Tetesi: Mtikisiko: Chama kipya cha Kutetea Haki na Maslahi ya Waalimu Tanzania chaanzishwa

busar

JF-Expert Member
Dec 22, 2011
1,068
1,061
Karibu ndani ya Chama cha Kutetea Haki na Maslahi ya Waalimu Tanzania (CHAKAMWATA). Hiki ni chama mmbadala wa CWT, nk.
Ukijiunga na chama hiki utapata faida kadhaa ambazo huwezi kuzipata ukiwa CWT. Baadhi ya faida hizo ni:

Mosi; utakatwa 1% tu ya mshahara wako tofauti na CWT wanaokata 2% ya mshahara wako. Hivyo haya ni maajabu pekee yanayotokea huko CWT dhidi ya "haki" inayopatikana CHAKAMWATA.

Pili; ukistaafu kazi, ukisimamishwa kazi au kifo-kwa mwanachama, utarejeshewa nusu ya mchango uliochangia ndani ya chama, tofauti na maajabu yanayofanywa CWT.
KARIBU
 
mmechelewa sana cwt ilipofikia ni chama kikubwa sana miradi na benki pamoja umoja uliojengwa siku nyingi itakuwa kazi kuuvunja

Je kile cha nyanda za juu kusini kimefia wap?
 
Ni afadhali wengine waanze kujitambua ili wapambane na huyu dikteta uchwara kwa maana amedhamiria kuwatesa watumishi wa umma hasa hao washika chaki ambao wengi wao wana elimu duni huku wakiishi kwenye umaskini wa kiwango cha makinikia.
 
Mods hii sio tetesi,mimi mwenyewe nimeshajiunga tayr nichama kizuri kinaonyesha huenda kikatanguliza maslahi ya Mwl mbele
 
mmechelewa sana cwt ilipofikia ni chama kikubwa sana miradi na benki pamoja umoja uliojengwa siku nyingi itakuwa kazi kuuvunja

Je kile cha nyanda za juu kusini kimefia wap?
Bado hata cwt itatamba miaka kadhaa maana hata idadi ya wanachama ni wengi. Hiki kimeanzishwa kipindi ambacho ajira za walimu zimepungua kwa kasi. Hiki kupata wanachama elfu thelasini tu itakua ishu wakati kipind kilichopita cwt alikua anapata idad kama hiyo kila mwaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ndo mmeanza mnakata 1% sidhani kuwa nyie ni tofauti na CWT..
Anyways.. Pamoja na yote mjiweke mbali na CCM..!!
 
Walimu kweli wanafanywa kichwa cha mwwndawazimu.
Hamna pahali mlipoonyesha kuwa mtamwambia Sizonje awaongezee mshahara au posho.
Wakitimia 1000 tu katiba mnachange ,inakula kwao.
 
Walimu wana shida kweli pamoja nakuelimisha taifa bado hawajitambui mpaka watetezi mfike au ni janja ya kujipatia vipato vya walimu mkaa kwa mgongo wa kuwatetea
 
Karibu ndani ya Chama cha Kutetea Haki na Maslahi ya Waalimu Tanzania (CHAKAMWATA). Hiki ni chama mmbadala wa CWT, nk.
Ukijiunga na chama hiki utapata faida kadhaa ambazo huwezi kuzipata ukiwa CWT. Baadhi ya faida hizo ni:

Mosi; utakatwa 1% tu ya mshahara wako tofauti na CWT wanaokata 2% ya mshahara wako. Hivyo haya ni maajabu pekee yanayotokea huko CWT dhidi ya "haki" inayopatikana CHAKAMWATA.

Pili; ukistaafu kazi, ukisimamishwa kazi au kifo-kwa mwanachama, utarejeshewa nusu ya mchango uliochangia ndani ya chama, tofauti na maajabu yanayofanywa CWT.
KARIBU

kwa hio lengo lako ni makato????

nyambaffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffffff
 
Karibu ndani ya Chama cha Kutetea Haki na Maslahi ya Waalimu Tanzania (CHAKAMWATA). Hiki ni chama mmbadala wa CWT, nk.
Ukijiunga na chama hiki utapata faida kadhaa ambazo huwezi kuzipata ukiwa CWT. Baadhi ya faida hizo ni:

Mosi; utakatwa 1% tu ya mshahara wako tofauti na CWT wanaokata 2% ya mshahara wako. Hivyo haya ni maajabu pekee yanayotokea huko CWT dhidi ya "haki" inayopatikana CHAKAMWATA.

Pili; ukistaafu kazi, ukisimamishwa kazi au kifo-kwa mwanachama, utarejeshewa nusu ya mchango uliochangia ndani ya chama, tofauti na maajabu yanayofanywa CWT.
KARIBU
Mbona katika maelezo yote haya sijaona ni namna gani kitatetea maslahi ya walimu. Naona kinajitambulisha kwa mikakati ya jinsi ya kupata pesa tu.
 
Back
Top Bottom