Provisional, Meaning and Constructivism rely heavily on imposed ideologies, those are the basis that forms a human reason-ability or the commonsense. The're based on past experience and socialization process that is to say a human nature is never a myth scientifically to a large extent, explore the human thinking and you would understand his/her socialization process.
That is the beauty of knowledge it makes you aware of those procedure and how they are acquired before becoming your ideas.
Knowledge allows you to make rationale decisions, since politics is a study of managing social creature it is a matter of aspiring politicians utilizing what they understand about human ideas and how to make them work for the better whole. Therefore a politicians has to think in terms of benefiting his society whilst including every ideology.
I beg differ with you. Ukitaka utawala wa haki na sheria ni lazima ujifunze au uwe na utaratibu wa kufuata vyombo vya sheria. Mtikila anatumia katiba japo haipendi. Na anakwenda mahakama japo kuwa mahakama zetu ni za kubabaisha.
Viongozi wengi wa upinzani wameisoma katiba baada ya uchaguzi wa 2010. Na mahakama hawataki kuitumia. Je utamaduni wa kutumia katiba, sheria na mahakama watejenga lini? Wakiwa watawala?
Nakubaliana na wewe, and mahandamano na mikutano also falls under utawala wa sheria na katiba. Lakini swala siyo kujifunza utawala washeria au kufuata sheria, mi nadhani la muhimu ni which strategy is the best to win your case. Hauwezi kushinda mahakamani kila siku ilikumconvince mtu kijijini kwa ccm is a ****. Hotuba, mikutano au vipeperushi is one of the best to address critical issues, na ndo maan tunashule and university and we do not do home schooling. Swala la mahakama could be a political strategy but is very weak. Mahakama to me should be used only if the level of intelligence in politics is within our reach. But, i dare to say, chadema is perhaps far and beyond the interpretation of our laws kwenye mahakama. Its good for Mtikila coz he lks to make contraverse, may be he is genetically predispose to do that. Otherwise, si amini kama kushinda mahakamani ni nnjia bora ya kujenga chama au kueneza sera za chama.
Huyu Mtikila hata UHURu wetu aliupinga akisema wazungu walikuwa watu bora sana ndio walotuletea ustaarabu (dini) na kadhalika leo waondolewe kwa kuitwa mabeberu!. Alipingana na dhana nzima ya Uhuru wa mwafrika leo mnamwona ndiye hero wenu? ama kweli sasa naanza kuelewa wapi hasa tunapogongana..
Kwa hiyo hata wewe unapingana na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar sio? Kiini macho ni swala jingine kabisa na kupinga muungano wa Tanganyika na Zanzibarakifikia kushtaki na kudai usd millioni 160.. Lazima ujue tofauti.. na kuhusu mahubiri sijui wewe unaelewa vipi au unakisia vipi?..
Katika hilo mkuu wangu tupo wengi sana tu tunahoji Muungano lakini kwa mwenye kufahamu ataelewa wazi kwamba ndio njia pekee ilituwezesha kuwa pamoja kwa miaka karibu 50. Nina hakika serikali tatu ingekufa hata kabla ya miaka 10, serikali moja isingechukua miaka 10 kwa sababu sisi MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO na tutaendela kuwa watumwa wa fikra za kugawana umaskini. PanAfricanism isingewezekana ikiwa hili dogo la nchi mbili tu limetushinda wala sio sisi tu Tanzania bali nchi kibao zimetengana baada ya miaka 10 na zinaendelea utengana kila siku. Sasa tunagombania mipaka tena ya maji ambako watu hawaishi isipokuwa kuna nmafuta, halafu wanasema kwa nini hatukuweka mipaka yetu wakati wa Uhuru. Hapo PanAfrica utaitazama wapi na viongozi wa leo kina mama banda wanaotumia ushahidi wa mwaka 1800..Mkuu Mkandara,
Tuliache suala la mtikila na madai yake ya mamilioni, naomba uelewe kwamba msingi wa hoja yangu ni madai ya Tanganyika hata kama mtikila hata husishwa; Lakini kabla sijaenda mbali, naombe nisema kwamba: Nitakuwa mwehu kama itaeleweka kwamba Mchambuzi anapinga muungano; Naomba iende on records kwamba sipingi muungano bal mfumo wake, na ninapendelea tuwe na serikali tatu kwani hivyo ndivyo tutaweza kuimarisha muungano huu ambao hakika tunauhitaji sana, na kama tunautakia mema, ni lazima tuache siasa na viini macho na tuangalie realities, vinginevyo tutauvunja bila kutegemea;
I strongly believe in panafricanism above all, na ni Nyerere ndiye ambae alimpinga Kwame Nkrumah juu ya THE MEANS TOWARDS A UNITED STATES OF AFRICA; lakini cha ajabu, ni yeye alikuja kukosea kuhusu the MEANS kwa Tanzania; with all due respect to Mwalimu, hapa alikosea na nisingependa kuwa mwoga au mnafiki kuweka msimamo huo;
On the one hand, Nyerere alihimiza umuhimu wa kuanza na regional blocks kama vile EAC, ECOWAS lakini muhimu zaidi kwana kulikomboa bara zima kwanza, kabla ya fikra za Nkrumah za UMOJA WA AFRIKA; On the contrary, Nkrumah yeye alitaka Afrika iungane right away; in the short run, Nyerere alionekana dhaifu kihoja na Nkrumah akageuka kuwa a REAL PANAFRICANIST, lakini baada ya miaka mingi, sasa historia imempa alama ya "A+" Mwalimu Nyerere juu ya means towards a UNITED STATES OF AFRICA, huku Nkrumah akipata tu credit ya kuanzisha wazo hilo but marks anazopata kwenye suala la MEANS ni ndogo sana ingawa sio "F";
With all due respect to muungano and Nyerere's vision, kwa kweli he rushed suala hili sana, may be because it transpired in the womb of Cold War ambapo marekani walikuwa wanaogpa sana Zanzibar pengine isigeuke kuwa another Cuba, especially baada ya vurugu za Chege kule East Congo; Mbaya zaidi ni kwamba muungano pamoja na kuwa ni wazo zuri, ulijengwa kwa mfumo wa kuiga iga hiki na kile kwani hauku reflect realities on the ground bara na visiwani licha ya kwamba zanzibar na ukanda wa pwani wa tanganyika ulikuwa na historia na muingiliano wa muda mrefu, na hata kuwa himaya moja ya Sultani katika kipindi fulani; Vinginevyo muundo wake uliiba a few elements za United Kingdom, na hili Nyerere alilizungumza wazi na lipo kwenye vitabu vingi vya historia; kwa mtazamo wangu, hili likawa kosa la kwanza, na kosa hili lilikuja kuwa dhahiri zaidi pale assumption za Mwalimu kwamba pengine Tanzania ingeendelea kuwa nchi ya chama kimoja for the next unforeseable future ilipogota, kwani katika suala la muungano, suala la vyama vya siasa halikutajwa - halikuwepo na bado halipo kwenye hati ya muungano, lilikuja ingia baadae kwenye katiba ya muda mwaka 1965 kwa mara ya kwanza;
Kwa kifupi, mwalimu hakuweka provision of WHAT IF baadae another political party wins visiwani, na chama kingine wins bara katika uchaguzi mkuu; katika hali ya kuchanganyikiwa, mfumo wa vyama vingi ulipo ingia, mwalimu akampa Jaji Bomani jukumu la kutafuta suluhisho juu ya hili, na ndipo Jaji akapendekeza mfumo wa mgombea mwenza unaotumika Marekani; kwahiyo, mfumo wetu wa muungano upo based on muundo wa Unitary Government wa Uingereza na Federation government ya Marekani, kuwaunganisha wananchi walio mbali kabisa from these two contexts; Kama wahenga wetu walivyonena, mshika mawili, moja humponyoka, .... Surely, this was not going to work, na ndio maana leo tupo kwenye mgogoro huu mkubwa kwa kujitakia;
Mkuu Mkandara, inastaajabisha wewe kutoona madhaifu kama haya, ambayo ni muhimu tuyarekebishe ili tuweze kujenga muungano ulio imara; nitafafanua mengi zaidi katika makala yangu ya kumuunga mkono Tundu Lissu juu ya msimamo wake kuhusu muungano wetu;
Mchambuzi
Unasoma makala za Mzee Mwanakijiji hukusu Muungano?
Unasoma michango ya Nguruvi3 na JokaKuu kuhusu Muungano?
Hawa watu wanawafundisha wazanzibari kujitoa kwenye Muungano lakini hawashajihishi au kutoa elimu kwa wadanganyika kudai Tanganyika.
Katika JF hawa ni watu wa fikrapevu lakini linapokuja suala la kudai Tanganyika na serikali ya Tanganyika huwa wanakuwa kama kuku aliyemwagiwa maji. Huwa napata mashaka wakati mwengine kama Chai Chapati Maharage wamewaweka mfukoni au ni kuhofia utaifa wa Tanganyika dhidi ya utanzania?
Mbona utaifa mbili unawezekana? (dual nationality), mfano british lakini pia ni english, scotish au welsh.
Bado hata Lissu ameishia kauli ya kusema upo umuhimu wa kuirudisha Tanganyika, vitendo bado (awasilishe mswada bungeni unaodai kuirudisha serikali ya Nchi ya Tanganyika ili kumaliza hiki kiini macho.
Liko wapi kundi jipya la G55 au G110?
Hiki ni kipindi cha kutoa maoni kuhusu katiba mpya, hakuna anaetoa elimu kwa wananchi kudai serikali ya Tanganyika bali wapo akina MMjj na Nguruvi3 wanaotushajihisha tudai serikali moja.
Siasa za Tz zinaweza kumtia mtu maradhi ya moyo.
Nguruvi3, Mzee Mwanakijiji karibuni katika hili kundi la kudai serikali ya Tanganyika na saa ya ukombozi ni sasa!
Are you sure? How?
I beg differ with you. Ukitaka utawala wa haki na sheria ni lazima ujifunze au uwe na utaratibu wa kufuata vyombo vya sheria. Mtikila anatumia katiba japo haipendi. Na anakwenda mahakama japo kuwa mahakama zetu ni za kubabaisha.
Viongozi wengi wa upinzani wameisoma katiba baada ya uchaguzi wa 2010. Na mahakama hawataki kuitumia. Je utamaduni wa kutumia katiba, sheria na mahakama watejenga lini? Wakiwa watawala?
Huyu Mtikila hata UHURu wetu aliupinga akisema wazungu walikuwa watu bora sana ndio walotuletea ustaarabu (dini) na kadhalika leo waondolewe kwa kuitwa mabeberu!. Alipingana na dhana nzima ya Uhuru wa mwafrika leo mnamwona ndiye hero wenu? ama kweli sasa naanza kuelewa wapi hasa tunapogongana..
Hakuna mwanasiasa yeyote nchini tangu uhuru ambaye amepigania haki za kiraia na kushinda kama Christopher Mtikila. NInaamini historia itakuja kumkumbuka kama shujaa wa demokrasia kwani pamoja na yote ambayo amepitishwa ameendelea kusimama kudai haki za raia wa Tanzania kwa namna ambayo mahakama zimekuwa upande wake mara ZOTE!
Leo hii napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa mtetezi huyu wa haki za raia. Ni mwanasiasa pekee ambaye amefanikiwa kulazimisha serikali kufanya isiyotaka kufanya na hata ilipokataa kufanya ametuwezesha kuona kuwa serikali haitaki kwa sababu tu haipendi si kwamba hoja ziko upande wake. HE IS MY HERO!
Ukweli ni kuwa amewapita kwa mbali sana wale wanasiasa wetu ambao labda majina yao ni maarufu sana na ambao wanaonekana ni maarufu; siyo tu Mtikila anazungumza anachozungumza bali anafanya pia anachozungumza. Of course, haiondoi ukweli mwingine wa mapungufu yake au siasa zake lakini ukweli ni kuwa kila alipojaribiwa na watawala amewashinda. Rekodi yake ya ushindi kwa miaka ishirini na ushee sasa inasimama kama ushahidi wa ushujaa wake.
Inasikitisha haijatokea wanasiasa wengine wa upinzani hata mara moja kuwa sehemu ya kesi zake au kuonekana wanajiingiza kama friends of the court (amicus curiae) kuonesha wanaunga mkono hoja zake.
When it comes to the 'walking' Mtikila does the walk!
Sawa sawa mkuu, nimekuwa naandaa mjadala wa namna hiyo, hasa nikilenga kufafanua kwanini Lissu yupo sahihi anaposema muungano wetu ni kiini macho; nitakuwa tayari na mada hiyo kabla ya mwisho wa mwezi;