtoto mdogo keshakosa imani na serikali...!
   
 5. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #5
  Jan 12, 2011
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280
  Hii kweli kali!
   
Loading...