Mtindo wa Misiba ya Siku Hizi: Watoto waliozaliwa mijini (1990's) wanavyokataa kusafirisha miili ya wazazi wao kwenda kuzikwa kijijini na kupasua ukoo

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,316
Je, kuna umuhimu wa wazazi kuwapeleka watoto kijijini wakati wa kipindi cha likizo? Unawapelekaga watoto wako?

Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu watanzania;

Siku za hivi karibuni nimekuwa nikishuhudia matukio mengi sana zaidi ya mara 4 katika misiba niliyopata kuhudhuria ambapo watoto waliozaliwa mijini (1980's - 1990's) wanavyokataa kusafirisha miili ya wazazi wao kwenda kuzikwa kijijini na kusababisha mpasuko wa mahusiano ndani ya ukoo.

Kwa hapa Tanzania, makabila yetu yamegawanyika katika makundi makuu mawili. Kuna makabila ambayo kuzika mtu kwao sio jambo la maana sana kiasi kwamba hata ukifia Magomeni wao kukuzika makaburi ya Kinondoni ni kawaida tu.

Kundi la pili ni yale makabila ambayo ni mwiko kabisa kuzika mwili wa ndugu yao nje ya kijiji. Yaaani kama mtu alifia Dar, basi ni lazima asafirishwe mpaka mkoa wa Mara, tena akazikwe katika makaburi ya ukoo.

Hata kama mtu amekufa tuseme huko Ulaya, basi ni lazima aletwe kutoka huko New York mpaka Rorya hukoooo Shirati au Utegi. Juzi hapa nilienda katika msiba mmoja hapa jirani na nilipopanga wa watu wa kabila moja la huko Mkoa wa Kigoma.

Katika msiba huu ndio ninakutana na hiki kisanga cha watoto 3, ambao financially wapo njema sana na mmoja wao ni Country Manager wa kampuni moja ya wazungu huku Dar tena ni mtoto wa kiume.

Sasa wakuu ninaomba kujua chanzo kikuu ni nini? Je, ni wazazi wenyewe kutopenda kuwapeleka watoto kijijini wakati wa kipindi cha likizo ya mwaka ili wajuane na mazingira pamoja na ndugu zao wa huko au shida ipo wapi hapa wakuu?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Watoto ambao hawajazoea kwenda kijijini wanakomaa wazazi wazikwe Dar .. sababu wanaona usumbufu kwenda mkoani kusafisha kaburi ama kuombea wazazi wao makaburini kila baada ya muda.

Pongezi nyingi kwa wachaga.. kwa kuzoesha watoto kwenda Moshi mara kwa mara
 
Maisha ya kuzika ndugu kwenye makaburi ya manispaa ni ya ajabu ila ndio hivyo mjini watu hawana viwanja vikubwa au wengine wamekulia kwenye nyumba za kupanga hamna sehemu ya kuzika.

Watoto wa mjini wakiona nyumba mjini ina kaburi mbele wanashangaa hasa wazaramo.
Ni heshima kuzika kwenye ardhi ya kwenu hata kama ni kijijini
 
Je, kuna umuhimu wa wazazi kuwapeleka watoto kijijini wakati wa kipindi cha likizo? Unawapelekaga watoto wako?
Kuwapeleka watoto vijijini kuna faida nyingi tusizozielewa. Licha ya kujua maneno ya kilugha, watajua ndugu, mila na desturi.

Pia watakwenda shambani na kuona kilimo cha mazao kinavyofanyika. Hili linapanua upeo wao ki elimu. Watoto wa mijini hawajawahi kuona nanasi likiwa shambani.

Watoto wa mijini wengine hawajawahi kuona milima. Ukipita Uruguru pale unawaonyesha watoto milima ya Uruguru na kuwaambia kuwa hii ni mfano ya milima meza kama ya Usambara.
 
...
Pia watakwenda shambani na kuona kilimo cha mazao kinavyofanyika. Hili linapanua upeo wao ki elimu. Watoto wa mijini hawajawahi kuona nanasi likiwa shambani.
....
... wanakutana nalo mezani tu; sana sana wakilifanyia kazi ni kulitoa kwenye friji kupeleka mezani kwa maelekezo ya mama! Ha ha ha! Hatari sana hii.
 
Sasa 'nimefia' zangu Marekani ( japo sijawahi kufika na huenda hadi nikienda Udongoni sitofika pia ) na inasemekana Nauli ya Kunileta 'Sandukuni' kwa Mbung'o ( Ndege ) kwa sasa ni kama Tsh Milioni 25 mpaka 30 za Kitanzania.

Sasa kwanini tu 'nisizikwe' huko huko Marekani na hiyo Hela itumike kuwasaidia Wazazi wangu na Ndugu zangu huku Tanzania ili na Wao hata wakiwa 'wameshiba' zao Matembele na Maharage yao wanaweza 'wakajifariji' kwa Majirani kuwa wana Ndugu yao Mmoja 'Popoma' amezikwa kwa Donald Trump Marekani na Wakasifiwa vile vile?
 
Sasa 'nimefia' zangu Marekani ( japo sijawahi kufika na huenda hadi nikienda Udongoni sitofika pia ) na inasemekana Nauli ya Kunileta 'Sandukuni' kwa Mbung'o ( Ndege ) kwa sasa ni kama Tsh Milioni 25 mpaka 30 za Kitanzania.
It's too expensive to carry a body of the deceased from abroad to Tanzania. Ni wachache sana huweza kumudu gharama hizi...
 
Mada hizi zinachanganya sana watu. Mzazi alitokea kijijini, akiomba azikwe kijijini tutajitahidi tumpeleke, lakini uwezo ukipatikana.

Mnaweza kuwa na nia nzuri ya kumpeleka lakini nauli ikawa shida kuipata, sidhani kama mtalazimisha. Mtafanya mtakavyoweza kwa wakati huo.

Binafsi ningependa nizikwe kijijini kwa baba yetu, lakini kama uwezo utakuwepo wakati nafariki na watakao kuwepo wakiweza kunifikisha huko itakuwa vyema, lakini siyo lazima ikiwa uwezo utakuwa mdogo kusafirisha mwili.

Ila kama marehemu uliacha pesa na utaratibu wa kuzikwa kijijini kwenu na isiwe hivyo hapo kweli tuliobaki tutawalaumu vijana.

Kila mtu anapenda apendavyo.
 
Kuwapeleka watoto vijijini kuna faida nyingi tusizozielewa. Licha ya kujua maneno ya kilugha, watajua ndugu, mila na desturi.

Pia watakwenda shambani na kuona kilimo cha mazao kinavyofanyika. Hili linapanua upeo wao ki elimu. Watoto wa mijini hawajawahi kuona nanasi likiwa shambani.

Watoto wa mijini wengine hawajawahi kuona milima. Ukipita Uruguru pale unawaonyesha watoto milima ya Uruguru na kuwaambia kuwa hii ni mfano ya milima meza kama ya Usambara.
Vijiji vyenyewe vishaanza kuwa miji.
Tofauti ni idadi ya watu tu.

Maisha hayawezi kufanana siku zote, mabadiliko yapo na lazima tutapokee.

Jambo la msingi hapa kwamba bu vizuri kuwa na mahusiano mazuri na watu wengi wa jamii yako uliyokulia au ambayo ukoo wako walio wengi wanaishi.
 
Siyo kosa kusafirisha mwili wa mpendwa wako, lakini siyo suala la kufa na kupona.

Maana hilo si jambo la kiibada kwa hizi dini zetu kubwa.

Kusafirisha mwili ili kumzika alikozaliwa kuna kiasi furani cha upagani.

Maana baadhi ya mira za kiafrika makaburini ni sehemu ya kufanyia IBADA (Maombi).

Kwahiyo baadhi ya makabila yetu hupenda ukaribu na wafu wao ili wasipate usumbufu wakati wa matambiko.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom