Mtikila: Nitaenda mahakama ya kimataifa kwa ajili ya kufungua kesi kuhusu Rasimu ya Katiba

mageuzi1992

JF-Expert Member
Apr 9, 2010
2,503
252
Christopher mtikila amesema kuwa ataenda mahakama ya kimataifa kwa ajili ya kufungua kesi kuhusu rasimu ya katiba kutoitambua tanganyika.....hapa namuunga mkono mia kwa mia. Mtakubaliana nami kuwa siku chache zilizopita tumesikia habari ya kutolewa kwa rasimu ya katiba....rasimu hii si katiba kamili bali ni hatua kuelekea katiba kamili. Rasimu hii inatoa fursa kwa watu mbalimbali kuikosoa au kueleza baadhi ya mambo ya kuongeza au kupunguza.

Kuna mambo machache ambayo tusipokuwa makini na kuendelea kuisifia sifia bila kuichambua kwa umakini tutakuja kushtukia '' majuto ni mjukuu''. Maneno haya hayamaanishi kuwa rasimu ni mbaya! Lahasha! Ina mambo mengi ambayo ni mazuri na yanayokidhi matakwa ya watanzania walio wengi. Kwa upande mwingine ina machache ambayo yasipowekwa sawa yataleta matatizo mbele....mfano...swala la kutoitambua tanganyika!!!!!!

Hatuwezi kuwa na serikali tatu mbili zinatambulika kwa majina sahihi wakati moja imenyimwa jina lake la asili....iweje isemwe kuwa serikali hizo tatu ni tanzania,zanzibar na tanzania bara hakuna nchi inaitwa tanzania bara...lazima katiba mpya itambue tanganyika kama moja wapo za serikali hizo tatu
 
Kwa kweli mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Mtu ambae amekuwa akipigania Tanganyika na Mgombea binafsi kwa muda mrefu sana ni Mchungaji Mtikila.
Nadhani kila mtu atakuwa anafahamu mchango mkubwa aliotoa Mchungaji Mtikila kwenye suala la Tanganyika na Mgombea Binfsi
Aliishinda serikali mara kkadhaa Mahakamani lakini Mahakama kuu nadhani kukiwa na shinikizo kutoka CCM wakatengua hukumu ya Mgombea Binafsi
Nadhani ni wakati muafaka wa majaji ambao waliwanyima waTZ wasio na vyama kushiriki kwenye Uchaguzi uliopitia (kwa kukataza wagombea binafsi bila sababu yeyote) waachie ngazi na kumuomba radhi Mchungaji Mtikila
Wana JF ni muda sijamsikia Mch Mtikila. Mtu yeyote anaweza kumhoji Mch kuhusu hii Rasimu ya katiba mpya na kuyaleta haya mahojiano hapa ingekuwa vizuri zaidi


Hebu tujikumbushe hukumu ya mgombea Binafsi
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-mgombea-binafsi-hii-hapa-ag-vs-mtikila.html
 
ukisoma rasimu ya katiba ibara ya kwanza na ya tatu inatamka neno tanganyika
 
Siyo mahakama kuu bali ni mahaka ya rufaa ndiyo iombe radhi. Mahakama kuu ilimpa ushindi mtikila lakini mahakama ya rufaa ikatengua.
 
serikali ya ccm imeuaminisha uma kuwa mch,mtikila ni mwehu,tena toka enzi za mwalimu,sumu hii imetembea kwenye mishipa ya kizazi cha mkapa na sasa jk,kwa hyo kila analoongea huonekana halina maana ila ndani ya miaka kadhaa unakuja kugundua what he said was true,na style hiyo hyo nape na mwigulu na kina mtelamko mwampamba na bi juliana nao wapiga kelele zile zile kuwa dr ana matatizo mara kibabu,but ukija kwenye fact sehemu kubwa ya maneno ya dr slaa hayana chembe ya uongo<sema kuna watu hawapendi ukweli ujulikana,uongo kwao ndiyo ukweli> kwa hyo na yeye anapigwa vita ya ajabu,kinachosaidia ni jamii kutambua mchango wake.

Mtikila kama una nia kweli pls go ahead,nenda mzee wangu,najua una mengi sana ila hakuna mahakama hapa nchini itakayo kusikiliza na kukuelewa zaidi ya huko uendako,kikubwa fata taratibu zote kikamilifu,hawakiwii kukuweka ndani tena mpk 2015
 
UTANGULIZI
KWA KUWA, Sisi, Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua
rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayoheshimu na kuzingatia misingi ya
utu, uhuru, haki, usawa, udugu, amani, umoja na mshikamano katika nyanja zote za
maisha yetu;
NA KWA KUWA, tunaamini kuwa misingi hiyo inaweza tu kutekelezwa katika
jamii yenye mfumo wa demokrasia na utawala bora ambayo Serikali yake inasimamiwa
na Bunge lenye Wabunge waliochaguliwa na wanaowawakilisha wananchi na Mahakama
huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote, na
kuhakikisha kuwa haki za binadamu zinalindwa na kudumishwa na kwamba wajibu wa
kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu;
NA KWA KUWA, umuhimu wa kutunza mali ya Mamlaka za Nchi na ya pamoja,
kupiga vita aina zote za uharibifu, ubadhilifu, na kuhimiza matumizi bora na endelevu ya
rasilimali na maliasili zetu pamoja na kulinda na kuhifadhi mazingira yetu kwa
mustakabali wa maisha ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo;
NA KWA KUWA, umuhimu na faida za kujenga, kukuza na kuendeleza, amani,
umoja, urafiki na ushirikiano miongoni mwa Watanzania, Mataifa mbalimbali ya Afrika
na Dunia kwa ujumla;
KWA KUWA, azma ya kujenga Umoja wa Bara la Afrika katika misingi ya
Umajimui wa Afrika ambao inadhihirishwa na Muungano wa iliyokuwa Jamhuri ya
Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar;
NA KWA KUENDELEZA, dhamira yetu hiyo ni muhimu:
(a) kulinda, kuimarisha na kuudumisha Muungano wa nchi za Jamhuri ya
Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar;
(b) kujenga Taifa huru na linalojitegemea;
(c) kuimarisha na kuendeleza utawala wa sheria;
(d) kukuza na kuendeleza maadili, uwajibikaji na uwazi;
(e) kujenga umoja na mshikamano utakaowezesha kutimiza malengo ya kisiasa,
kiuchumi, kijamii, kimazingira na kulinda urithi kwa ujumla;
(f) kujenga na kuendeleza ukuu wa mamlaka ya watu;
(g) kujenga na kuendeleza utii wa mamlaka ya Katiba; na
(h) kuimarisha na kudumisha uzalendo kwa Taifa miongoni mwa Watanzania;
NA KWA KUZINGATIA, urithi tulioachiwa na Waasisi wa Taifa letu wa kujenga
nchi yenye Umoja wa Watu wake ambao hawabaguani kwa misingi ya ukabila, udini,
rangi, jinsi au ubaguzi wa aina nyingine yoyote;
NA KWA KUZINGATIA, uzoefu wa zaidi ya Miaka Hamsini ya Uhuru na Miaka
Hamsini ya Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na
umuhimu wa ushiriki mpana na bayana wa wananchi
 
ni haki yake kwenda mahakamani... moja ya misingi mizuri iliyowekwa na CCM
 
Kila la heri mchungaji pia atutaki wakuu wa mikoa wa kuteuliwa na rais na pia ukuu wa wilaya ufutwe mara moja na pia tume kuundwa kuchunguza kama una akili timamu nayo uiwasilishe huko.
 
Naamini hata wajumbe wa hii Tume wanajua ukweli kuwa ilikuwapo nchi inaitwa Tanganyika na Zanzibar au ukipenda nchi ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar! Hivyo basi kuwatendea haki watu na wakazi wa nchi hizi, ni vizuri tutumie majina sahihi kwa vitu sahihi kwa ajili ya kumbukumbu za kihistoria! Hivyo basi kwenye Katiba ijayo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo mwanzo wake mzuri umeanza na hii Rasimu, ni muhimu kutumia majina sahihi. Sisi wa nchi liyokuwa ikiitwa TANGANYIKA tuitwe kwa jina hilo, yaani JAMHURI YA TANGANYIKA kwani ndiyo SAHIHI na ndugu/jirani zetu waitwe kwa jina lao sahihi yaani ZANZIBAR au JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR au vyovyote watakavyochagua.
 
mwacheni mtikila aende atarudi atatukuta tunaendelea kujenga tanzania yetu yawezekana yeye siyo mtanzania.
 
...Naunga mkono hoja, hakuna nchi ndani ya Muungano wetu iliyokuwa inaitwa Tanzania Bara, bali kuna Tanganyika, hivyo katu tusikubali uwepo wa Serikali ya Tanzania Bara bali Serikali ya Tanganyika. Na kwa kuwasaidia Wazanzibar, Zanzibar ni kubwa zaidi ya Mapinduzi ya 1964, sio lazima ukubaliane na Mapinduzi kuwa Mzanzibar, naamini sio sahihi kuiita ni Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar bali jina sahihi lilipaswa liwe Serikali ya Zanzibar..
 
Siyo Mtikila peke yake anayepaswa kwenda huko bali watanganyika wote , Warioba kwa kudiriki kuikataa Tanganyika nina Mashaka kwamba hana asili , au labda Asili yake iko nje ya mipaka ya Tanganyika !
 
Huyu Comrade namwaminia. Na hivi hajasikika kwenye kesi siku nyingi. Ngoja waone mziki wake.
 
zile pesa alizopewa na rostam ashazirudishe uyu ni mnafiki,alikuwa anamponda rostam lakin ela zake anapokea,kuweni makin na awa wanasiasa wanafiki wasiwaingize mkenge
 
Me hapo tu ndyo huwa nachoka
..unajua wanaamini watanganyika hawana kelee
ndyo maana wanawachagulia vitu. hii ndyo inayowafanya
wazanzibar kuamini watanganyika wanautaka muungano
na ndyo walioulazimisha muungano huu kwa mana wakomaa
na jina la tanzania na kusahau la kwao tanganyika me nadhani kuna haja ya
kuitambua tanganyika ya watu 45,000,000 kama inavotambulika zanzibar ya
watu 800,000. NB nasikia eti watani wa watu zanzibar per square meter umezidi
standard za kimataifa. sa inakuwaje hapo na wengine wapo tanganyika.
 
Back
Top Bottom