• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Mto Kawe NEC nani anahusika na uchimbaji mchanga. TRA mnajua hili?Mkuu wa Wilaya saidia

BASIASI

BASIASI

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2010
Messages
8,872
Points
2,000
BASIASI

BASIASI

JF-Expert Member
Joined Sep 20, 2010
8,872 2,000
Wapendwa ktk bwana
Bwana Yesu Asifiwe
Assalahm Allheikhum

Wa NEC kuna malori yanaendelea kubeba mchanga mto Kawe ingawa mh Makonda alishawahi kupiga marufuku

Hali ya mto kawe si salama hata kidogo tena kwa uchimbaji tunaomba NEC wafike waone hali halisi

Hizi lori zinazolipa wahuni kadhaa waliojimilikisha mto Kawe na hata kuanzisha SACCOS yao kutokana na pesa za mtoni

Mto huu kuna watu wa manispaa wamekuwa wakija na mashine na kulipiza kila lori

Nabaki najiuliza sana hivi TRA wako wapi iweje sehemu zingine wapo huku mtoni kama wamewapa kibali nani anahusika na kwanini TRA awakusanyi kodi

Mh Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni msaada wako tafadhali maana hata polisi wa Kawe wakiongozwa na mkuu wao wanajua huu uchafu

Mbaya zaidi gari za polisi zimekuwa zikishuka chini na kugeuka bila mafanikio ya kusitisha nawaza zinakuja kufanya nini?

Naamini Serikali mtalisimamia hili..
 

Forum statistics

Threads 1,405,596
Members 532,052
Posts 34,490,107
Top