Mtindo huru (Free style)

Sanda Matuta

JF-Expert Member
May 9, 2007
949
140
Wakubwa zangu,na wakuu wenzangu!
Napenda kuwasalimu kwa lugha ya kwetu.
Mambo! Nadhani kwa pamoja mtajibu Poa tu!
Katika kuinzi na kuiendeleza kiswahili chetu.
Napenda kuileta kwenu Thread hii hapa kijiweni kwetu.
Tupate kuchangia tuliendeleza mapambano katika nchi hii yetu.
Kifikra,Uchumi, na kwamendeleo kwa ujumla pasipo kuchangia thread za siasa tu.
Mitindo huru inakuja kutokana na POST ya mmoja Mwenzetu.
Naomba ku-quote hapa china na hicho kizungu ni kuonyesha masititizo.......tu.,

"Nina wazo. Kutokana na baadhi ya wana jf kuonyesha kipaji cha kuandika mashairi, kwa nini tusianzishe kamtindo ka kuchagua mada halafu kila mpenda kuandika shairi anaandika shairi lake kuhusu hiyo mada? Nafikiri hii style itachangamsha zaidi utundu wa mashairi, zaidi ya kumsubiri mkjj atoke halafu ndio ajibiwe.

Pengine tunaweza kutengeneza kitabu cha jf mashairi na kupeleka huko mashuleni kitumike. Who knows?

Ni wazo tu!


Huyu bwana aniitwa QM..!

Mitindi huru inakuja kwa ajiri hii,ya kwamba sikumoja watoto wetu wajue hata humu chini chini (JF) Kiswahili kilitumika kupinga UFISADI na mambo yote mabaya yanayo endelea humu nchini kwa kipindi hiko.

Maishairi,naambiwa ni Lugha ambayo hata vitabu vikuu vitakatifu vya DINI vimeandikwa yaani kwa maneno mepesi hata MUNGU muumba ametumia mashairi kuwaletea ujumbe wanaadamu.
Sasa tafadhali shime wenzangu wale wajuao na wale wajifunzao huu na hii ndio muda na nafasi kwa ajiri ya kiendeleza Lugha,kutoa ujumbe na kufurahii kutokana na hizo JUMBE (kuburudika).

Mitindo huru inaruhusu mashairi yanayo fata misingi ya kishairi na yasio fata ilimradi tu kunakitu ndani ya shairi hilo.


..............Karibuni wote..................

Sanda Matuta.
 
Nakuja kwenye mitindo huru.
Nahapa wala silipii ushuru.
Kusema yote bila kujikitheru.
Mwkjj alikuja hapa na Mbuzi.
hatukuelewa tukaanza kupiga niluzi.
Wengine wakasema ipoa labda ni nazi.
Hapana si nazi ni maladhi.
UFISADI kama kazi.
Walificha sasa wazi wazi.
 
Malenga wa Bara,na wale Pwani.
Wale wa Ulaya,na wa Unyamwezini.
Labda sikueleweka,najileta upenuni.
Wako mtindo weka,wala usiuweke kapuni.

Sema unavyo weza,kama ni yule Mkapa.
Au hata Mzee Ruksa,Usisite hata Lowassa.
Kama Mwakembe sema,hata mzee wa vijisenti.
Watu waishi chini ya dola,alafu analeta ushenzi.

Mtindo huru,weka shairi.
Usiseme Mbuzi,sema Raisi.
Nasema wazi,Mawaziri ni wezi.
Hichi ni kigano,kama mfano.
 
Nami nazama uwanjani
kushusha yalo moyoni
Wenzangu bara na pwani
twatafuta mchawi nani
Anaozamisha chombo majini

Wanaozamisha si twawajua
Mbona twatoa macho kama kibua?
Si kuna hatua zakuchukua
Au watanyesha mvua
Yenye mateso na surua?
 
ukimya sasa wanishinda
nami nataka kusema
kwanini mti tupande wote
matunda ule mwenyewe
 
Tutaongea yalo maana
Kwa wazee na vijana
Hatubaki kushika tama
Hatuachi chombo enda mrama
Hatutotaka kuoneka wema
Ili tu aburudike rama

Ni vema tukasongea
Watu kuwaelezea
Kwamba hatutopea
Tukiacha kuongea
 
Mwenye kupanda hali,
mwenye kula hakupanda,
kwanini hili ni kweli,
mwenzenu limenishinda!
Natatizika kauli,
Mbele tena sitokwenda
Matunda yote mawili
Anakula asopanda!

Shamba hakusafisha,
Na ardhi hakuilima
Wa kwanza kutaifisha
Haraka ataka chuma,
magugu hakusafisha,
Hata heka hakulima,
Nini kimempofusha,
Matunda kutaka chuma?

Moja, mbili, au tatu,
Yeye ataka rudia,
Kuchuma kwa roho kwatu,
Yale asiyolipia
Hivi kweli huu utu,
Kazi usivyofanyia
Mimi leo nina kutu,
Mbali namfukuzia!
 
Waweza panda ufuta
Ukaona kama si mali
Kwa pembeni wakakuteta
Wakafanya udalali
Waweza kuwa kuruta
Ukaona si dili
Mgambo akafutuka
Akakuona fahali

Wengi wapanda mazao
ila wengine ndo wavunao
Wachache wana peteo
wamevifanya vya kwao
Wakipigwa tafrao
watetema kama cheteo
 
Katu si kitu sakata
sakata liso matata
kwani anataka
takataka na utata
utata wenye mashaka
nakataa katakata.

sitishiki na mikiki
mikiki iso mantiki
kwani lini lini mchikichi
ukazaa matikiti
au lini mtikiti
ukazaa parachichi
kuhusu wao mkakati
nimekataa mwenyekiti
mafisadi wanafiki
tutawasaga tikitiki!
 
ukifika juu kinachofuata ni kudondoka chini,
Siamini kama Lowasa leo unakunywa bia kwa macheni,
Alifuata msabaha na baadae karamagi,
Lakini hayo yote yanamaanisha mmeumiza wengi,
Ukipenda cha wizi utaishia jela,
Losawa unastahili segelea,
Chenge ulikua juu sasa uko chini kama mzoga,
anaefuatia ni Kapuya na Mgonja,


I like free style
 
Back
Top Bottom