Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 48,851
- 18,948
Mtikila kortini kwa uchochezi
2008-08-05 10:35:17
Na Hellen Mwango
Mchungaji Christopher Mtikila, jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka ya kutoa lugha ya uchochezi na kudai kuwa Rais Jakaya Kikwete ni gaidi.
Mtikila alisomewa mashtaka yake jana mbele ya Hakimu Mkazi Focus Mkeha wa mahakama hiyo.
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Charles Kenyella, alidai kuwa, Oktoba 21, mwaka jana, eneo la Ilala katika kota za Shirika la Nyumba (NHC) zilizopo karibu na Kiwanda cha Bia (TBL), jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alitoa lugha za uchochezi.
Ilidaiwa kuwa, maneno hayo yalikuwa ya kuikashifu serikali na kwamba yalisababisha upotevu wa amani kwa wananchi.
Kenyella, alinukuu maneno ya Mtikilila akidai kuwa, ``Papa alikuwa na mgeni ambaye ni gaidi ninaomba niseme haya kwa sababu ninasema mimi, Rais Kikwete ni gaidi wa kwanza kutaka kupeleka bungeni,`` alinukuu kupitia hati ya mashtaka.
Katika shtaka la pili, Mtikila anadaiwa kuwa, siku na eneo la tukio la kwanza alitoa lugha ya uchochezi na kudai kuwa, ``ahadi zote za Jakaya Kikwete siku zote zinaongozwa na imani yake ya dini, tena kutekeleza malengo yake ya kusilimisha nchi, ``hatuwezi kuvumilia mtu anayekuwa muhuni aongoze nchi``.
Mtikila alikana mashtaka yote ambapo upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika na kwamba uliomba tarehe nyingine ya kutajwa.
Hata hivyo, Hakimu Mkeha aliahirisha shauri hilo hadi Agosti 22, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.