Mtizamo wa Bloga: Uamuzi wa CHADEMA Kususia Hotuba ya Kikwete Bungeni

Kitendo cha CHADEMA kutoka ni tukio la kawaida katika medani za siasa, Nawashangaa sana hawa mafisadi ambao wanaona ni kitendo cha ajabu. kwani kusikiliza hotuba mpaka uwepo mjengoni? Waacheni CHADEMA huenda walikuwa na mambo yao ya muhimu. Isitoshe hata baadhi ya wabunge wa CCM wanaopinga ufisadi jana hawakutia mguu mjengoni sasa hao nao mnasemaje?

Tatizo ni kuwa kinawauma kishenzi! Hicho kitendo kimetia doa historia ya Kikwete na chama chake. Legacy yake aliyotaka kuiacha wont be read the way he wanted it to be read. Kwake ni total humiliation apende asipende.
 
Kwanza mimi naung Mkono walichofanya CHADEMA 100%.

Unapopinga jambo inabidi kufanya kwa vitendo, na walichofanya wanaharakati wa CHADEMA wamewaonyesha wachakachuaji kuwa hawakubaliani na fikra na mawazo yao hata kidogo.

Na huo ni mwanzo tu, tunawapa taarifa wajipange vizuri mbeleni mambo ni magumu zaidi. Enzi za kuburuzana zimekwisha!"You can fool some people some of the time, bu you can't fool all the people all of the time"
 
Hoja za kitoto kwa sababu nahoji sincerity na consistency ya CHADEMA ?

Kukurumuka mambo ya Kalemie au wapi hayo?

Kwa uelewa wako mdogo, unafikiri ninapoongelea habari ya CHADEMA kushiriki uhakiki wa Waziri Mkuu, naongelea habari ya Pinda. No wonder unameza vitu vizima vizima bila kumung'unya.

Kwa kushiriki uhakiki wa Pinda, chaguo la Kikwete, wabunge wa CHADEMA wamemtambua Kikwete kama rais tayari, sasa sijui hizi habari za kutomtambua Kikwete zinaanzia wapi wakati walishamtambua mpaka kupigia kura chaguo lake la Waziri Mkuu.

CHADEMA hawana consistency wala maturity ya kuchukuliwa seriously, nililisema kabla na sasa wanadhihirisha hili.

Hebu nikuulize wewe unadhani haya yote yanayo tendeka na kufanywa na serikali ya CCM na JK kuwa kuna wana CCM wanapenda hayo? kwa Taarifa yako nadhani wewe huijui democrasia safi wewe ni fuata mkumbo wa watu tuuu, wana CCM wengi hawapendezwi na serikali yao inavyoindesha hii nchi ni kuwa tu watu hawajaijua KATIBA na ole wenu watanzania wenge waje kuijua hii KATIBA na HAKI zao ndio mtawajua vyema tutizame alama za nyakati jamani.

Kwa kukumbusha Kidogo what happened in KENYA,ZIMBABWE hapo karibu tuu na sio mbali kwingine ni Ndani ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hapo Zanzibar CUF walikuwa hawamtambui Karume laki ndio huyo huyo waliingianae mikutano ya siri na kutoka na jibu la serikali ya muungano zanzibar sasa sikuelewi wewe unaendana na wakati au? How OLD are You by the way?

Waziri mkuu ameteuliwa na JK. Kwanini basi wasingejitoa? Kukaa ndani na kushiriki katika upigaji kura hata kama kura yenyewe ni ya hapana tayari walishakubali process.

Kuteuliwa na kuchaguliwa ni vitu viwili tofauti, waziri Mkuu kateuliwa hili azibitishwe kikatiba lakini kwa kuwa katiba yetu ni mbovu kupinga uteuzi ni vigumu sana, kwani vipengele vingi vinakiukwa chini ya mfumo wa vyama vingi, kukubali uteuzi uo kwa mfumo huu ni sehemu ya kuburuzwa hivyo ndio maana wengine walipiga kura za kumkataa, katiba ikibadilishwa ni lazima wazili mkuu awe amependekezwa alfu achaguliwe miongoni mwa wabunge
 
Suala ambalo limetawala maongezi ya Watanzania wengi kwenye social media kwa leo ni kitendo cha wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kususia hotuba ya Rais Jakaya Kikwete wakati anazindua Bunge jipya mjini Dodoma.Kwanza niweke wazi msimamo wangu kuwa naunga mkono uamuzi huo wa Chadema.Sifanyi hivyo kwa minajiki ya kukipenda chama hicho bali ni katika kuzingatia ukweli kuwa Chadema wametumia HAKI yao ya Kikatiba na kidemokrasia kuonyesha upinzani wak kwa vitendo.Nimeandika HAKI kwa herufi kubwa kwa vile neno hilo ni muhimu katika "kuwahukumu" Chadema.

Baadhi ya wenzetu wamekishutumu vikali kitendo hicho huku wengine wakikiita "utovu wa nidhamu wa hali ya juu".Lakini wakati wenzetu hao wanatumia HAKI zao za Kikatiba na kidemokrasia kuwalaumu Chadema,hawataki kutafakari japo kidogo kuhusu HAKI kama hizo kwa chama hicho,yaani HAKI yao ku-protest kwa amani dhidi ya mwenendo mzima wa uchaguzi uliopelekea Jakaya Kikwete kuwa Rais tena.

Inawezekana tukio hilo linaonekana sio la kawaida kwa vile ni mara ya kwanza kutokea nchini.Lakini kwa wanaojishughulisha kufahamu kinachoendelea sehemu nyingine duniani watafahaku kuwa hali hiyo imeshatokea kwenye mabunge mbalimbali,kwa mfano nchini Afrika Kusini,Gambia,Sudan, India,Pakistan na Iraki,to mention only a few.

Kwa namna moja au nyingine,vipengere dhalimu vya Katiba yetu vimewaacha Chadema na alternatives chache zaidi ya hatua kama hiyo ya leo kwa vile Katiba yetu inanyima uhuru wa kupinga matokeo ya ushindi wa Rais mahakamani hata kama ushindi huo umepatikana kwa njia zisizo halali.Leo mapungufu hayo makubwa kwenye Katiba yetu yanaweza kuonekana kama jambo dogo.Lakini yayumkinika kuamini kuwa inaweza tokea tukapata Rais dikteta ambaye ameshindwa kwa mabavu lakini tukajikuta hatuna njia ya kupinga "ushindi" wake kwa vile Katiba inamlinda.

Tatizo la Katiba nyingi katika "Nchi za Dunia ya Tatu" na hususan barani Afrika ni ile tabia hatari ya katiba hizo kutumika kwa mahitaji na maslahi ya watawala walio madarakani.Na kwa vile wengi wa watawala hao ni walafi na waroho wa madaraka,na kwa vile madaraka makubwa waliyonayo yanawapa uhuru wa kufanya lolote wapendalo,katiba hizo huwekwa viraka hapa na pale sio kwa minajili ya ustawi wa taifa husika bali kikundi kidogo cha watawala.

Laiti Katiba ingekuwa inaruhusu ushindi wa Rais kupingwa mahakamani basi ni dhahiri Chadema wangeshafungua kesi.Kuna wanaosema "sasa wakitoka nje ya Bunge ndio inasaidia nini?"Majibu ni mengi ila hapa nitatoa machache tu.Kwanza,ikumbukwe kuwa Chadema ndio chama kikuu cha upinzani bungeni.Pamoja na uchache wa idadi ya wabunge wao ukilinganisha na wale wa CCM,hadhi ya chama kikuu cha upinzani ni kubwa na muhimu ndani na nje ya nchi.Pamoja na mazingira na sheria kandamizi dhidi ya vyama vya upinzani,kwa nchi masikini kama Tanzania kuna kila sababu ya sote kuonekana tumeshikamana hata kama mshikamano huo ni wa kinafiki na unawanufaisha zaidi mafisadi.Ndio maana basi nchi wafadhili zilikuwa zikiwakalia kooni watawala wetu kuhusu upatikanaji wa suluhisho la kudumu huko Zanzibar,ambapo hatimaye CCM kwa shingo upande (na licha ya ngebe za akina Makamba) leo hii tunashuhudia serikali ya umoja wa kitaifa huko Zanzibar.

Of course,hali ya kutoelewana huko Zanzibar ilikuwa serious sana hasa kutokana na vurugu za uchaguzi zilizopelekea mauaji ya watu kadhaa,ukweli unabaki kuwa msimamo thabiti wa chama kikuu cha upinzani visiwani humo,yaani CUF,kutotambua matokeo ya chaguzi mbalimbali,sambamba na kelele walizopiga kwa jumuiya ya kimataifa ndivyo vilivyopeleka leo hii kuwepo serikali ya umoja wa kitaifa.

Kwahiyo wanaohoji umuhimu wa wabunge wa Chadema kususia hotuba ya Kikwete wanapaswa kuelewa kuea msimamo imara sambamba na matendo yanayothibitisha msimamo huo yanasaidia kuleta mabadiliko yanayokusudiwa.Leo pale Dodoma kulikuwa na wawakilishi wa nchi na jumuiya mbalinbali za kimataifa.Vyovyote itavyokuwa,wameguswa na tukio hilo ambalo kwa hakika limetia dola utawala wa Kikwete.Baadhi ya nchi hizo ni wafadhili ambao bila wao basi mambo yanakuwa si mambo.

Lakini jingine la muhimu ni kufikisha ujumbe kwa Kikwete na serikali yake (including vyombo vya dola na Tume ya Uchaguzi) kuwa zama za "ndiyo mzee" zimefika kikomo.Hata kama Katiba inaendelea kuhalalisha sheria dhalimu (kama hiyo inayonyima fursa ya kupinga ushindi wa rais mahakamani) mwanya mdogo wa uhuru wa kidemokrasia kupingana pasipo kupigana unawezesha Chadema kuzalisha harakati mpya za mapambano dhidi ya udhalimu lakini pasipo vurugu au umwagaji damu.Kwa tunaotaka kuona Tanzania yenye kuheshimu na kuzingatia haki na stahili za Watanzania,kitendo cha leo cha Chadema kinafungua ukurasa mpya wa matumaini.Kadhalika,kitendo hicho ni hatua kubwa na muhimu ya kukua kwa demokrasia yetu kutoka vyama vinavyokubali yaishe hata pale penye uthibitisho kuwa vimejumiwa kwenye chaguzi,kwenda kwenye zama ambapo uchakachuaji wa chaguzi unaharamishwa hadharani tena kwenye live tv.Message delivered!

Ni wazi kuwa tukio la leo limemgusa Kikwete na serikali yake kama ambavyo limewagusa Watanzania wengi na jumuiya ya kimataifa.Yayumkinika kuwa inawezekana nguvu kubwa iliyotumika kuchakachua matokeo ya uchaguzi uliopita sasa itaelekezwa katika kuihujumu Chadema ili idhoofike na hatimaye kuachana na msimamo wake wa kukataa kumtambua Kikwete.Zitafanyika jitihada za kuwqgombanisha viongozi wa chama hicho kama ilivyokuww kww NCCR-Mageuzi ya Mrema.Kuna uwezekano pia wa Dokta Wilbroad Slaa kuzushiwa zengwe zaidi ya lile ya maisha yake binafsi.Lakini hayo yanaweza kupita pasipo madhara makubwa kwani hata Baba wa Taifa na wenzake walipokuwa wanahangaikia ukombozi wa Tanzania kutoka himaya ya mkoloni walikumbana na vizingiti hivyo.Haya ni mapambano kati ya wenye uchungu na nchi yao dhidi ya wale wanaotaka kuigeuza nchi yetu kuwa "shamba la bibi" na makao makuu ya ufisadi.

Sie Wakristo tunaamini kuwa mwenye haki ataanguka saba mara sabini ( hapa simaanishi kuanguka kama kule kwa Kikwete pale Jangwani) lakini mwishowe atasimama.Kukubali uchakachuaji wa kura kutapelekea matokeo ya ain moja tu: uchakachuaji zaidi.Historia inatufundisha bayana kuwa kukubali kitu kibaya hakusaidii hata chembe kitu hicho kibaya kugeuka kizuri au athari zake kupungua.Wanaoshauri Dkt Slaa na Chadema "wakubali matokeo" hawana tofauti na wanaoweza kusema tuache mapambano dhidi ya malaria au ukimwi kwa vile magonjwa hayo yamekuwepo miaka nenda miaka rudi.

Laiti Nyerere na mashujaa wengine wa mapambano dhidi ya mkoloni wangepatwa na mawazo hayo ya "kukubali yaishe" leo hii tungeendelea kuwa chini ya mkoloni ( I know kuna watakaosema bora mkoloni kuliko fisadi.Mie nasema ukoloni na ufisadi ni mbaya kama ilivyo kwa kansa na ukimwi.Hakuna cha nafuu,wote ni maadui wanaostahili kuangamizwa).Na laiti Nyerere "angekubali yaishe pale Nduli Idi Amini alipotuvamia,basi huends leo tungekuwa sehemu ya Uganda chini ya dikteta Idi Amini au mrithi wake.

Giving up is not an alternative.Mapambano ya kudai haki (kwa amani) lazima yaendelee.Waingereza wana msemo kwamba kukubali kitu pungufu kwa minajili ya bora liende hatimaye hupelekea kupata kilicho pungufu zaidi ya kilichostahili kupatikana.Kadhalika,hatua zote za mabadiliko huanza kwa hatua chache na pengine ndogo lakini zenye impact na hatimaye kutengenrza mazingita mazuri kwa hatua kubwa zenye impact kubwa zaidi na pengine zenye kuweza kuandika historia mpya.Vilevile,actions speak louder than words.Na hiyo imethibitka leo kwani japo Chadema walishatangaza kuwa hawatomtambua Kikwete uzito wa tamko hilo haukuwagusa wengi kulinganisha na tukio la leo la kususia hotuba ya Kikwete.

And by the way,hotuba hiyo ilikuwa na tofauti gani na hotuba lukuki alizotoa wakati wa utawala wake 2005-2010?Hivyo vipaumbele sijui 13 (or were they 19) tulishavisikia kwenye kampeni za 2005 na zikarudufiwa kwenye kampeni za mwaka huu.Kama kuna yeyote aliyechukulia vimpaumbele hivyo seriously all I can say asubiri muda si mtefu atabaini "imekula kwake" as they say in the streets.

KULIKONI UGHAIBUNI: Uamuzi wa Chadema Kususia Hotuba ya Kikwete Bungeni Dodoma
Ndg zangu CHADEMA wanafaa kuungwa mkono mia kwa mia. Natoa ushauri kwa hao ndg zetu walioko ughaibuni huyu jamaa anayependa sana kujirusha akifika huko andamana apigwe na mayai viza kuonyesha kuwa ametwaa nchi yetu kimabavu. Hatua za kukataliwa ziendelee kila maali, ili hata hao wapambe wake wajue kuwa Watanzania wamechukia, aonyeshwe vitendo sio maneno tuu! BIG UP CHADEMA.

Oppotunities do not come with their values stamped upon them. Maltbie Babcock.

Katiba haitobadilishwa na Tume huru ya uchaguzi haitaundwa, sasa amueni kabisa 2015 mtaingia ulingoni ? Rais hafanyi kazi kwa shinikizo la CHADEMA, na hayo wanayo yataka warudi wayaombe kwake kwa njia ya mazungumzo tu na si vinginevyo
 
Ndugu yangu tambua kwamba nchi yetu inaongozwa kwa utawala wa sheria na utawala bora.usishawishi watu wafanye vurugu, na kuvunja amani zipo taratibu nyingi za kufuatwa kama haki yako haujapewa kuwmakini sana
 
the issue is no one is serious enogh to lead us out of poverty.

kama 1995(ben mk), uchaguzi ulichakachuliwa,2000(ben mk) mambo yaleyale, 2005(jk) kama kawa, 2010(jk) ulitegemea nini?

si upinzani ungefanya kama morgan tsivangiray wa zimbabwe? gomea uchaguzi na tume tangu mwanzo.

2sipoachana na siasa jaza ma2mbo hakuna kitakachoeleweka. ni walewale 2! kuna sehemu kibao wameuza kura (tetesi) mawakala na wagombea. NINI IYO????eti w2 hawakujitokeza kupiga kura!!!

wanajali ma2mbo yao 2, au si wafanye kama zanzibar. wasishiriki shughuli zozote za bunge na serikali. wako tayari kuachia mil13?????
 
Hata mseme vipi mkwere msg sent na sijui kama jana hajaanguka home kwake. Atashika adabu tu hata kama siyo leo
 
kwa hakika serikali ya ccm na kikwete imetikisika kwa kiwangi cha hali ya juu kwa kuwa kitend hicho kilifanyika mabele ya mabalozi wa nchi wahisani ambao wananchangi sehemu kubwa ya bajeti ya serikali ya ccm na jk. Japo jana kikwete alitamba kuwa serikali yake imetunga sheria mpya ya kupambana na rushwa, wengi tutakukmbuka kuwa ilibidi nchi wahisani wazuie kiasi cha bilioni 270 walizoahidi kutoa katika bajeti ya 2009/10 ndipo sheria hiyo ifikishwe bungeni. Hicho ni kiashiria kuwa serikali ya ccm na jk inakuwa remotelly controlled.

jana hiyo mabalozi watakuwa wametuma kwa serikaliz ao hali halisi ya kisias hapa nchini, ambapo kalia mara kikwete atakapopelek bakuli ataulizwa je umeshaelewana na wapinzani wako? Kama alivyokuwa akiulizwa kuhsu cuf hadi 2009; (tazama atachment mpaka august 2009 ccm na jk walikuwa bado wanatumia jeshi kuwakansdamiza wapemba) ndipo ccm na jk wakakubali kuingia muafaka na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na cuf. It was donors pressure and nota their consent.

same to us bila kuonyesha misuri kiudogo kwa njia za amani kama hizi ccm hawataweza kuelewa lugha yetu.
 
Dawa ya mwizi ni kumuambia umeiba na kumtendea kitendo kitakachofanya ajue umeiba. Sio anakuibia alafu unamkenulia, unaziba macho na masikio kisha unampa ili ajue ameiba,...... SAFI CHADEMA, JANA KAUMBUKA MBELE MI BWANA INAYOMPA ULAJI NA TRIP ZA ULAYA
 
Hoja za kitoto kwa sababu nahoji sincerity na consistency ya CHADEMA ?

Kukurumuka mambo ya Kalemie au wapi hayo?

Kwa uelewa wako mdogo, unafikiri ninapoongelea habari ya CHADEMA kushiriki uhakiki wa Waziri Mkuu, pnaongelea habari ya Pinda. No wonder unameza vitu vizima vizima bila kumung'unya.

Kwa kushiriki uhakiki wa Pinda, chaguo la Kikwete, wabunge wa CHADEMA wamemtambua Kikwete kama rais tayari, sasa sijui hizi habari za kutomtambua Kikwete zinaanzia wapi wakati walishamtambua mpaka kupigia kura chaguo lake la Waziri Mkuu.

CHADEMA hawana consistency wala maturity ya kuchukuliwa seriously, nililisema kabla na sasa wanadhihirisha hili.
upeo wako wa kuelewa mambo ni mdogo sana chadema ni smart na pragmatic akili yako inayokwambia kupiga kura uchaguzi wa wm basi wamemkubali kikwete ni upumbavu
 
I suspect Kiranga doesn't have any good intention for CHADEMA. He is simply playing with words to mud-smear CHADEMA.
 
Ndugu Kiranga Heshima sana
leo mara kadhaa nimeoshangazwa jinsi ambavyo umetoa hoja za kitoto juu ya kitendo walichofanya CHADEMA.
Nadhani kukaa kimya ni busara kuliko kukurumuka. Ikiwa chadema ingeshugulika na Pinda isngefikisha ujumbe iliokusudia katika jumuiya ya kimataifa kwa nguvu na uzito wa pekee kama ilivyotokea jana.
Kumbuka aliyetangazwa mshindi na nec si Pinda ila Kikwete na kwa hiyo hapo palikuwa mahali sahihi kabisa kufanya kitendo walichofanya. Ulimwengu umeelewa na nakuhakikishia kuw jambo hili litamsumbua rais wa JMT popote atakapokwenda nadni na nje ya nchi. Wale watoa fedha watamsumbua na maswali ya kero ambayo asingependa kuukulizwa na hatimaye njia itapatikana.

Kwetu neno 'Kiranga' lina maana 'Shetani' so connect the dots yourself..
 
Hoja za kitoto kwa sababu nahoji sincerity na consistency ya CHADEMA ?

Kukurumuka mambo ya Kalemie au wapi hayo?

Kwa uelewa wako mdogo, unafikiri ninapoongelea habari ya CHADEMA kushiriki uhakiki wa Waziri Mkuu, naongelea habari ya Pinda. No wonder unameza vitu vizima vizima bila kumung'unya.

Kwa kushiriki uhakiki wa Pinda, chaguo la Kikwete, wabunge wa CHADEMA wamemtambua Kikwete kama rais tayari, sasa sijui hizi habari za kutomtambua Kikwete zinaanzia wapi wakati walishamtambua mpaka kupigia kura chaguo lake la Waziri Mkuu.

CHADEMA hawana consistency wala maturity ya kuchukuliwa seriously, nililisema kabla na sasa wanadhihirisha hili.

Watanzania wangapi wameshiriki kumchagua Kikwete na wangapi wamemkubali? Ina maana ukishiriki kupiga kura kumthibitisha mtu tayari umethibitisha hata kama ulimpa kura ya hapana? Kama ingekuwa hivyo, kwa nini hakupata kura kwa 100% na kwa nini Pinda mwenyewe alisema alishangaa wabunge wa Chadema kutomuunga mkono?
 
Hoja za kitoto kwa sababu nahoji sincerity na consistency ya CHADEMA ?

Kukurumuka mambo ya Kalemie au wapi hayo?

Kwa uelewa wako mdogo, unafikiri ninapoongelea habari ya CHADEMA kushiriki uhakiki wa Waziri Mkuu, naongelea habari ya Pinda. No wonder unameza vitu vizima vizima bila kumung'unya.

Kwa kushiriki uhakiki wa Pinda, chaguo la Kikwete, wabunge wa CHADEMA wamemtambua Kikwete kama rais tayari, sasa sijui hizi habari za kutomtambua Kikwete zinaanzia wapi wakati walishamtambua mpaka kupigia kura chaguo lake la Waziri Mkuu.

CHADEMA hawana consistency wala maturity ya kuchukuliwa seriously, nililisema kabla na sasa wanadhihirisha hili.

Pole sana fisadi kiranga.

Najua kinachokuliza ni kuwa unaona dalili za wazi za kitumbua chako kuingiwa mchanga. kilio hiki si kwako pekee ni kwa vibaraka wote wa ccm. mnajaribu kuibua mjadala na hoja dhaifu sana lakini mnajua kabisa kuwa meseji ya CHADEMA imefika mahali pake, walichofanya wabunge wa CHADEMA wamewakilisha mawazo ya sisi wapiga kura wao na sio nyie wapigakura wa ccm. Nyie angalieni kama ccm inawatekelezea ilichowaahidi au la! Lakini sio kuhoji wanachofanya CHADEMA maana wanafanya tunachotaka sie wafuasi wao.
 
Nasikia Mkwere anasema waliotoka Bungeni leo watalazimika kumpigia magoti ili awape hela za kuendeleza majimbo yao!!!!
Siamini hilo kama ni kweli - silaha dhaifu!!! Hivi huyu Mchakachuaji hawajui hawa CDM; kwaniCHADEMA ilipokuwa inakua hadi kutoka wabunge 4 hadi 23 aliwapa hela ngapi. Wait and see the creative minds of CHADEMA!!!!!
Naunga mkono hatua ya kutoka mjengoni na nawapongeza wote waliotoka, na hata wale ambao hawakuwepo.

Hiyo hela anayosema hawapi inatoka mfukuno mwake?
 
the issue is no one is serious enogh to lead us out of poverty.

kama 1995(ben mk), uchaguzi ulichakachuliwa,2000(ben mk) mambo yaleyale, 2005(jk) kama kawa, 2010(jk) ulitegemea nini?

si upinzani ungefanya kama morgan tsivangiray wa zimbabwe? gomea uchaguzi na tume tangu mwanzo.

2sipoachana na siasa jaza ma2mbo hakuna kitakachoeleweka. ni walewale 2! kuna sehemu kibao wameuza kura (tetesi) mawakala na wagombea. NINI IYO????eti w2 hawakujitokeza kupiga kura!!!

wanajali ma2mbo yao 2, au si wafanye kama zanzibar. wasishiriki shughuli zozote za bunge na serikali. wako tayari kuachia mil13?????

Naona wewe hujui tofauti kati ya bunge na serikali kama CUF ilivyokuwa haielewi ndo maana huoni moyo wa kizalendo wa wabunge wa CHADEMA wa kushiriki shughuli za bunge lakini kumsusia kikwete.
 
Ndugu yangu tambua kwamba nchi yetu inaongozwa kwa utawala wa sheria na utawala bora.usishawishi watu wafanye vurugu, na kuvunja amani zipo taratibu nyingi za kufuatwa kama haki yako haujapewa kuwmakini sana

We Nyuki umeteleza kidogo; nchi yetu inaongozwa na sheria mbovu na utawala mbovu hivyo tubadilike. Naunga mkono CHADEMA mia kwa mia.
 
Katiba haitobadilishwa na Tume huru ya uchaguzi haitaundwa, sasa amueni kabisa 2015 mtaingia ulingoni ? Rais hafanyi kazi kwa shinikizo la CHADEMA, na hayo wanayo yataka warudi wayaombe kwake kwa njia ya mazungumzo tu na si vinginevyo

Tutaingia msituni
 
Back
Top Bottom