Mtizamo wa Bloga: Joka Lenya Vichwa Vitatu Linaweza Kusalimika Likikatwa Vichwa Viwili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtizamo wa Bloga: Joka Lenya Vichwa Vitatu Linaweza Kusalimika Likikatwa Vichwa Viwili?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kulikoni Ughaibuni, Apr 10, 2011.

 1. Kulikoni Ughaibuni

  Kulikoni Ughaibuni JF-Expert Member

  #1
  Apr 10, 2011
  Joined: Dec 12, 2007
  Messages: 234
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 60
  [​IMG]

  [​IMG]

  CHANZO: CCM: Joka Lenya Vichwa Vitatu Linaweza Kusalimika Likikatwa Vichwa Viwili? ~ Kulikoni Ughaibuni
   
 2. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Ndio joka hilo sasa ndio haswa linapaswa kuitwa JOKA manake katika dhana nzima ya REALITY alijapata tokea kusikia JOKA LA VICHWA VITATU [JAPO NI KUSADIKIKA] kama Urais wa JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ulivyokua ukisadikika kua ni ubia wa watatu hao.

  Na amini sasa JOKA HALISI amepatikana kama ambavyo watanzania waliitaji kumuona Rais wao akisimamia maamuzi magumu.Kama JK ataisimia yote yale ambayo wananchi wamekua wakiayapigia kelele kwa muda wote basi,jipu limepata mtumbuzi japo katika muda uliokwenda.

  Katika hili hii ni heri kwa watanzania manake mustakabali wa nchi utapata mwelekeo kwani kwa mpasuko huo ni muda mwema ambao Rais atapata Timu mpya tofauti na ile ambayo macho ya watanzania wengi waliamini na kusadiki kua ilikua inaudwa na kundi la mafisadi.

  Watakao mkaribia na kumsogelea Rais watakua ni wale ambao hawana kashifa kwenye jamii na ni watu wanaokubalika na jamii.Ni muda ambao CCM wanafahamu kitendo cha KUMWEKA MADALAKANI KWENYE NGAZI YOYOTE KICHAMA NA SERIKALI MTU AMA KIONGOZI MWENYE KASHIFA AMA JAZIBA ITAKUA IMEWAANGUSHA KWENYE SURA YA JAMII [YAANI IMEKULA KWA WANA CCM].

  JK
  atakua amekula BINGO KWA WATANZANIA KWA MWANZO MZURI, Ila kama ndio mwanzo basi uzi uwe ule ule, kama ulitishiwa kumwagiwa mboga wakati yeye ndie mnunuzi wa mboga hiyo basi hana budi kuwanyima chakula hao waliomtishia kumvua madaraka hayo, wakijua kwa mfumo ambao chama cha mapinduzi kimekua kikiutumia cha kofia mbili kama siraha ya kulinda chama na serikali incase kama itatokea kama alivyopata kuitumia Rais Mstaafu BWM, tena akiwatamkia thahiri wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.

  Kwa wapenda mageuzi mfumo wa kofia mbili [STATE NA PARTY POWER] sio mwema hata kidogo kwa maana kwenye demokrasia ni mfumo unao walewesha chama husika.kupitiwa na kijisau kuwa wameazimwa madaraka na UMMA na kuwa MADARAKA NI MALI YA UMMA.

  Lakini uamuzi wa kuondoa madaraka hayo kutoka ndani ya chama tena pasipo hiari au ushawishi wa Rais husika hayo ni mapinduzi ndani ya chama.Ilipaswa Rais asimamie mchakato huo yeye akiwa kiongozi asilia wa mageuzi hayo, yaani Rais awe ndie mmilki wa AGENDA hiyo kwa maana ya nia ya kukisaidia chama kupambana na mageuzi asilia ya UMMA kutaka Chama Kijitoe kwenye kumilki madaraka [ABSOLUTE PEOPLE'S POWER] na kubaki na jukumu la exercise Power kupitia Sanduku la Uchaguzi pindi wanaposhinda na kuingia madarakani na kuunda serikali [DOLA].

  Kwa hili JK hongera kazi moja ni kuthibitisha kuwa anaweza na alipitiwa kama bindamu yoyote yule na kuwa utamaduni wa kitanzania wa kuthaminiana kwenye urafiki na kosa la mwanzo la kuamini Rafiki atabadilika kuwa mfuasi wa ITIKADI YAKO alitajirudia. Tufike sehemu kwa walio watu wazima wanajua staha ambayo walihivika kama jamii haswa ndani ya chama cha Mapinduzi.Swala la kuwajibishana kwa watu wazima wa umri kuanzia miaka 45- kuendelea hilo limekua ni JIPU/BOMu ambalo madhara yake CCM wamejifunza kupitia mwitikio wa UMMA [Respond] [Chini ya kauri mbiu za chama cha mapinduzi kama HUYU NI MWENZETU/NDUGU YETU].Kauri hizo ziliondoa sura ya uwajibikaji na kukosoana pindi mwanaccm anapokosea ama kutenda ndivyo sivyo kwenye jamii, utetezi uliowekwa mbele ulikua huyu ni mwenzetu.

  Impact hiyo kiibidamu mtetewaji alipaswa kubadilika lakini kwa mfumo [system] ulivyomlevya anashindwa kutambua kua anawajibika kwa kosa lile na kutumia fursa aliyopewa na wenza [wanaccm wenzake] kujirekebisha anajikuta anaongeza wigo wa makosa na kuzalisha wafuasi wa utetezi wa makosa hayo kuyafanya ni njama dhidi ya chama cha Mapinduzi na maadui wasio wanachama wa CCM na mtu akiipinga matendo ya viongozi wa CCM viongozi wasio waadilifu ugeuka na kusema mpingaji anaipinga nchi.

  Ingawa Mageuzi haya Mwenyekit yeye binafsi litamuachia KOVU KUBWA bali litamletea Heshima yeye na kumpa nafasi nyingine ya kuonyesha imani ya watanzania wengi waliyokua wameiweka kwake kufikia hatua ya yeye kuonekana si lolote,Ingawa watanzania walimwamini yeye na walikua na imani nae,na kwa vichwa viwili hivyo ambavyo ni matunda ya uumbaji wake ana nafasi ya kulekebisha muundo atakao taka mwenyewe kwani anakila uwezo na nyenzo za kufanya hivyo bila kuhujumiwa kwa sasa.
   
Loading...