MP CHACHANDU
JF-Expert Member
- Dec 4, 2016
- 875
- 616
Haya yamebainishwa na waziri Wa fedha ndugu Mpango katika mazungumzo yake ya ripoti ya hali halisi ya uchumi Wa Tanzania.
"Madai ya biashara nyingi kufungwa: Kwa upande wa madai ya biashara nyingi kufungwa katika siku za karibuni, tumefuatilia na kwa kiasi fulani kuna ukweli. Imebainika kwamba kasi ya wafanyabiashara kufunga biashara zao imeongezeka kati ya mwezi Agosti na Oktoba 2016. Mfano Ilala 1,076, Kinondoni 443, Temeke 222 na Arusha 131. Aina ya biashara nyingi zilizofungwa ni katika sekta ya ujenzi na biashara ya jumla na rejareja, na chache katika huduma za usafiri.
Hata hivyo, sababu hasa zilizopelekea biashara hizo kufungwa hazijabainika kutokana na ugumu wa kupata taarifa kutoka kwa wenye biashara zilizofungwa.
Sababu za mtu kufunga biashara yake zinaweza kuwa nyingi, ikiwemo, kushindwa kuingiza bidhaa nchini bila kulipa kodi stahiki, kushindwa kulipa au kulipwa madeni, kubadilisha aina ya biashara, kushindwa kusimamia biashara, gharama kubwa za uendeshaji, wabia katika biashara kutoelewana au kutapeliana, kuibuka kwa washindani wa kibiashara wenye nguvu au huduma bora zaidi n.k."