Mtindo wa Misiba ya Siku Hizi: Watoto waliozaliwa mijini (1990's) wanavyokataa kusafirisha miili ya wazazi wao kwenda kuzikwa kijijini na kupasua ukoo

Ukweli utabaki pale pale, hakuna mtu atajenga makaazi ya kuridhisha na kuweka mazingira safi kijijini kwao alafu asiwe na tabia ya kuwapeleka watoto wake au yeye kwenda kijijini walau mara moja kwa mwaka, wasiokuwa na tabia ya kwenda kijijini mara nyingi hata mazingira hawajandaa vizuri. Nimejifunza kwa Wachaga na Wahaya, ukweli hawa watu utamaduni wao unaendana wote wanajitahid sana kutengeneza makwao vijijini ndiyo maana walio wengi wanazikwa kwao na pia wanatabia za kuwapeleka watoto kwao.
Okay...
 
Last week nilihudhuria msiba mmoja wa kichaga, walizika hapa hapa mjini ila tukiwa msibani ilionekana wachaga wengi hawajaridhika maziko kufanyika dar hata askofu kwenye misa ya mazishi alisema mila zisizo na ulazima zinaweza kuvunjwa tu na ikasemekana marehemu na mumewe walishakubariana kuwa wakifa hamna kwenda moshi tunazika dar, yani maana yake hata mzee mwenyewe akifa atazikiwa dar, hii ni familia haina njaa pia ni influencial sana hata msibani mdee na gwajima walikua wanapigana sana vikumbo kuonesha kila mmoja yupo karibu nao, nikajifunza kama wachaga wamefikia kuzikwa dar basi soon kila mtu atazikwa alipoishi.
 
Last week nilihudhuria msiba mmoja wa kichaga, walizika hapa hapa mjini ila tukiwa msibani ilionekana wachaga wengi hawajaridhika maziko kufanyika dar hata askofu kwenye misa ya mazishi alisema mila zisizo na ulazima zinaweza kuvunjwa tu na ikasemekana marehemu na mumewe walishakubariana kuwa wakifa hamna kwenda moshi tunazika dar, yani maana yake hata mzee mwenyewe akifa atazikiwa dar,
Okay...
 
hii ni familia haina njaa pia ni influencial sana hata msibani mdee na gwajima walikua wanapigana sana vikumbo kuonesha kila mmoja yupo karibu nao, nikajifunza kama wachaga wamefikia kuzikwa dar basi soon kila mtu atazikwa alipoishi.
Sawa mkuu
 
binafsi hata mtoto wangu sipendi aitwe hata jina la babu au bibi yake marajina la mjomba,shangazi yake nk.

sasa kuhusu kuzika kijijini ndio kabisa naona ni upuuzi kwa mawazo yangu lakini
 
binafsi hata mtoto wangu sipendi aitwe hata jina la babu au bibi yake marajina la mjomba,shangazi yake nk.

sasa kuhusu kuzika kijijini ndio kabisa naona ni upuuzi kwa mawazo yangu lakini
Kama pesa ipo kuzikana kijijini ni jambo jema sana mkuu
 
Kwa view nzuri namna hii, zinapatikana kijijini tu!
IMG_20200401_094053_3.jpg
 
Hali ya maisha imebadilika,unakuta mtu kwao Tarime,halafu kafia mtwara,hao wanaodai maiti iletewe kijijini hawachangii hata mia
 
Uchumi baba hali ya maisha imebadilika!
Zamani tu kwenye kuzika misiba ya wakristo mfano ilikuwa inakaa mpk siku 4 au 5 watu wanakula na kunywa ila sahv ukifa leo kesho au keshokutwa tunakuzikaaa

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Sio kuwapeleka watoto nyumbani likizo. Kama bado una wazazi wako baba, mama, mashangazi, wajomba, n.k unaowaamini au ambao walikulea na wewe na bado wapo kijijini, peleka wanao wakasomee huko angalau elimu ya msingi tu alafu watoe waendelee na elimu zingine huku mjini. Hii itawafanya sio kujua nyumbani bali kuwa sehem ya jamii ya kwenu. Pili watapapenda sana kwa moyo wao na watakuwa wanataka wenyewe kwenda na sio kuwalazimisha kwenda kwa sababu wana moments nyingi sana za kukumbuka huko nyumbani, wana marafiki waliokua nao huko tangu utotoni, n.k. Lakini pia unawafungulia nafasi ya fursa nyingine nyingi kwa kuwa watakuwa na uwezo wa kurudi kijijini kutumia fursa zilizopo ukizingatia mijini kumeshakuwa congested na fursa nyingi ziko occupied. Mfano mtu anaweza kurudi kijijini kugombea hata nafasi za kisiasa kama udiwani, ubunge, n.k na bado akafanikiwa maana anatambulika na jamii yenyewe.

Lakini pia watoto wakikulia kijijini wanakuwa warithi wa boma na mashamba yenu na kuyaendeleza. Mfano mzuri mimi niliacha kazi Standard Chartered Bank mwaka 2015 nikarudi kijijini nikapewa mashamba na babu nikaanza kilimo na sasa nimepiga hatua na nimefungua kampuni ya masuala ya kilimo. Babu alinipa mashamba nikalime kwa kuwa nimekulia kwake na anaona kabisa baba yangu na baba wadogo wameshalowea mjini hawawezi kurudi kukaa tena kijijini. Sasa babu ameshafariki mimi ndio jicho la ukoo mzima maana baba na baba wadogo wote na familia zao wakija wanafikia kwangu na hata wao kama Mungu akiwachukua wana uhakika familia yetu ina mtu wa kuendeleza heshima yake pale kijijini japokuwa watoto wao wengine hawataki kukaa kijijini ila wanapendaga kuja kwa ajili yangu.

Watoto wakifanikiwa kurudi kijijini hata nyie wazazi mnakuwa na hamu ya kwenda kijijini.

N.B: Japokuwa kila jambo lina faida na hasara zake na ndo maana wengi hamko tayari kupeleka watoto wenu wakalelewe na wazazi au ndugu zenu kwa kufikiria ndo kuwapenda sana, ila pia ina faida sana kwa upande mwingine na kwa baadae.

Unawapeleka wanakuja kulogwa unafikiri kwa nini watu hawataki kurudi
 
Kwenye koo zetu kwa baba na mama ukivuta lazima ukazikwe kijijini..tena makaburi utakuta yamepangwa Kama kuanzia babu wa babu hadi namna wanavyoendelea kuzika.
Mimi sitaki wanipeleke kijijini basi tu
 
Back
Top Bottom