Mtikila: Shujaa wa Demokrasia, Mwanamapinduzi halisi na Shujaa wangu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtikila: Shujaa wa Demokrasia, Mwanamapinduzi halisi na Shujaa wangu...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Sep 25, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Sep 25, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Hakuna mwanasiasa yeyote nchini tangu uhuru ambaye amepigania haki za kiraia na kushinda kama Christopher Mtikila. NInaamini historia itakuja kumkumbuka kama shujaa wa demokrasia kwani pamoja na yote ambayo amepitishwa ameendelea kusimama kudai haki za raia wa Tanzania kwa namna ambayo mahakama zimekuwa upande wake mara ZOTE!

  Leo hii napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa mtetezi huyu wa haki za raia. Ni mwanasiasa pekee ambaye amefanikiwa kulazimisha serikali kufanya isiyotaka kufanya na hata ilipokataa kufanya ametuwezesha kuona kuwa serikali haitaki kwa sababu tu haipendi si kwamba hoja ziko upande wake. HE IS MY HERO!

  Ukweli ni kuwa amewapita kwa mbali sana wale wanasiasa wetu ambao labda majina yao ni maarufu sana na ambao wanaonekana ni maarufu; siyo tu Mtikila anazungumza anachozungumza bali anafanya pia anachozungumza. Of course, haiondoi ukweli mwingine wa mapungufu yake au siasa zake lakini ukweli ni kuwa kila alipojaribiwa na watawala amewashinda. Rekodi yake ya ushindi kwa miaka ishirini na ushee sasa inasimama kama ushahidi wa ushujaa wake.

  Inasikitisha haijatokea wanasiasa wengine wa upinzani hata mara moja kuwa sehemu ya kesi zake au kuonekana wanajiingiza kama friends of the court (amicus curiae) kuonesha wanaunga mkono hoja zake.

  When it comes to the 'walking', Rev.Mtikila does the walk!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ni mpigaji mzuri asiyekata tamaa!
   
 3. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,522
  Likes Received: 2,108
  Trophy Points: 280
  Published on Sep 25, 2012 by ITV TANZANIA

  Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu imemwachilia huru mwenyekiti wa Democratic Party - DP Mchungaji Christopher Mtikila baada ya ushahidi uliotolewa na jamuhuri dhidi yake katika kesi ya uchochezi iliyokuwa ikimkabili kutokuwa na ushahidi wa kutosha kumtia hatiani.  Source: ITV TANZANIA youtube
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  teh teh teh! Mtikila is one of those characters with formidable influence in the public. Ila kila zuri halikosi kasoro...Rostam alimuweza kweli.
   
 5. denoo49

  denoo49 JF-Expert Member

  #5
  Sep 25, 2012
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 5,647
  Likes Received: 5,240
  Trophy Points: 280
  Mkuu uko sahihi.

  Changamoto alizozitoa katika serikali na mahakama zitabaki kuwa historia ambayo haitakaa kamwe ifutike katika ukombozi wa Tanzania mpya.

  Tutajifanya kufumba macho lakini ipo siko na "kope" zetu zitachoka.

  Mpaka leo kesi ya mgombea binafsi imebaki kua msumari wa moto kwa hizo nguzo mbili tajwa hapo juu.

  Let God show his mercy.
   
 6. kisugujira

  kisugujira JF-Expert Member

  #6
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 769
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huyo ndiye Simba wa Tanganyika. Big up mzee wa saa ya ukombozi.
   
 7. A

  Ame JF-Expert Member

  #7
  Sep 25, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Umeniwahi...Isingekuwa njaa basi leo hata EPA angekuwa kesha tuwakilisha vizuri ... I realy admire his attitude!
   
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  Sep 25, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Vizuri umesema HERO WAKO lakini sii wangu miye kwa sababu siku zote anapigania haki yake yeye na sii ya WANANCHI. Kama nguvu hii ageiweka ktk kupigania haki za wananchi bila shaka kama sio mwaka 1995 basi 2000 angechukua nchi..MTIKILA ni Mbinafsi, mtu anayependa sana kutetea na kulinda maslahi yake kama mgombea..
   
 9. A

  Ame JF-Expert Member

  #9
  Sep 25, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Umenikumbusha mbali sana nakumbuka enzi hizo kati ya 1993/94 alitupandisha mori tukachuma majani tukiwa pale viwanja vya pale jangwani tayari kwenda kuyavamia majengo na magari ya magabachori waliotusababishia umasikini na rushwa iliyo kithiri (according to him)....Tusikutane na nguvu ya FFU bwana wee japo enzi hizo walikuwa hawauwi bali macho na miili ilikoma! Jamani tumetoka mbali na ukombozi wa hii nchi...
   
 10. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #10
  Sep 25, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Namkumbuka zaidi katika harakati zake za kuidai Tanganyika yetu pamoja na mabadiliko ya KATIBA yatakayoruhusu mgombea binafsi. Shujaa huyu alifungua kesi mahakamani na kushinda shauri lake litakaloweza kuruhusu mgombea binafsi. Lakini kutokana na sisi wananchi kutomuunga mkono, pamoja na serikali kuhofia utekelezaji wa shauri hili, ulilitupilia mbali na kueleza juujuu kuwa serikali haipo tayari kwa hili. Mtikila amesaidia sana kufumbua macho wananchi wengi, na bilashaka sasa ni wakati wa kuyasimamia mawazo yake mazuri mengi pamoja na ya wadau wengine katika mchakato wa kuipata KATIBA yenye tija kama kweli mfumo wa kuipata utaruhusu hilo.
   
 11. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #11
  Sep 25, 2012
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  MMK unachekesha, eti Mtikila atakuwa hilo! unadhani ingekuwa kesi hii inamuhusu Wenje, MSIGWA au Lema ingekuwa na sura gani? hukumu ya leo ingekuaje? tafakari! State wanajua Mtikila hana impact yoyote kwao, mwaka 2008 nilikwambia rudi nyumbani haukunisikia, mwisho kuna kitu nitakushirikisha wakati ukifika ili uweze kushauri,
   
 12. commited

  commited JF-Expert Member

  #12
  Sep 25, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  nimemuona leo baada ya kushinda kesi yake ya kukutwa na nakala za uchochezi ameishinda jamhuri, lakini pia mbele ya waandishi wa habari amekataa kushikwa na polisi, akimwambia yule polisi" wewe unacheo kidogo sana wala huwezi kunikamata, nenda kawaambie wakubwa zako waje" polisi amenywea mbaya mbele ya kamera.. huyu mzeee ni jasiri sana sijui ni wanagapi tuoweza kufanya hivi.... kwa kiasi fulani ni mtu makini na anayezijua sheria sana angekuwa cdm huyu.. kakutana na mzee Tundu lissu, wakina zitto, na prof safari daah magamba yangekufa kabisa mwaka huuu
   
 13. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #13
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Ukweli huu usiopingika ni alama dhahiri umesoma sana mwenendo wa huyu mpigania haki mashuhuri katika nchi hii tangu mfumo wa vyama vingi uingie nchini.

  Umashuhuri wake zaidi umejionyesha pale watanzania wengi kutomuunga mkono katika hoja zake kivitendo ingawa zinasomeka wazi ni za msingi na muhimu. Pamoja na kuwa peke yake hakukata tamaa amekuwa mpiganaji kuwashinda wale wa vita vya msituni hadi kuitikisa serikali mahakamani na kuishinda mara kadhaa licha ya vitisho kama katika kesi yake iliyomalizika leo kusingiziwa.

  Wanasiasa wengi Tanzania hasa vyama vya siasa hawajaonyesha ushirikiano na mpigania haki huyo kwa kile tulichokizoea kukosa umoja kwa vyama vya upinzania hali ambayo imechelewesha hata mageuzi Tanzania tofauti na nchi kadhaa zinazotuzunguka katika kuendesha wimbi la mageuzi ya kweli kwa kukata mzizi wa fitina unaolindwa na watawala kujizatiti kwa kupokezana vijiti kana hatuna wenye uwezo na nafasi ya kufanya hivyo.

  Mtikila udhaifu wake pia wa kutowakubali au kuwapa nguvu wanasiasa wenzake katika vyama vya upinzani huenda ni chanzo cha kutopata ushirikiano wa kutosha, hata hivyo sioni kama hoja ya kutompongeza kwa vile ayafanyayo ni mahsusi kwa demokrasia ya kweli katika nchi yetu, kama wastaarabu na waungwana tuna haki ya kumpongeza kwa nguvu moja kwa ushujaa alio nao, kwani amepigania haki za watanzania wote bila kujibakisha hadi kufikia pengine kuhatarisha usalama wake, ila tegemeo lake kama mchungaji ni Mungu pekee.

  Naam, histori haitamwacha mtu huyu mashuhuri katika kutetea demokrasia ya kweli nchini mwetu bila woga, bila kukata tamaa, hadi kuishinda serikali mahakamani mara kadhaa kwa nia moja tu kutetea wanyonge wa taifa letu.

  Ipo siku utajengwa mnara wa kumbukumbu yake katika kijiji alichozaliwa kiitwacho Milo kando ya mapangano ya milima ya Livingstone huko Upangwani iliyojipindapinda na magenge mengi kuteremkia bonde kuu la ufa huko Ziwa Nyasa ambako wenyewe wa huko ni sawa na nabii hakosi heshima ila katika nchi yake mwenyewe, aka wilayani Ludewa kwa mwanamapinduzi mwenzake Deo Filikunjombe.
   
 14. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #14
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hakuna binafsi aliye mkamilifu, kila mmoja wetu hapa na wengineo wote wanazo kasoro nyingi ambazo kama tungeziweka wazi tungeona mapungufu ya kila mmoja. Tunachokiongelea hapa ni makubwa aliyofanya katika kukuza demokrasia, tunapaswa kumpongeza bila kujali mapungufu yake binafsi pengine ndiyo yaliyo sababisha chama chake kikose kukua licha ya kuwa ni mpiganaji mashuru pengine number one nchini bila kukata tamaa wala kurudi nyuma, lakin pamoja na mapungufu hayo, Mungu humwandaa kila mmoja kwa makusudio yake.

  Hata timu ya mpira uwanjani ni wachezaji wachache wanaoweza kucheza nafasi zote na ni nadra sana, hivyo kwa nafsi yake amefanya kweli na ulimwengu unamtambua ndo maana amefanikiwa kwa nguvu ambayo hatuijui na amepataje nguvu ya uwezo wa kiakili na kiuchumi kupigania hayo, maana kesi kama hizo mahakama ni ghali sana unaposhindana na dola yenye kuendesha uchumi wa nchi.
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Sep 25, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kwani kuna mmoja wetu hapa anagombea URAIS?..mkuu tunataka kuwapima wananchi vipi ikiwa hawagombei urais na wala hawapo kujisifia wao kwa kesi hizi. Hivi kweli mnataka kunambia ni Mtikila pekee ambaye kapelekwa mahakamani na akashinda kesi au ushujaa wake unatokana na nini?. Labda nifahamishe Ushujaa wake unatokana na yepi alowatetea wananchi wote kama sio nafasi za kisiasa zinazomhusu yeye..
   
 16. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #16
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,558
  Likes Received: 1,903
  Trophy Points: 280
  Mtikila ameisoma katiba vyema na kuielewa,ni mtu anayefahamu haki zake,lakini mbinafsi sana.Mtu anayeyumbishwa kwa mlungula hata iwe vipi hawezi kuwa hero wangu.Toka alipopokea ile pesa ya RA na ushahidi ukawekwa,pamoja na kule Tarime alipotumika hadi akapopolewa mawe,sina imani naye.However kwenye kupambana kuhusu haki flani flani na kesi dhidi ya serikali yupo fit.Isipokuwa mara zote ni issue zake binafsi na hazionyeshi benefits kwa general public.
   
 17. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #17
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  MMM umenishangaza sana

  Unasifia mtu anayeshindana na mfumo dhalimu vipi kama naye ni mmoja wao ila ndio wanaotumika kama decoys??

  umeshawahi kuimagine wengine wangefanya afanyayo mtikila wangekua wapi??

  I would label him as a hero, coz he usually shed his skin when needed, remember 2010 kuanzia may hadi september??
   
 18. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #18
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Well said Mzee Mwanakijiji, lakini itafikia wakati historia itamweka sehemu anapohusika, hasa hii hypnosis [kiini macho] cha muungano kitakapo tatuliwa; Nataka nikufahamishe tu Mzee Mwanakijiji kwamba Mtikila ni SHUJAA WA TANGANYIKA, na ADUI WA TANZANIA yenye muundo mbovu wa kiutawala (muungano wenye misingi mibovu na ya ovyo), ndio maana kwa sasa amefifia; Lakini yote yatageuka with the RESURRECTION of our state of Tanganyika; Kwa kushirikiana na waelewa wengine wengi tu kama kina Tundu Lissu na wengineo, ipo siku tutafanikiwa; Ni bahati mbaya tu the fact kwamba he is a reverend imechangia sana jamii kupotoshwa kuhusu Mtikila na hivyo shujaa huyu kutopewa attention yenye uzito uliostahili wakati ukweli ni kwamba harakati zake zimekuwa very secular;

  Long live Christopher Mtikila, umeteseka sana kwa kupigania haki yetu ya KIKATIBA, ingawa tulipumbazwa sana tukudharau kama vile wewe ni CHIZI NA MCHOCHEZI; Tumeshatenga pumba na mchele, na tutaendeleza pale ulipoishia na nina uhakika ipo siku watakaobaki katika mapambano watafika;
   
 19. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #19
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hoja moja ambayo inaweza kutia uzito wa suala hili ambalo hata mahakimu wa afrika katika kesi inayoendelea kuhusu mgombea binafsi walimwuliza kwamba yeye ana chama cha siasa ambacho yuko na nafasi ya kugombea, kwa nini ahangaikie kutetea nafasi ya mgombea binafsi.

  Ukweli unaanza kujitokeza kwamba huyu mchungaji ni kama nabii wa taifa la Isaeli aliyekuwa anapigania haki za waisraeli, ndivyo ilivyo kwa huyu kwamba anapigania haki za wengi ambazo wengi wetu hwajadiriki hata kuipeleka serikali mahakamani.

  Mauaji yaliyotokea Iringa na Chadema kusumbuliwa kwa kukataliwa vibali, nilimwandikia barua pepe na kuweka uzi hapa JF kwa viongozi wa chadema kwamba sasa wageukie upande wa kudai haki zao Mahakamani kwani kushinda kugombania haki kwa mtindo wa sasa ni kuzidi kuumiza wanachi, wanachana na viongozi kwa viatendo viovu vya serikali.

  Hata hivyo hakuna hatua iliyochukuliwa wala hawakunijibu ujumbe wangu. Mtikila angeshawafungulia mashtaka mahakamini kwa vile mahakani ni kushindana kwa hoja, lakini kwa mtindo wa sasa Chadema wanaongea peke yao mitaani wakati serikali ikiwa juu ya jukwaa kama jogoo na kusema watanifanya nini.

  Hilo tu ni mfano mzuri wa uimara na umaarufu wa mtikila katika kuilaza serikali mahakamani na kuishinda katika kesi kadhaa ikiwepo ya kudai mgombea binafsi.
   
 20. N

  Nonda JF-Expert Member

  #20
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Sasa anajitayarisha kudai serikali ya Tanganyika.

  Katika hili pia anabaki ni shujaa kwako?

  link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/279351-mtikila-kufungua-kesi-kudai-tanganyika.html

  link Mtikila ajiandaa kufungua kesi kupinga mchakato wa Katiba

  Kwa nini hili huwa unalipiga chenga? Kwa nini hatumuungi mkono kuirejesha Tanganyika?
   
Loading...