Mtikilia adai kutojiunga na mtandao wa "Saidia Kikwete Ashinde"!

Luteni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Messages
2,274
Likes
10
Points
0

Luteni

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2010
2,274 10 0
Na Hapiness Katabazi: Tanzania Daima

MWENYEKITI wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila ambaye ametupwa lupango baada ya kufutiwa dhamana kwa kosa la kushindwa kujiheshimu, amedai hatua hiyo imetokana na msimamo wake wa kukataa kuingizwa kwenye mtandao wa kumsaidia Rais Jakaya Kikwete ashinde.
Tayari hivi sasa kuna madai ya kuwapo kwa baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani ambao wako katika mtandao unaojulikana kama ‘Saidia Jakaya Kikwete Ashinde’.
Baadhi ya viongozi wanaotajwa na ambao siku za hivi karibuni wamekuwa wakitoa kauli za kuwashambulia wanaompinga Rais Kikwete, ni pamoja na Rais wa Chama cha TADEA, Lifa Chipaka, Mwenyekiti wa UPDP, Fahmir Dovutwa na Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema.
Mtikila alitoa madai hayo mazito ya kukataa kuingizwa kwenye mtandao huo wa Rais Kikwete juzi, muda mfupi kabla ya kuwekwa mahabusu kwa kosa la kutojiheshimu na kuruka dhamana.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano kwa njia simu, Mchungaji Mtikila ambaye ana historia ya kukabiliana na kesi za kashfa dhidi ya viongozi wa juu serikalini, alisema Jumatano ya wiki iliyopita, aliitwa na Katibu wa Rais Kikwete, Kassim Mtawa katika Hoteli ya Kempinski ya jijini Dar es Salaam na kuwa na mazungumzo ya faragha.
Mtikila ambaye amepata kuhukumiwa kwenda jela mwaka mmoja kwa kosa la kumkashifu Mwalimu Nyerere, alidai kuwa alipofika hotelini hapo alikutana na Mtawa na kuelezwa kuwa lengo la kikao chao ni kutaka ajiunge kwenye mtandao wa Saidia Kikwete Ashinde katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba.
“Mtawa alinipa majukumu matatu; moja ni la kuitisha mkutano na vyombo vya habari na kutoa kauli ya kuwalaani wote waliomshambulia Rais Kikwete kwenye mdahalo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere, pili alinitaka niitishe mkutano na wanahabari ili niweze kuunga mkono utabiri wa Sheikh Yahya Hussein na tatu, niwachafue wote wanaotaka kujitokeza kumpinga Rais Kikwete ndani ya CCM.
“Mimi nilikataa katakata kufanya kazi hiyo kwani kwangu mimi huo ni udhalimu kwa sababu ninamuogopa Mungu na kuheshimu katiba ya nchi na suala la kugombea nafasi yoyote ni haki ya kila mtu kikatiba,” alisema Mtikila kwa sauti ya upole.
Aliendelea kudai kuwa katika mazungumzo yao, Mtawa alimuahidi kuwa endapo angekubali kufanya mambo hayo matatu, angepewa fedha nyingi za kuendeleza familia yake.
Hata hivyo Mtikila alipoulizwa kama katika mazungumzo hayo hakuchukua kiasi chochote cha fedha, alisema alizikataa kwani alikataa kuingizwa kwenye mtandao huo.
Akizungumzia madai hayo dhidi ya Rais Kikwete kwa njia ya simu, Katibu wa Rais, Mtawa alikanusha na kuyaita ni ya uongo na uzushi wa hali ya juu.
“Jamani huo ni uongo wa hali ya juu. Mimi sijakutana na Mtikila kama anavyodai. Kwanza mimi si niliyemshitaki. Mtu anapofutiwa dhamana maana yake amevunja masharti ya dhamana, ameyakiuka mwenyewe, ndiyo maana mahakama imemfutia dhamana.
“Tena mimi si Msajili wa Mahakama, sasa nashangaa anavyotaka kuniingiza kwenye mambo yasiyo na msingi… Huyo Mtikila ni muungo, tena nashukuru sana umenipa nafasi ya kujieleza,” alisema Mtawa.
Juzi Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, ilimfutia dhamana Mtikila kwa madai ya kushindwa kujiheshimu.
Amri hiyo ya kumfutia dhamana ilitolewa na Hakimu Mkazi Waliarwande Lema baada ya kusikiliza utetezi wa mshitakiwa ambaye alifika katika viwanja vya mahakama hiyo saa tano asubuhi akiwa amechelewa na ghafla alijikuta akikamatwa na askari polisi wa mahakamani hapo.
Kwa mujibu wa habari hizo, Mtikila alipaswa kufika mahakamani hapo majira ya saa tatu asubuhi wakati kesi hiyo ilipotajwa, lakini hakuwepo, ndipo Wakili wa Serikali, Beatrice Mpangala aliomba hati ya kukamatwa kwa mshitakiwa.
Kabla ya Mtikila kukamatwa, aliiambia mahakama kwamba alidamka mapema na kumtafuta daktari wake aliyemtaja kwa jina moja la Katembo, ambaye alimfanyia upasuaji baada ya kugongwa na nyoka aina ya kobra wakati alipokuwa katika shughuli za kidini nchini Zimbabwe mwaka jana.
Alisema alijitahidi kuwatafuta wadhamini wake ili wafike mahakamani kwa niaba yake, lakini hakuweza kuwapata, ndiyo maana alikuja mwenyewe mahakamani hapo akiwa na maumivu makali mwilini mwake.
Hata hivyo hakimu Lema alieleza kutoridhishwa na utetezi huo na kuamuru Mtikila atupwe rumande hadi Januari 25 kesi yake itakapotajwa tena.
Hii ni mara ya pili kwa Mchungaji Mtikila kushindwa kufika mahakamani wala wadhamini wake. Mara ya kwanza ilikuwa Oktoba 22, mwaka jana.
Mchungaji Mtikila anakabiliwa na kesi ya uchochezi namba 1767/2007. Ilidaiwa kuwa alitoa maneno ya uchochezi na kashfa dhidi ya Rais Kikwete kwa kumuita gaidi kwa madai kuwa serikali anayoiongoza inataka kuanzisha Mahakama ya Kadhi, jambo ambalo ni kinyume na katiba ya nchi.

Source: Tanzania Daima
 
Facts1

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2009
Messages
308
Likes
5
Points
0

Facts1

JF-Expert Member
Joined Dec 23, 2009
308 5 0
Tayari hivi sasa kuna madai ya kuwapo kwa baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani ambao wako katika mtandao unaojulikana kama ‘Saidia Jakaya Kikwete Ashinde'.
Baadhi ya viongozi wanaotajwa na ambao siku za hivi karibuni wamekuwa wakitoa kauli za kuwashambulia wanaompinga Rais Kikwete, ni pamoja na Rais wa Chama cha TADEA, Lifa Chipaka, Mwenyekiti wa UPDP, Fahmir Dovutwa na Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema.
Ni jana tu nilisema huku kukamatwa kwa Mtikila isije kuwa mbinu yake ya kutaka asikike sasa tumeanza kuona tusiyoyajua. Wanasiasa si wakuamini inawezekana sisi tunajua kafutiwa dhamana na sheria inachukua mkondo wake lakini inawezekana vile vile ilikuwa planed aidha na Mtikila au na serikali au kuna dili limeshindikana, jana alipotoa zile sababu za kutokwenda mahakamani na za wakili wake nilisema moja kwa moja si sababu za msingi na Mtikila anajua kabisa si sabau za msingi, sidhani hadi leo hii bado yuko mahabusu.

Huu mtandao inawezekana kweli upo maana kauli zinazotolewa siku hizi huwezi amini kama ni kauli za viongozi wa upinzani.
 
alibaba

Senior Member
Joined
Jun 24, 2009
Messages
185
Likes
3
Points
0

alibaba

Senior Member
Joined Jun 24, 2009
185 3 0
"Angepewa fedha nyingi za kuendeleza familia yake" Hiyo ni kauli ya Mh Mtikila, mbona inaonekana kama uongo wa kizamani. Watu wazima wawili mkae kikao kizito na upewe ahadi dhaifu kamahiyo? Kwa nini asitajiwe kima cha pesa? na kwa nini alishiwe kuwa pesa hizo zitaendeleza familia yake? Hapa kuna walakini................. .
 
Kiby

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2009
Messages
5,451
Likes
1,258
Points
280

Kiby

JF-Expert Member
Joined Nov 16, 2009
5,451 1,258 280
Enhe kama mambo ndio hayo basi Africa kiupeo haitofautiani sana na mnyama nyani na ndio maana wenzetu weupe wametukadiria daraja la chini. Rais aliyepo madarakani anaogopa nini hata kuanza kuwanunua wapinzani wamsaidie ktk kampeni? Ni kweli Jk anaogopa kushindwa uchaguzi au anaogopa kupunguza kiwango cha ushindi kutoka asilimia 80?. Tz kuna kiini macho tu hakuna uchaguzi, na kama Wtz hawatafanya jitihada za kubadili katiba kwanza kabla ya uchaguzi kura za ballot hazitakaa zimlete kiongozi. Fikiri rais ana wateule wake kama wakuu wa mikoa na wa wilaya na tume ya uchaguzi ni yake sasa serikali inapokuwa imeondoka kupisha uchaguzi sii kweli kwamba imeondoka bali robo ya serikali ndio imeondoka na hivyo hii robo tatu inabaki madarakani kwa kazi moja nayo ni kuwarejeza walioondoka ikiwa ni pamoja na aliyewapa huo ulaji yaani rais. Kwa habari ya mtikila kama ni kweli basi atakuwa anaogopa maana ana kumbukumbu ya kilichompata kule kwa Wangwe aliponunuliwa na ccm kwa staili hiyo hiyo.
 
Jasusi

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2006
Messages
11,492
Likes
209
Points
160

Jasusi

JF-Expert Member
Joined May 5, 2006
11,492 209 160
The details are coming out slowly. Ikulu badala ya kujibu hoja zilizotolewa kwenye Kongamano na MNF wakamtumia Sheikh Yahya, halafu Mrema, and I do not know who is going to be next. Kwa hiyo kuna mkakati wa Saidia Kikwete Ashinde. Kufika Oktoba tutakuwa tumeyaona mengi kweli.
 
Kiranga

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Messages
39,849
Likes
12,504
Points
280

Kiranga

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2009
39,849 12,504 280
Kikwete is so insecure, hii nchi anaichukua, labda ajikojolee kwenye mimbari.

Sasa hizi rafu za rushwa kama anagombea tena 2005 (this time hagombei, anapitishwa tu) ndizo zitakazomu expose na kumfanya aonekane how insecure he is.

I mean this time ana vyombo vyote vya serikali, na tume ya uchaguzi, anaweza hata kushindwa na kugeuza matokeo bila shida, ana taabu gani ya kuanza kuhonga na machinations zote hizi?

Some people are just insecure no matter what.
 
Joined
Jul 21, 2009
Messages
72
Likes
0
Points
0

Kibori

Member
Joined Jul 21, 2009
72 0 0
Na Hapiness Katabazi: Tanzania Daima

“Jamani huo ni uongo wa hali ya juu. Mimi sijakutana na Mtikila kama anavyodai. Kwanza mimi si niliyemshitaki. Mtu anapofutiwa dhamana maana yake amevunja masharti ya dhamana, ameyakiuka mwenyewe, ndiyo maana mahakama imemfutia dhamana.
“Tena mimi si Msajili wa Mahakama, sasa nashangaa anavyotaka kuniingiza kwenye mambo yasiyo na msingi… Huyo Mtikila ni muungo, tena nashukuru sana umenipa nafasi ya kujieleza,” alisema Mtawa.

IT IS TOUGH TO BE BLACK ! TANGU LINI KATIBU WA RAIS AMEKUWA MZUNGUMZAJI WA MAHAKAMA ...... KWANZA he is contradicting himself anasema MTIKILA amevunja masharti ya Dhamana AMEJUAJE ? Kwani yeye aliona wapi file la Mtikila na kuona masharti aliyopewa MTIKILA !!!

Huwezi kusoma kwenye magazeti na kusema hivyo !

Yet he goes on kusema kawa niaba ya Mahakama kwamba Mtikila amevunja masharti as if yeye ni mmoja ama aliyetoa maagizo au ni spokesperson wa Mahakama ! Kuna WALAKINI !

Juzi Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, ilimfutia dhamana Mtikila kwa madai ya kushindwa kujiheshimu.
Amri hiyo ya kumfutia dhamana ilitolewa na Hakimu Mkazi Waliarwande Lema baada ya kusikiliza utetezi wa mshitakiwa ambaye alifika katika viwanja vya mahakama hiyo saa tano asubuhi akiwa amechelewa na ghafla alijikuta akikamatwa na askari polisi wa mahakamani hapo.

IT IS SEEMS KAMA VILE HII MOVE ILIANDALIWA KWANINI ASKARI NDIO WAMPOKEE BILA MAHAKAMA KUSIKILIZA SABABU ZILIZOMFANYA MTIKILA ACHALEWE ....

HII NAONA ILISHAPANGWA !!! KAWAIDA MTU MWENYWE DHAMANA ANAHAKI YA KUSIKILIZA NA SABABU YAKE KAMA NILIVYOSOMA, IS VALID LABDA KAMA ANGESHINDWA KUIAMINISHA MAHAKAMA KWAMBA ALIKUWA NA TATIZO HILO ANALOLISEMA AMEPATA HUKO ZIMBABWE !

Kwa mujibu wa habari hizo, Mtikila alipaswa kufika mahakamani hapo majira ya saa tatu asubuhi wakati kesi hiyo ilipotajwa, lakini hakuwepo, ndipo Wakili wa Serikali, Beatrice Mpangala aliomba hati ya kukamatwa kwa mshitakiwa.

KWANI MTIKILA HAKUWA NA WAKILI WAKE ? ALIKUWA WAPI ? KWANINI WAKILI WA SERIKALI ATOKE OMBI LA KUFUTIWA DHAMANA HARAKA HARAKA NA OMBI KUKUBALIWA HARAKA HIVYO .... SOMETHING IS FISHY HERE !

Kabla ya Mtikila kukamatwa, aliiambia mahakama kwamba alidamka mapema na kumtafuta daktari wake aliyemtaja kwa jina moja la Katembo, ambaye alimfanyia upasuaji baada ya kugongwa na nyoka aina ya kobra wakati alipokuwa katika shughuli za kidini nchini Zimbabwe mwaka jana.
Alisema alijitahidi kuwatafuta wadhamini wake ili wafike mahakamani kwa niaba yake, lakini hakuweza kuwapata, ndiyo maana alikuja mwenyewe mahakamani hapo akiwa na maumivu makali mwilini mwake.

THIS IS A VERY REASONABLE ARGUMENT MAHAKAMA ILITAKIWA KUMPA NAFASI ADHIBITISHE HILO SIO SIKU HIYO HIYO KAMA MASHAHIDI HAWAKUPO ANGEDHIBITISHAJE ?

Hata hivyo hakimu Lema alieleza kutoridhishwa na utetezi huo na kuamuru Mtikila atupwe rumande hadi Januari 25 kesi yake itakapotajwa tena.

KAMA VILE KUNA ORDER TOKA JUU !!

Source: Tanzania Daima
SIKU HIZI IT IS SAD TO SAY MAHAKAMA ZETU HAZITENDI HAKI, KAMA ZINATENDA HAKI BASI HAKI HAIWONEKANI IKITENDEKA "

JUSTICE MUST NOT ONLY BE DONE BUT SHALL MANIFESTLY AND UNDOUBTEDLY SEEN TO BE DONE

ALICHOFANYIWA REV. MTIKILA SIO KABILA. Katika Nchi huru na yenye Amani , watu kama wakina Mtikila are BOUND to exist ! To Eliminate them ni Kukiuka The Law of Nature !

MUST WE REACT TO EVERYTHING SAID OR DONE TO THE PRESIDENT ? I AM NECESSARILY TAKING ABOUT LAW .

Politicians-Leaders drives power from the PEOPLE sasa wote wapelekwa Gerezani watatoa wapi HAYO MAMLAKA .

President BUSH mstaafu ( JUNIOR) wa USA, once was asked a question of what he feels of US citizen's JOKES about him ! He said in country where citizens are free to joke about their political leaders or Official Leaders, it means there is a little GAP between leaders and the citizens but it also means THERE IS STRONG RESPECT TO DEMOCRACY !!!

Sisi wa kwetu ni opposite, hata wakati hujasema kitu .... chochote you are implicated forget about when you said something little !

Kazi IPO !!!!!
 
Che Kalizozele

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2008
Messages
778
Likes
7
Points
0

Che Kalizozele

JF-Expert Member
Joined Jul 20, 2008
778 7 0
ADAIWA KUMTAKA MTIKILA KWENYE MTANDAO WAKE

na Happiness Katabazi
MWENYEKITI wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila ambaye ametupwa lupango baada ya kufutiwa dhamana kwa kosa la kushindwa kujiheshimu, amedai hatua hiyo imetokana na msimamo wake wa kukataa kuingizwa kwenye mtandao wa kumsaidia Rais Jakaya Kikwete ashinde.

Tayari hivi sasa kuna madai ya kuwapo kwa baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani ambao wako katika mtandao unaojulikana kama ‘Saidia Jakaya Kikwete Ashinde’.

Baadhi ya viongozi wanaotajwa na ambao siku za hivi karibuni wamekuwa wakitoa kauli za kuwashambulia wanaompinga Rais Kikwete, ni pamoja na Rais wa Chama cha TADEA, Lifa Chipaka, Mwenyekiti wa UPDP, Fahmir Dovutwa na Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema.

Mtikila alitoa madai hayo mazito ya kukataa kuingizwa kwenye mtandao huo wa Rais Kikwete juzi, muda mfupi kabla ya kuwekwa mahabusu kwa kosa la kutojiheshimu na kuruka dhamana.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano kwa njia simu, Mchungaji Mtikila ambaye ana historia ya kukabiliana na kesi za kashfa dhidi ya viongozi wa juu serikalini, alisema Jumatano ya wiki iliyopita, aliitwa na Katibu wa Rais Kikwete, Kassim Mtawa katika Hoteli ya Kempinski ya jijini Dar es Salaam na kuwa na mazungumzo ya faragha.

Mtikila ambaye amepata kuhukumiwa kwenda jela mwaka mmoja kwa kosa la kumkashifu Mwalimu Nyerere, alidai kuwa alipofika hotelini hapo alikutana na Mtawa na kuelezwa kuwa lengo la kikao chao ni kutaka ajiunge kwenye mtandao wa Saidia Kikwete Ashinde katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba.

“Mtawa alinipa majukumu matatu; moja ni la kuitisha mkutano na vyombo vya habari na kutoa kauli ya kuwalaani wote waliomshambulia Rais Kikwete kwenye mdahalo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere, pili alinitaka niitishe mkutano na wanahabari ili niweze kuunga mkono utabiri wa Sheikh Yahya Hussein na tatu, niwachafue wote wanaotaka kujitokeza kumpinga Rais Kikwete ndani ya CCM.

“Mimi nilikataa katakata kufanya kazi hiyo kwani kwangu mimi huo ni udhalimu kwa sababu ninamuogopa Mungu na kuheshimu katiba ya nchi na suala la kugombea nafasi yoyote ni haki ya kila mtu kikatiba,” alisema Mtikila kwa sauti ya upole.

Aliendelea kudai kuwa katika mazungumzo yao, Mtawa alimuahidi kuwa endapo angekubali kufanya mambo hayo matatu, angepewa fedha nyingi za kuendeleza familia yake.

Hata hivyo Mtikila alipoulizwa kama katika mazungumzo hayo hakuchukua kiasi chochote cha fedha, alisema alizikataa kwani alikataa kuingizwa kwenye mtandao huo.

Akizungumzia madai hayo dhidi ya Rais Kikwete kwa njia ya simu, Katibu wa Rais, Mtawa alikanusha na kuyaita ni ya uongo na uzushi wa hali ya juu.

“Jamani huo ni uongo wa hali ya juu. Mimi sijakutana na Mtikila kama anavyodai. Kwanza mimi si niliyemshitaki. Mtu anapofutiwa dhamana maana yake amevunja masharti ya dhamana, ameyakiuka mwenyewe, ndiyo maana mahakama imemfutia dhamana.

“Tena mimi si Msajili wa Mahakama, sasa nashangaa anavyotaka kuniingiza kwenye mambo yasiyo na msingi… Huyo Mtikila ni muungo, tena nashukuru sana umenipa nafasi ya kujieleza,” alisema Mtawa.

Juzi Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, ilimfutia dhamana Mtikila kwa madai ya kushindwa kujiheshimu.

Amri hiyo ya kumfutia dhamana ilitolewa na Hakimu Mkazi Waliarwande Lema baada ya kusikiliza utetezi wa mshitakiwa ambaye alifika katika viwanja vya mahakama hiyo saa tano asubuhi akiwa amechelewa na ghafla alijikuta akikamatwa na askari polisi wa mahakamani hapo.

Kwa mujibu wa habari hizo, Mtikila alipaswa kufika mahakamani hapo majira ya saa tatu asubuhi wakati kesi hiyo ilipotajwa, lakini hakuwepo, ndipo Wakili wa Serikali, Beatrice Mpangala aliomba hati ya kukamatwa kwa mshitakiwa.

Kabla ya Mtikila kukamatwa, aliiambia mahakama kwamba alidamka mapema na kumtafuta daktari wake aliyemtaja kwa jina moja la Katembo, ambaye alimfanyia upasuaji baada ya kugongwa na nyoka aina ya kobra wakati alipokuwa katika shughuli za kidini nchini Zimbabwe mwaka jana.

Alisema alijitahidi kuwatafuta wadhamini wake ili wafike mahakamani kwa niaba yake, lakini hakuweza kuwapata, ndiyo maana alikuja mwenyewe mahakamani hapo akiwa na maumivu makali mwilini mwake.

Hata hivyo hakimu Lema alieleza kutoridhishwa na utetezi huo na kuamuru Mtikila atupwe rumande hadi Januari 25 kesi yake itakapotajwa tena.

Hii ni mara ya pili kwa Mchungaji Mtikila kushindwa kufika mahakamani wala wadhamini wake. Mara ya kwanza ilikuwa Oktoba 22, mwaka jana.

Mchungaji Mtikila anakabiliwa na kesi ya uchochezi namba 1767/2007.

Ilidaiwa kuwa alitoa maneno ya uchochezi na kashfa dhidi ya Rais Kikwete kwa kumuita gaidi kwa madai kuwa serikali anayoiongoza inataka kuanzisha Mahakama ya Kadhi, jambo ambalo ni kinyume na katiba ya nchi.
 
Hofstede

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2007
Messages
3,584
Likes
40
Points
0

Hofstede

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2007
3,584 40 0
Mtikila kazi yake ni kuongea bila woga ni mojawapo ya shughuli zinazomuweka. Japo mnamwita kichaa ila huyu jamaa anatumiwa sana kwa issue sensitive kuzianika. Umuhimu wa huyu ni kuvuruga. Mimi ninaamini kabisa kuwa katibu wa rais alijaribu kumpa dili alilosema Mtikila naye akalikataa. Ila ingekuwa vizuri kama mtikila angekuwa na kinasa sauti aweke hadharani. Vinginevyo itaishia kuwa stori ya "kamtongoza mke wangu" ila kwa kuwa hukuwepo utaishia kulalama
 
nguvumali

JF Bronze Member
Joined
Sep 3, 2009
Messages
4,891
Likes
182
Points
160

nguvumali

JF Bronze Member
Joined Sep 3, 2009
4,891 182 160
Mtikila, your so wonderful, hukosi vijineno, hukosi mikasa, wewe ni mwanasiasa wakipekee, najua ukirudi uraiani utaitisha mkutano na waandishi wa habari kufafanua hayo, pole mkuu, wewe ni mwanasiasa wa kwanza wa upinzani niliekua nakuzimia miak ya 90, ila sikuhizi unaniboa.
 
Forum statistics

Threads 1,191,647
Members 451,726
Posts 27,716,446