Mtikila: Slaa alishinda kwa 71%

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,975
9,566
Mch. Christopher Mtikila amesema kwamba Dr. Slaa alishinda uchaguzi wa urais kwa 71%, na anamshangaa Dr. Slaa kwa kutokuchukua hatua za kisheria kudai haki yake.

Hata hivyo CHADEMA wametoa tamko rasmi kuwa hawayatambui matokeo ya urais, na hawamtambui Kikwete kama rais wa Tanzania.

source: Mwananchi.
 
Well, 'm impressed 2 hear he said that. Lipumba should swallow his pride & admit the same hata kama ni underground supporter wa sisiem.
Ningependa kama Dr. Slaa angefungua kesi mahakaman petitionin matokeo yaliyochakachuliwa
 
Mtikila asituletee hapa mambo ya ajabu, tunajua CHADEMA ilishinda lakini mambo ya kumshinikiza Dr. Slaa aropoke hatuyataki. Dr. Slaa hayupo pekeyake katika chama, hivyo tamko atakalo toa lazima lijadiliwe kichama na lipate baraka za chama.:nono:
 
Well, 'm impressed 2 hear he said that. Lipumba should swallow his pride & admit the same hata kama ni underground supporter wa sisiem.
Ningependa kama Dr. Slaa angefungua kesi mahakaman petitionin matokeo yaliyochakachuliwa

Katiba na Sheria ya Bongo hairuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais kupingwa mahakamani. Ndiyo maana tunataka iundwe tume huru ya uchaguzi, na kufanywa kwa marekebisho ya katiba.
 
mtikila noma sana,anasema pia idadi ya wapiga kura ilipungua kwa sababu walimuengua yeye kugombea uraisi
 
many people believe as Mtikila the difference is that he has the guts to speak it in public
 
thanks ma man! Rev. Mtikikila, a very charismatic leader.....and a fighter too. I miss him.
 
Katiba na Sheria ya Bongo hairuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais kupingwa mahakamani. .
Katiba hiyo hiyo katika kipengele kimoja kinachohusu tume ya uchaguzi na ambacho kiko nyuma ya pazia kinatamka kuwa;
kifungu kidogo na. 1:
Kutakuwa na tume ya uchaguzi itakayo teuliwa na raisi na kuhakikisha kuwa mgombea wa uraisi wa chama tawala anashinda katika kila uchaguzi ambao Tume itasimamia.
Kifungu kidogo na. 2:
Kukiwa na jambo lolote ambalo tume itahitaji ufafanuzi basi tume itarejea kifungu kidogo na. 1 hapo juu!
 
... yeyote mwenye taarifa sahihi zaidi atuwekee hapa chini kuhusu source ya Mtikila ya huu ushindi wa 71%, please!!!!!!!!
 
Mch. Christopher Mtikila amesema kwamba Dr. Slaa alishinda uchaguzi wa urais kwa 71%, na anamshangaa Dr. Slaa kwa kutokuchukua hatua za kisheria kudai haki yake.

Hata hivyo CHADEMA wametoa tamko rasmi kuwa hawayatambui matokeo ya urais, na hawamtambui Kikwete kama rais wa Tanzania.

source: Mwananchi.

Namwomba Mtikila akasome kwanza ibara ya 41 (7) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndipo aongelee suala hili.
 
Katiba hiyo hiyo katika kipengele kimoja kinachohusu tume ya uchaguzi na ambacho kiko nyuma ya pazia kinatamka kuwa;
kifungu kidogo na. 1:
Kutakuwa na tume ya uchaguzi itakayo teuliwa na raisi na kuhakikisha kuwa mgombea wa uraisi wa chama tawala anashinda katika kila uchaguzi ambao Tume itasimamia.
Kifungu kidogo na. 2:
Kukiwa na jambo lolote ambalo tume itahitaji ufafanuzi basi tume itarejea kifungu kidogo na. 1 hapo juu!

Sasa kama ndio hivi jamaa wametekeleza matakwa ya katiba kwa kukihakikishia ushindi chama kilichoko madarakani,hii inaonyesha kwamba tuko kwenye mfumo tofauti na ule ambao katiba ilitengenezwa kwa ajili yake.Hivyo hoja ya kusukuma mabadiliko ya katiba ni muhimu sana.
 
Namwomba Mtikila akasome kwanza ibara ya 41 (7) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndipo aongelee suala hili.

Mwanamayu:

Ibara ya 41 (7) Inasema: Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka yakuchunguza kuchaguliwa kwake.

(7) When a candidate is declared by the Electoral Commission to have been duly elected in accordance with this Article, then no court of law shall have any power to inquire into the election of that candidate.

Kimantiki ibara hii inasema kuchunguza. Hakuna mahakama inayofanya uchuguzi. Kazi ya mahakama ni kutoa maamuzi ya kisheria baada ya kusikiliza hoja kutoka pande zinazopingana.

Je umeshawahi kusikia kuwa mahakama inamfanyia uchunguzi mtuhumiwa wa mauaji au mwizi? kusema ukweli hata lugha ya kiswahili inarudishwa nyuma kwa kufanya arbitration na Investigation kuwa kitu kimoja.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom