Mtizamo wa Bloga: Ama Kweli Mungu si Tambwe Hiza! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtizamo wa Bloga: Ama Kweli Mungu si Tambwe Hiza!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kulikoni Ughaibuni, Jan 22, 2011.

 1. Kulikoni Ughaibuni

  Kulikoni Ughaibuni JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2011
  Joined: Dec 12, 2007
  Messages: 234
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 60
  [​IMG]

  Imagine wale vibaka wanaowanyima raha pale mtaani wasingekuwepo!

  Imagine baba au mama mwenye nyumba angeheshimu mkataba mlowekeana kuhusu jengo unalopanga kwake,na kutambua kuwa kodi unayolipa ina-cover uhuru na haki zako kama mpangaji!

  Imagine waandaaji wa filamu za kibongo wangezingatia zaidi uwezo na vipaji vya waigizaji badala ya maumbile au "jina kubwa" (kama sio rushwa za ngono)!

  Imagine vituo vya redio vinavyojigamba kuwa vinawalenga vijana vingeachana na watangazaji vilaza wanaojifanya kuifahamu siasa (na hivyo kujipachika wadhifa wa political analysts/commentators) japo wanatambua uwezo wao ni zero,zilch,nada,sifuri,kaput!

  Imagine ajira na promosheni makazini vingezingatia ujuzi na uwezo badala ya kujuana plus undugunazesheni (not forgetting rushwa za ngono)!

  Imagine baadhi ya wachunga kondoo wa Bwana wangetambua kuwa wanamkasirisha Muumba kwa "kugeuza kondoo wake kuwa vitoweo vya bure" japo wakiwa madhabahuni wanakemea kwa nguvu zote ubanjuaji wa Amri ya Sita!

  Imagine na sie mabloga tungejifunza kutoka kwa kampeni ya Rais Obama na,kwa hivi karibuni kabisa,Tunisia,na kuwekeza nguvu zetu katika matumizi ya social media ku-address matatizo yanayoikabili nchi badala ya hali ilivyo sasa ambapo baadhi yetu wako bize zaidi kujikomba kama sio kuripoti tu matukio (na hapa tunaweka kando wenzetu ambao wako bize zaidi na "flani kafanya hili au lile" badala ya nini kifanyike kuikomboa jamii yetu)!

  Imagine vyombo vya habari vinavyoendeshwa kwa fedha za walipa kodi vingetambua kuwa kazi ya kupigia debe CCM inapaswa kuachwa kwa Uhuru,Mzalendo na Redio Uhuru pekee!

  Imagine Kamati Kuu ya CCM ingekuwa na wazalendo wa kutambua kuwa hata kichaa akiporwa hawezi kumlipa aliyempora,sembuse wao watu wenye akili timamu na wenye dhamana ya kutuongoza lakini wanaendekeza ufisadi na kuhalalisha malipo kwa majambazi wa Dowans!

  Imagine....Imagine...Imagine...Too much imagination

  And imagine,fani ya siasa Tanzania ingeachwa kwa wenye wito,uwezo na uzalendo badala ya hali ilivyo sasa ambapo kila Tom,Dick and Harry anayeweza kununua wapiga kura anaweza kulala jambazi akaamka mbunge,kama sio waziri au mkurugenzi wa hovyo hovyo!

  Na imagine ulimwengu wa siasa za Tanzania ungekuwaje laiti baadhi ya viumbe wangetambua umuhimu wa co-ordinationa kati ya ubongo na mdomo kabla ya kuropoka lolote hadharani.Kwa hakika dunia ingekuwa mahala bora sana pa kuishi laiti baadhi ya wanasiasa wasemaovyo,vichwa maji,vichwa makabati matupu,nk wasingepewa fursa ya kuongoza hata kundi la mifugo,let alone kuongoza wananchi.

  Yes,dunia ingekuwa mahala bora kabisa laiti watu kama Yusuph Makamba na Tambwe Hiza wasingeruhusiwa kutamka lolote hadharani hadi itakapothibitika kuwa watakachoongea hakitazidi kuisogeza Tanzania yetu kuelekea kwenye mshikemshike kama wa huko Ivory Coast, au mahala kwingine kwenye mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.


  Talking of Tambwe Hiza,nimeshindwa kujizuwia kupaliwa na kicheko baada ya kukutana na habari ifuatayo:

  Lol!Mchimba kisima katumbukia mwenyewe kisimani.Jitu zima ovyooo!Linaropoka tu,na kujipachika udaktari wa magonjwa akili to an extent of kum-diagnose Dkt Slaa na maradhi ya akili,kumbe lenyewe lina matatizo makubwa ya afya.Msomaji mpendwa,huhitaji hata dakika moja ya kozi ya utabibu kumaizi kuwa kichaa cha kuzuzshiwa hakifui dafu kwa gonjwa la hatari kama PUMU na SHINIKIZO LA DAMU.

  Naomba nisiwe mnafiki kumwombea Tambwe apate nafuu.Ndio,Biblia inatuasa kuwapenda maadui zetu lakini busara katika jamii zinatuasa pia kuwa ADUI YAKO MWOMBEE NJAA (njaa hapo symbolises mambo mabaya kama hayo yalomkuta Msema Ovyo Tambwe Hiza).

  Kufungika kwa mdomo mmoja mchafu kunaifanya dunia kuwa mahala bora kabisa kuishi.Sio siri kwamba laiti maradhi yanayomkabili Tambwe yakipelekea kupunguza,kama sio kumaliza,tatizo lake la kuutumia ubongo wake kama matope,kisha kuunyima ubongo huo ushirikiano na mdomo wake,and therefore kupelekea uropokaji usiosahili hata kwenye vilabu vya gongo,siasa za Tanzania zinaweza kuchukua sura mpya.Yaani,siasa minus mbwatukaji mmoja ambaye kauli zake za ovyo ovyo ni maarufu zaidi kuliko madaraka yake.

  Ndio maana nimeandika hapo juu kuwa MUNGU SI TAMBWE HIZA.Yeye anajifanya kumsemea ovyo Dokta Slaa,na kumhukumu kuwa ana kichaa,ilhali yeye Tambwe ndiye mwenye matatizo makubwa ya kiafya yanayoweza kabisa kuwa na uhusiano na tabia yake ya kuropokaropoka.

  IMAGINE SIASA ZA TANZANIA MINUS UROPOKAJI WA TAMBWE HIZZA!SURELY,THAT WOULD MAKE THE WORLD SUCH A WONDERFUL PLACE TO LIVE...Lol!

  KULIKONI UGHAIBUNI: Ama Kweli Mungu si Tambwe Hiza
   
 2. n

  ngoko JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  VUVUZELA la JK
   
 3. doup

  doup JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2011
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  jamaa hatumii kabisa up stair yake vizuri, nilimsikiliza jana kwe kipim joto cha ITV,Ni aibi, nafikili Makamba atapiga tena marufuku wanachama wa ccm kushiliki kwenye midahalo ya katiba
   
 4. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #4
  Jan 22, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  Na imagine tungelipa mikopo wanafunzi wetu na kununua madawa kwenye hospitali zetu badala ya kukimbilia kuwalipa Door-ones na ushenzi mwingine
   
 5. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #5
  Jan 22, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,293
  Trophy Points: 280
  Alikuwa anatia kinyaa!! Sijui kiwango cha upeo wa akili zake darasani kilikuwaje! Napata picha mtu kama TH yeye ni pangu pakavu tia mchuzi, popote penye ulaji ndiko wanakoegemea na pasipo na chochote hawana haja napo. Mtu wa aina ile hata urafiki hafai na haaminiki hata kwa amana ya kutupa uchafu. Jana alionesha wazi ni aina gani ambayo Viongozi na wanachama walio wengi wa CCM wanawahitaji. Hana uchungu hata chembe na taabu za wananchi wala uongozi wa kiwajibikaji kwa nchi hii yeye kila kitu anakiona sawasawa! Inaonesha huyu ndiye Al-Sahaf haswa wa CCM na serikali yake. Na ikiwa hali ndio hii basi tena!!
   
 6. Mkereketwa

  Mkereketwa JF-Expert Member

  #6
  Jan 22, 2011
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli jinsi huyu jamaa alivyoboa jana, nashswishika hata kuuliza kiwango cha elimu yake ni level gani? Mwenye data tunaomba, maana mnaweza kuta mnamchambua mtu hapa kumbe tatizo ni upeo wa elimu hana plus kukosa busara = Ni balaa tupu.
   
 7. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #7
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Si ya katiba tuu... sababu wote ni pumba atazuia kila kushiriki kila aina ya midahalo!!!:A S-fire1:
   
 8. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #8
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nilisikiliza japo kwa sehemu kipindi cha ITV-Kipimajoto!!!!
  Maneno na jinsi huyu jamaa Tambwe Hiza, na kupima na nafasi yake katika CCM!!!!!!!!!! Sikuamini masikio yangu!!!!!!!!!!!!
  Tambwe Hiza na Makamba (kuhusu tukio la Arusha) hakuna tofauti!!!!!!!!!!!!!!!!
  Hii CCM ya sasa ni wazi inapeleka nchi pabaya sana-pimeni matamshi yao kuhusu masuala nyeti ya kitaifa.
   
 9. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #9
  Jan 22, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo hukumu ya kesi inayoendelea huko Arusha imeshapangwa na serikali ya CCM?
   
 10. Kulikoni Ughaibuni

  Kulikoni Ughaibuni JF-Expert Member

  #10
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 12, 2007
  Messages: 234
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 60
  You're a mini-Tambwe Hiza,if not Tambwe himself,I suppose.
   
 11. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #11
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Huyo ni mwanae ndo maana kauli zao zinafanana na Makamba ndiye
  aliyemuweka pale
  Hivi kule TOT plus nafasi zilijaa?
   
 12. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #12
  Jan 23, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  It takes a lot of energy to be stupid.
  Ugua salama Kilaza Tambwe.
   
 13. S

  Skype JF-Expert Member

  #13
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 7,284
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Vilaza kama tambwe hiza ni wengi mno ccm, kwa wale tunaofuatilia wizara ya elim, huwezi kumtofautisha tambwe hiza na bogus mwingine kama pita msolwa, jumanne magembe, mwantumu mahiza, josefu mungai na wengine wengi kama hao.
  kichaa akikukwapua nguo zako haina haja ya kukimbizana nae, mwache tu ataumbuka mwenyewe kama Dr. Slaa alivoliacha likilaza tambwe liropoke weeeee matokeo yake limeumbuka lenyewe.
   
 14. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #14
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,515
  Likes Received: 1,685
  Trophy Points: 280
  crap
   
Loading...