Mtori una asili ya wapi?

Mtori ni asili ya wachaga,kule wanakunywa asubuhi na chapati ndio Siri ya wachaga kuwa na akili mingi,na mtori tumeu expose nchi nzima Chagas sio watu wa mchezo mchezo
Mtori asili yake ni chakula cha kabila la wachaga. Hiki chakula ni maalum (kilikuwa maalum kuwa sahihi zaidi) kwa kinamama waliojifungua. Miezi mitatu ya mwanzo baada ya kujifungua ndicho kilikuwa chakula chao kikuu (pamoja na kingine cha aina ya mtori, lakini badala ya nyama na supu kinachanganywa na maziwa ya ng'ombe ya mgando). Siku hizi mtori umeenea sehemu nyingi na umekuwa unauzwa kama kifungua kinywa.
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom