BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,082
Waungwana kama kuna yeyote mwenye more info kuhusu kamati hii au kama akipata hizo info siku za usoni azimwage hapa ukumbini.
Alutta Continua
Date::7/8/2008
Mtikila, wenzake kufungua kesi dhidi ya mafisadi
Na Kizitto Noya na James Magai
Mwananchi
KAMATI ya Kupambana na Uporaji wa Nchi (PILCOM) imesema hairidhishwi na kitendo cha baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi, kutumia makanisa kujisafisha.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo na kiongozi wa Kanisa la Full Salvation, Christopher Mtikila, alidai jana katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam kwamba, ni ukiukwaji wa haki na misingi ya sheria za nchi, kwa wezi wa kuku na vibaka kufungwa gerezani na mafisadi wa fedha za umma kuachwa huru.
Alidai kuwa kamati hiyo inakusudia kufungua kesi mahakamani dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
''Moja ya kazi za kamati hii ni kuwafikisha mbele ya sheria watu wote walioshiriki katika wizi wa matrilioni ya fedha za nchi yetu katika Benki Kuu na kurejesha mapesa yote waliyoyaiba pamoja na riba na gharama kutoka kila walikoyaweka nje na ndani ya nchi,'' alisema Mchungaji Mtikila.
Alisema katika maandalizi ya kufungua kesi hiyo, jana kamati ilimwandikia barua Jaji Mkuu na Jaji Kiongozi kuwataka waharakishe hukumu ya kesi ya Katiba namba 86/2006, iliyofunguliwa na kamati hiyo kuitaka iruhusu watu binafsi kuendesha kesi za jinai.
Alisema hivi sasa kamati hiyo inangoja hukumu ya kesi hiyo, ili iweze kufungua kesi dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi.
Alidai kuwa wamemwandikia Gavana wa BoT na Spika wa Bunge waipatie taarifa muhimu za wizi huo, ili sheria ichukue mkondo wake.
''Tunawahakikishia wananchi kwamba, kama inavyosema Katiba ya Jamhuri ya Muungano, hakuna mwizi aliye juu ya sheria, awe rais mstaafu au aliye madarakani, waziri, kigogo wa CCM au gabacholi jeupe au jeusi, mradi ameshiriki katika wizi wa mali za umma lazima atafikishwa mahakamani,'' alisema Mtikila
Kwa mujibu wa Mtikila, Kamati hiyoambayo inawahusisha viongozi wa makisa kadhaa, inashughulikia wizi wa Sh216 kutoka Mfuko wa Import Support, mabilioni ya EPA, DCP na OGL, ufisadi katika mkataba wa Richmond na Dowans, Meremeta na Tangold, IPTL, Songas, Aggreko, Netgroup Solutions, TICTS, Radar, TTCL, Benki ya Taifa ya Biashara,Tanzanite, migodi ya dhahabu na uporaji wa majumba ya serikali na vigogo wa CCM.
Kamati pia ilimtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kushiriki kikamilifu katika vita hiyo ya ufisadi na kuhakikisha kuwa wahusika wote umma wanazirejesha na kufikishwa mahakamani.
Akizungumza katika mkutano huo, Askofu Gordon Kiaro wa kanisa la Pentecostal Fellowship (INT) alisema suala la kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa ufisadi sio la kidini wala dhehebu na kwamba, linapaswa kuungwa mkono na Watanzania wote.