Elections 2010 Mtikila: Viongozi wa dini wanafiki

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233

Mtikila: Viongozi wa dini wanafiki

na Andrew Chale

MWENYEKITI wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, ameponda hatua ya ujumbe wa viongozi wa dini nchini kumtaka Dk. Willibrod Slaa, kukubali matokeo ya kushindwa kwenye uchaguzi wa rais uliomalizika hivi karibini na kuwafananisha na Yuda Eskalioti, aliyepewa vipande 30 vya fedha kisha kumsaliti Yesu.

Mtikila aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati akiongea na Tanzania Daima, akidai kuwa, kitendo hicho ni cha kinafki, kwani viongozi hao hawakupaswa kumfuata Dk. Slaa na ujumbe wao huo wa kumtaka akubali matokeo ili kulinusuru taifa na machafuko ya kisiasa.

Badala yake aliwataka viongozi hao wangeanza kwenda Tume ya Taifa ya Uchaguzi pamoja na Rais Kikwete ili kuona hatua ya kufuata ili kuzuia mpasuko uliopo sasa nchini.

“Tume imekubali kuwa kulikuwa na makosa mbalimbali kwenye uchaguzi na watayafanyia kazi ili yasitokee tena, vivyo hivyo walitakiwa kumfuata na Rais Kikwete ili kumuona angesemaje juu ya hatua hiyo ya Dk. Slaa, lakini kwa kitendo cha kwenda kwa Dk. Slaa sasa ni cha kinafki na ndio wanaoifanya dini kama mradi wa kuficha maovu,” alisema Mtikila.

Akinukuu vifungu vya Biblia, kikiwamo cha Tito 2:11, Waraka wa pili wa Timotheo 4:2, ambavyo vyote vinalaani na kukemea machafuko na dhuluma kwa wanadamu, Mtikila alisema kuwa viongozi wa dini wameafiki hali ya uchakachuaji uliofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kuiba kura za wananchi na kudhani ni za Dk. Slaa.

“Kilichotakiwa kufanywa na viongozi hawa wa dini kama wanaona kuna machafuko, walitakiwa wagome kwa pamoja hatua ya kuapishwa kwa rais na kudai maridhiano ya pamoja. Lakini wao waliafiki moja kwa moja kwa kukubali kupewa vipande 30 vya fedha kama Yuda na kisha kumsaliti Yesu,” alisema Mtikila.

Aidha, Mtikila alikubaliana na hatua hiyo ya Dk. Slaa kuyakataa matokeo hayo yaliyochakachuliwa, kwani ni kitendo cha dhahiri, anasimamia masilahi ya taifa ambalo lilimchagua ili awakomboe.

“Kura zilizoibwa na CCM ni za wananchi wote wa Tanzania wanaopenda mageuzi ya kweli, waliochoka na manyanyaso na masuala ya ufisadi, ijulikane hawakumuibia Dk. Slaa ambaye kura yake ni moja tu,” alimalizia Mtikila.

Alisema kuwa kama ingekuwa ni wahuni tu wanamfuata Dk. Slaa na kumtaka akubali matokeo, tungesema wameshalewa madawa, lakini viongozi wa dini ambao ni taswira kwenye taifa ni jambo la kushangaza, halitavumiliwa kamwe na lisifumbiwe macho,” alisema Mtikila.

Pia aliweza kutolea mfano juu ya nchi mbalimbali ambazo viongozi wa dini waliamua kupambana waziwazi ili kulinda hali ya amani, ikiwemo kutoa ushawishi mkubwa wa kupatikana haki ya msingi, ambapo ushawishi wao ulisaidia kufanikisha baadhi ya mambo.

Mtikila alizitaja nchi hizo kuwa ni pamoja na maaskofu wa nchi ya Afrika Kusini, waliokuwa upande wa watu walioonewa wa vyama vya ANC na PNC, kwa Malawi viongozi wa dini 16 waliamua kwa pamoja kumpinga Rais Banda.

Hivyo hivyo ilifanyika katika nchi za Ukraine, Thailand na Kenya, ambao walikuwa na machafuko makubwa.

Chanzo: Tanzania Daima

My take -

Pamoja na kwamba mara nyingi huwa sichukulii maanani sana kauli za mchungaji huyu, lakini kwa hii kagonga kweli kweli.

Hakika baadhi ya viongozi wa dini ni wanafiki tu na wanatumiwa na chama tawala kuvuruga, na mara nyingine eti kuwapoza wapinzani.

Kama ni kweli kwa maamuzi/utashi wao wenyewe ndiyo uliwasukuma kwenda kumwona Dr Slaa kumbembeleza akubali matokeo, kwa nini wasiende pia kwa JK kumueleza kwamba Tume yake (NEC) iliiba sana kura za wapinzani. Hapo ndiyo tungejua viongozi hao wa dini wako neutral!

Big up, Mchungaji. Nakugongea 100% -- ni wanafiki tu hawa wakuu wa dini.
 
Soma 1samweli 8: 1 - mwisho. utaona walichoenda kuomba kwa slaa hasa ukizingatia kuwa slaa ni chaguo la wengi hivyo ni chaguo la Mungu
 
Mi sielewi unamshauri mtu akubali matokeo kivipi, wakati yana njia yake asilia ya kujionyesha kama ni ya kweli ama la!...Kwanini ushawishi na si natural justice?
 
na katika Genge hilo la WACHUNGAJI NA VIONGOZI WA DINI linaongozwa na vibaraka msheli wa ccm , na yupo mwingine anaitwa Gamanywa wa WAPO MISSION, huyu ndio hana hata haya, alimwita na shehe wake mmoja wa pale Mnyamani kisa kuonya udini na kusihi watu wakubali matokeo, Mtikila Yuko sahihi,
 
Asante Rev.mtikila kwa kuwa mkweli tusaidie kueneza elimu ya uraia kwa raia wetu waliobaki ambao hawajui haki na wajibu wao ktk Taifa
 
Kwa kweli kwa hilo umenena mchungaji Mtikila! Viongozi hao wa dini ni wanafiki, wazabizabina, wazandiki na wazushi tu! Wangeeleweka tu kama wangeanza na JK pamoja na NEC yake! Wana masilahi binafsi hawa hawana lolote zaidi ya kujidhalilisha kwa kushabikia kudhulumu haki za watanzania!!!
 
Mtikila: Viongozi wa dini wanafiki

na Andrew Chale

MWENYEKITI wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, ameponda hatua ya ujumbe wa viongozi wa dini nchini kumtaka Dk. Willibrod Slaa, kukubali matokeo ya kushindwa kwenye uchaguzi wa rais uliomalizika hivi karibini na kuwafananisha na Yuda Eskalioti, aliyepewa vipande 30 vya fedha kisha kumsaliti Yesu.

Mtikila aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati akiongea na Tanzania Daima, akidai kuwa, kitendo hicho ni cha kinafki, kwani viongozi hao hawakupaswa kumfuata Dk. Slaa na ujumbe wao huo wa kumtaka akubali matokeo ili kulinusuru taifa na machafuko ya kisiasa.

Badala yake aliwataka viongozi hao wangeanza kwenda Tume ya Taifa ya Uchaguzi pamoja na Rais Kikwete ili kuona hatua ya kufuata ili kuzuia mpasuko uliopo sasa nchini.

“Tume imekubali kuwa kulikuwa na makosa mbalimbali kwenye uchaguzi na watayafanyia kazi ili yasitokee tena, vivyo hivyo walitakiwa kumfuata na Rais Kikwete ili kumuona angesemaje juu ya hatua hiyo ya Dk. Slaa, lakini kwa kitendo cha kwenda kwa Dk. Slaa sasa ni cha kinafki na ndio wanaoifanya dini kama mradi wa kuficha maovu,” alisema Mtikila.

Akinukuu vifungu vya Biblia, kikiwamo cha Tito 2:11, Waraka wa pili wa Timotheo 4:2, ambavyo vyote vinalaani na kukemea machafuko na dhuluma kwa wanadamu, Mtikila alisema kuwa viongozi wa dini wameafiki hali ya uchakachuaji uliofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kuiba kura za wananchi na kudhani ni za Dk. Slaa.

“Kilichotakiwa kufanywa na viongozi hawa wa dini kama wanaona kuna machafuko, walitakiwa wagome kwa pamoja hatua ya kuapishwa kwa rais na kudai maridhiano ya pamoja. Lakini wao waliafiki moja kwa moja kwa kukubali kupewa vipande 30 vya fedha kama Yuda na kisha kumsaliti Yesu,” alisema Mtikila.

Aidha, Mtikila alikubaliana na hatua hiyo ya Dk. Slaa kuyakataa matokeo hayo yaliyochakachuliwa, kwani ni kitendo cha dhahiri, anasimamia masilahi ya taifa ambalo lilimchagua ili awakomboe.

“Kura zilizoibwa na CCM ni za wananchi wote wa Tanzania wanaopenda mageuzi ya kweli, waliochoka na manyanyaso na masuala ya ufisadi, ijulikane hawakumuibia Dk. Slaa ambaye kura yake ni moja tu,” alimalizia Mtikila.

Alisema kuwa kama ingekuwa ni wahuni tu wanamfuata Dk. Slaa na kumtaka akubali matokeo, tungesema wameshalewa madawa, lakini viongozi wa dini ambao ni taswira kwenye taifa ni jambo la kushangaza, halitavumiliwa kamwe na lisifumbiwe macho,” alisema Mtikila.

Pia aliweza kutolea mfano juu ya nchi mbalimbali ambazo viongozi wa dini waliamua kupambana waziwazi ili kulinda hali ya amani, ikiwemo kutoa ushawishi mkubwa wa kupatikana haki ya msingi, ambapo ushawishi wao ulisaidia kufanikisha baadhi ya mambo.

Mtikila alizitaja nchi hizo kuwa ni pamoja na maaskofu wa nchi ya Afrika Kusini, waliokuwa upande wa watu walioonewa wa vyama vya ANC na PNC, kwa Malawi viongozi wa dini 16 waliamua kwa pamoja kumpinga Rais Banda.

Hivyo hivyo ilifanyika katika nchi za Ukraine, Thailand na Kenya, ambao walikuwa na machafuko makubwa.

Chanzo: Tanzania Daima

My take -

Pamoja na kwamba mara nyingi huwa sichukulii maanani sana kauli za mchungaji huyu, lakini kwa hii kagonga kweli kweli.

Hakika baadhi ya viongozi wa dini ni wanafiki tu na wanatumiwa na chama tawala kuvuruga, na mara nyingine eti kuwapoza wapinzani.

Kama ni kweli kwa maamuzi/utashi wao wenyewe ndiyo uliwasukuma kwenda kumwona Dr Slaa kumbembeleza akubali matokeo, kwa nini wasiende pia kwa JK kumueleza kwamba Tume yake (NEC) iliiba sana kura za wapinzani. Hapo ndiyo tungejua viongozi hao wa dini wako neutral!

Mkuu, usimpuuze hata kidogo huyu mchungaji,siku ukikaa na kutafakari utajua kile anachokipigania.
 
Hapa Mtikila kagonga. Wacha waseme lakini ujumbe wameupata. Walau Kakobe aliendesha elimu ya uraia na haki ya kupiga kura.
 
Kuna viongozi wa dini ambao nao ni mafisadi pia. Unawezaje kuungana na kundi la mbwa mwitu kukandamiza kondoo? Huu nao ni ufisadi, Ngoja kupitia nguvu ya watu tuuangushe ubeberu wa ccm na BAADA ya hapo tuingie kwenye Makanisa na Misikiti kuwapa elimu ya kuwa majasiri wa haki na si na wao kukumbatia tena maasi. Waache nidhamu za uwoga na njaa pia
 
kwani ni viongozi wa dini gani waliokwenda kumshawishi Dr. Slaa akubali matokeo? mimi siamini! kwani ni wale walioambiwa wasichanganye dini na siasa? au mambo yakiaribika wanatafutwa? ni wa dini gani hao tafadhali? watakuwa na akili kweli?
 
Mchungaji mtilkila anatukumbusha viongozi wadini wa kenya walimtolea uvivu Mwai Kibaki na kuamsha hamasa kwa wananchi ya kutaka mabadiliko.JK ametumia sana kichaka cha udini akiwatuhumu maaskofu kuwa wanahusika na pia JK aliweza kwenda mbali zaidi kwa kukumbusha kuwa kuna Makasisi wa kikatoliki walishiriki kuamsha mauji Rwanda kitendo hicho kiliwafanya maaskofu wa Kikatoliki Tanzania kurudi nyuma badala ya kuendela kueleza ukweli kwani yaliyotokea Rwanda yana mazingira tofauti na hapa iweje wamuache JK aibe kura bila kukemewa.Inauma viongozi wetu wa DINI CHANGAMKENI NCHI INAKWENDA AMANI MNAYOISEMA IKO REHANI.SUBIRINI MTASHANGAA
 
Ninavyoelewa wachungaji na maaskofu wakiona kuwa mtu ametenda dhambi ya uwizi wanamtubisha au kumtenga,siyo wanaenda kwake aliyeibiwa na kujaribu kumtuliza. Nauliza swali kwa hao maaskofu je mwizi anapaswa kufanyiwa nini kama aliyeibiwa ataambiwa akubaliane na uwizi aliyofanyiwa??????????
 
Mtikila: Viongozi wa dini wanafiki

na Andrew Chale

MWENYEKITI wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, ameponda hatua ya ujumbe wa viongozi wa dini nchini kumtaka Dk. Willibrod Slaa, kukubali matokeo ya kushindwa kwenye uchaguzi wa rais uliomalizika hivi karibini na kuwafananisha na Yuda Eskalioti, aliyepewa vipande 30 vya fedha kisha kumsaliti Yesu.

Mtikila aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati akiongea na Tanzania Daima, akidai kuwa, kitendo hicho ni cha kinafki, kwani viongozi hao hawakupaswa kumfuata Dk. Slaa na ujumbe wao huo wa kumtaka akubali matokeo ili kulinusuru taifa na machafuko ya kisiasa.

Badala yake aliwataka viongozi hao wangeanza kwenda Tume ya Taifa ya Uchaguzi pamoja na Rais Kikwete ili kuona hatua ya kufuata ili kuzuia mpasuko uliopo sasa nchini.

"Tume imekubali kuwa kulikuwa na makosa mbalimbali kwenye uchaguzi na watayafanyia kazi ili yasitokee tena, vivyo hivyo walitakiwa kumfuata na Rais Kikwete ili kumuona angesemaje juu ya hatua hiyo ya Dk. Slaa, lakini kwa kitendo cha kwenda kwa Dk. Slaa sasa ni cha kinafki na ndio wanaoifanya dini kama mradi wa kuficha maovu," alisema Mtikila.

Akinukuu vifungu vya Biblia, kikiwamo cha Tito 2:11, Waraka wa pili wa Timotheo 4:2, ambavyo vyote vinalaani na kukemea machafuko na dhuluma kwa wanadamu, Mtikila alisema kuwa viongozi wa dini wameafiki hali ya uchakachuaji uliofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kuiba kura za wananchi na kudhani ni za Dk. Slaa.

"Kilichotakiwa kufanywa na viongozi hawa wa dini kama wanaona kuna machafuko, walitakiwa wagome kwa pamoja hatua ya kuapishwa kwa rais na kudai maridhiano ya pamoja. Lakini wao waliafiki moja kwa moja kwa kukubali kupewa vipande 30 vya fedha kama Yuda na kisha kumsaliti Yesu," alisema Mtikila.

Aidha, Mtikila alikubaliana na hatua hiyo ya Dk. Slaa kuyakataa matokeo hayo yaliyochakachuliwa, kwani ni kitendo cha dhahiri, anasimamia masilahi ya taifa ambalo lilimchagua ili awakomboe.

"Kura zilizoibwa na CCM ni za wananchi wote wa Tanzania wanaopenda mageuzi ya kweli, waliochoka na manyanyaso na masuala ya ufisadi, ijulikane hawakumuibia Dk. Slaa ambaye kura yake ni moja tu," alimalizia Mtikila.

Alisema kuwa kama ingekuwa ni wahuni tu wanamfuata Dk. Slaa na kumtaka akubali matokeo, tungesema wameshalewa madawa, lakini viongozi wa dini ambao ni taswira kwenye taifa ni jambo la kushangaza, halitavumiliwa kamwe na lisifumbiwe macho," alisema Mtikila.

Pia aliweza kutolea mfano juu ya nchi mbalimbali ambazo viongozi wa dini waliamua kupambana waziwazi ili kulinda hali ya amani, ikiwemo kutoa ushawishi mkubwa wa kupatikana haki ya msingi, ambapo ushawishi wao ulisaidia kufanikisha baadhi ya mambo.

Mtikila alizitaja nchi hizo kuwa ni pamoja na maaskofu wa nchi ya Afrika Kusini, waliokuwa upande wa watu walioonewa wa vyama vya ANC na PNC, kwa Malawi viongozi wa dini 16 waliamua kwa pamoja kumpinga Rais Banda.

Hivyo hivyo ilifanyika katika nchi za Ukraine, Thailand na Kenya, ambao walikuwa na machafuko makubwa.

Chanzo: Tanzania Daima

My take -

Pamoja na kwamba mara nyingi huwa sichukulii maanani sana kauli za mchungaji huyu, lakini kwa hii kagonga kweli kweli.

Hakika baadhi ya viongozi wa dini ni wanafiki tu na wanatumiwa na chama tawala kuvuruga, na mara nyingine eti kuwapoza wapinzani.

Kama ni kweli kwa maamuzi/utashi wao wenyewe ndiyo uliwasukuma kwenda kumwona Dr Slaa kumbembeleza akubali matokeo, kwa nini wasiende pia kwa JK kumueleza kwamba Tume yake (NEC) iliiba sana kura za wapinzani. Hapo ndiyo tungejua viongozi hao wa dini wako neutral!

Ni kweli viongozi wa dini wanafiki kabisa hapo nimekuunga mkono na kumkubali Mtikila kusema ukweli! Haiwezekani wao waende kwa Slaa na kumwomba akubali matokeo, hali wakijua yalichakachuliwa! Kama kweli wapo kwa ajili ya kudumisha amani kwanini hawakumwendea Kikwete au Makame na kumweleza kuwa wizi wa kura wanaoufanya unahatarisha amani ya nchi yetu.
 
mi huwa nasema hapa, mtiila atakuja kumbukwa sana hapo baadaye baada ya sis wadanganyika kuwa na elimu sashihi ya uraia....
big up mchungaji.
 
Mtikila: Viongozi wa dini wanafiki

na Andrew Chale

MWENYEKITI wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, ameponda hatua ya ujumbe wa viongozi wa dini nchini kumtaka Dk. Willibrod Slaa, kukubali matokeo ya kushindwa kwenye uchaguzi wa rais uliomalizika hivi karibini na kuwafananisha na Yuda Eskalioti, aliyepewa vipande 30 vya fedha kisha kumsaliti Yesu.

Mtikila aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati akiongea na Tanzania Daima, akidai kuwa, kitendo hicho ni cha kinafki, kwani viongozi hao hawakupaswa kumfuata Dk. Slaa na ujumbe wao huo wa kumtaka akubali matokeo ili kulinusuru taifa na machafuko ya kisiasa.

Badala yake aliwataka viongozi hao wangeanza kwenda Tume ya Taifa ya Uchaguzi pamoja na Rais Kikwete ili kuona hatua ya kufuata ili kuzuia mpasuko uliopo sasa nchini.

"Tume imekubali kuwa kulikuwa na makosa mbalimbali kwenye uchaguzi na watayafanyia kazi ili yasitokee tena, vivyo hivyo walitakiwa kumfuata na Rais Kikwete ili kumuona angesemaje juu ya hatua hiyo ya Dk. Slaa, lakini kwa kitendo cha kwenda kwa Dk. Slaa sasa ni cha kinafki na ndio wanaoifanya dini kama mradi wa kuficha maovu," alisema Mtikila.

Akinukuu vifungu vya Biblia, kikiwamo cha Tito 2:11, Waraka wa pili wa Timotheo 4:2, ambavyo vyote vinalaani na kukemea machafuko na dhuluma kwa wanadamu, Mtikila alisema kuwa viongozi wa dini wameafiki hali ya uchakachuaji uliofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kuiba kura za wananchi na kudhani ni za Dk. Slaa.

"Kilichotakiwa kufanywa na viongozi hawa wa dini kama wanaona kuna machafuko, walitakiwa wagome kwa pamoja hatua ya kuapishwa kwa rais na kudai maridhiano ya pamoja. Lakini wao waliafiki moja kwa moja kwa kukubali kupewa vipande 30 vya fedha kama Yuda na kisha kumsaliti Yesu," alisema Mtikila.

Aidha, Mtikila alikubaliana na hatua hiyo ya Dk. Slaa kuyakataa matokeo hayo yaliyochakachuliwa, kwani ni kitendo cha dhahiri, anasimamia masilahi ya taifa ambalo lilimchagua ili awakomboe.

"Kura zilizoibwa na CCM ni za wananchi wote wa Tanzania wanaopenda mageuzi ya kweli, waliochoka na manyanyaso na masuala ya ufisadi, ijulikane hawakumuibia Dk. Slaa ambaye kura yake ni moja tu," alimalizia Mtikila.

Alisema kuwa kama ingekuwa ni wahuni tu wanamfuata Dk. Slaa na kumtaka akubali matokeo, tungesema wameshalewa madawa, lakini viongozi wa dini ambao ni taswira kwenye taifa ni jambo la kushangaza, halitavumiliwa kamwe na lisifumbiwe macho," alisema Mtikila.

Pia aliweza kutolea mfano juu ya nchi mbalimbali ambazo viongozi wa dini waliamua kupambana waziwazi ili kulinda hali ya amani, ikiwemo kutoa ushawishi mkubwa wa kupatikana haki ya msingi, ambapo ushawishi wao ulisaidia kufanikisha baadhi ya mambo.

Mtikila alizitaja nchi hizo kuwa ni pamoja na maaskofu wa nchi ya Afrika Kusini, waliokuwa upande wa watu walioonewa wa vyama vya ANC na PNC, kwa Malawi viongozi wa dini 16 waliamua kwa pamoja kumpinga Rais Banda.

Hivyo hivyo ilifanyika katika nchi za Ukraine, Thailand na Kenya, ambao walikuwa na machafuko makubwa.

Chanzo: Tanzania Daima

My take -

Pamoja na kwamba mara nyingi huwa sichukulii maanani sana kauli za mchungaji huyu, lakini kwa hii kagonga kweli kweli.

Hakika baadhi ya viongozi wa dini ni wanafiki tu na wanatumiwa na chama tawala kuvuruga, na mara nyingine eti kuwapoza wapinzani.

Kama ni kweli kwa maamuzi/utashi wao wenyewe ndiyo uliwasukuma kwenda kumwona Dr Slaa kumbembeleza akubali matokeo, kwa nini wasiende pia kwa JK kumueleza kwamba Tume yake (NEC) iliiba sana kura za wapinzani. Hapo ndiyo tungejua viongozi hao wa dini wako neutral!

Hawapaswi kuwa neutral!. Wawe upande wa HAKI
 
Back
Top Bottom