Mtikila: Mungu ameitumia Dowans kumwondoa Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtikila: Mungu ameitumia Dowans kumwondoa Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Jan 21, 2011.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Jan 21, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  MWENYEKITI wa Chama Cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, amesema kitendo cha serikali kutaka kuilipa Kampuni ya Dowans ni sawa na ujambazi na kwamba Mungu ameitumia kampuni hiyo kumuondoa Rais Jakaya Kikwete madarakani.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mtikila aliungana na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, kupinga serikali kuilipa kampuni hiyo Sh94 bilioni zilizotokana na hukumu ya Mahakama ya Usuluhishi ya Biashara ya Kimataifa (ICC).

  “Unajua mwisho wa utawala wa Rais Kikwete unaweza ukawa umejifinya nyuma ya hili suala la Dowans, kwa kuwa kila mtu sasa anajua Dowans ni nini, na kila mtu anajua ni uporaji,” alisema Mtikila.

  Alihoji sakata hilo kuwa gumzo nchini bila kutolewa ufafanuzi wowote na rais na kuongeza kuwa, ukimya wa Rais Kikwete unaibua maswali mengi ndani ya vichwa vya Watanzania.

  “Kwa nini Rais Kikwete hataki kuzungumzia Dowans, silence implies concerned (kimya kinamaanisha husika), siafiki kabisa serikali kuilipa Dowans, huu ni wizi na kama wananchi wakiamua kuingia mtaani kupinga jambo hili sidhani kama polisi wataweza kuwazuia, kwa kuwa wako wachache na risasi zao hazitatosha,” alisema Mtikila.

  Source: Gazeti la Mwananchi.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,523
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  man at work ... Dont joke with him.. Na moto petrol ndio ishamwaga na watu wameenda kununua lighter ,let wait and see them.
  Wanatudharau sana ila haya madharau yao yatakuja kutoboa mavitambi yao sasa sijui nao watakimbilia saudia. But hata wakikimbilia huko ....government ya uswis wata seize maaccount yao kama walivyowafanyia viongozi wa Tunisia na familia zao.
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mungu huchukia sana Wauza Unga, Wafadhili Ugaidi na Wachuuzi wa Uchaguzi katika mataifa mbalimbali.

  Lakini ili kuwaonyesha kwamba katika Mungu aliyejuu na ndiye atutiaye nguvu, Watanzania tunaweza yote bila CCM. Huyu Ndege Mjanja miaka yote kwa jina la CCM sasa imenasa katika tundu bovu la Dowans ya Rais Rostam Azizi.

  Sisi wananchi tunawasubirini CCM kwa hamu kubwa huku nje, msitucheleweshe sana kama mnawalipa Dowans bila ridhaa yetu fanyeni hivyo haraka!!!
   
 4. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #4
  Jan 21, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Jk unasikia mambo hayo??? Washauri wako wasikudanganye, toka huko magogoni njoo huku uswahilini utuambie dowans ni nani?? Hata ukituambia ni nani hatutakuruhusu uilipe hata senti tano. Ukiipuuza sauti ya umma, ndipo utatambua tofauti ya kachumbali na mboga. Hao askali unaowategemea wataua wananchi lakini kamwe hawatawamaliza kabla ya ukombozi wa nchi hii kupatikana na hapo ndipo utakapotambua kuwa hakika mwenye madaraka ni mwananchi na siyo viongozi, kama wengi wenu mnavyojidanganya. Kazi kwako.
   
 5. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #5
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Cha ajabu zaidi ni kwamba Jambazi Dowans hakuvunja ukuta wowote wakati anakuja kuibaka uchumi wetu.

  Hii kampuni ya kigaidi ilipitia LANGO KUU YA KUINGILIA NCHINI MWETU kuja kutenda madhambi yote ambayo mpaka sasa jamii ya Tanzania inafahamu tu taarifa chini ya robo yake.

  Haka kamdugu kaliingia nchini kwa zulia nyekundu, heshima ya kifalme, baadhi ya maafisa wake wakipamba na sifa za kijemedari na hatimaye kusaidiwa na mamlaka tulizoziheshimu, kuziamini na rasmi kuzikabidhi jukumu la kusimamia uzuri maslahi yetu kama taifa.

  Hapo nyuma kidogo wananchi tuliwauliza wakajipime na kuamua kama kweli bado kuna cha kuwafanya wabakie madarakani au wakajiondokee tu, lakini mpaka leo kimya kingi huonekana kutawala. Sasa maadam mambo ni kuamua kuwalipa tupende tusipende, basi muda umefika wa sisi kuwaombeni funguo zote za ofisi zetu umma.

  Nihitimishe kwa kurudia usemi wa wenzetu wa huko Ughaibuni kwamba: Baadhi ya viongozi wa juu wa CCM asanteni sana kwa kufaulu kutudanganya katika kila kona ya maisha yetu lakini nashukuru hamjafanikiwa kutudanganya milele daima.

  Watanzania wengi sana wamefunga kwa imani zetu tofauti tukiombea taifa salama taifa letu na kumsihi Mungu Mwenyezi kwa udhati kabisa akatuondolee salama VIWAVIJESHI vilivyotuzunguka na kutugawa kila siku kwa misingi ya kidini.

  Hata baada ya kuondoka serikali dhalimu bado kuna maisha nandio maana tunaendelea na sala zaidi kwa ajili ya Umoja wetu wa Kitaifa baada ya kupe kupisha.

  Sababu za kumfanya NGOMBE AITWAYE TANZANIA kuendelea kukonda miaka yote kiuchumi wa mtu mmoja mmoja licha ya TUNU YA AMANI tulionayo mpaka leo hii Mungu kaamua kutuonyeshea kwa njia ya kimiujiza ajabu!!!!!!!

  Watanzania wenzangu, acheni Mungu aitwe Mungu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 6. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #6
  Jan 21, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,207
  Trophy Points: 280
  Kikwete asifanye mzaha na swala hili la Dowans ingawa kuna watu wanabeza lakini linaweza kumwondoa madarakani, hili swala si dogo kama anavyofikilia kwa sababu linahusu wizi na ikijulikana kuwa yeye alihusika itakuwa fedheha sana kwake kama rais kutaka kuwaibia wananchi wake.

  Kwa sasa kulivyo na tension toka utata wa matokeo ya uchaguzi mkuu kinachotakiwa ni tamko la mtu mmoja tu ndiyo ntolee, kwani wananchi wakiamua kuingia mitaani haitachukua siku nyingi polisi watapiga siku ya kwanza siku ya pili watu wakiendelea mitaani polisi nao watakuwa taabani itabidi JK akimbie mwenyewe.
   
 7. Ngaramu

  Ngaramu JF-Expert Member

  #7
  Jan 21, 2011
  Joined: May 7, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nahisi harufu kali ya TUNISIA !!!
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Jan 21, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,523
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  nilidhani ni pua yangu tu..dw swahili leo nilikuwa nawasikiliza wanasema tunisia watu waliingia mtaani na polisi walivyokuwa wanaua ndio hasira za watu na munkari ulivyokuwa unazidi kuongezeka yaani wakiua mtu mmoja ndio walivyokuwa wana alter the rate of reaction(catalyst) mwishowe rais akaona isiwe tabu akajikata zake.
   
 9. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #9
  Jan 21, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Sikio la kufa halisikii dawa
   
 10. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #10
  Jan 21, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Warudie kama ya Arusha waje waone
   
 11. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #11
  Jan 21, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Ben Ali aliona isiwe taabu akakusanya familia yake hao Saudi Arabia maana aliona kitumbua kimeingia mchanga sasa huyu mwenzetu naona ni sikio la kufa ambalo halisikii dawa tena bila aibu ameuchubua tu utafikiri ni bubu
   
 12. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #12
  Jan 21, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280

  kama mimi!!
   
 13. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #13
  Jan 21, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,830
  Likes Received: 10,142
  Trophy Points: 280
  Huyu ana familia kubwa sana, sijui nani atampokea na utitiri wa watoto, wake na vido...+
   
 14. chobu

  chobu JF-Expert Member

  #14
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mimi nadhani JK sio kwamba hasikii au haoni hali ilivyo; yeye ni mtu mzuri sana wa kusoma nyakati. Tuvute subira kidogo ataongea tu!!!!!!!!
   
 15. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #15
  Jan 21, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,741
  Trophy Points: 280
  The only path out of official graft in this country is the impeachment of JK......................yeye ndiye kinara wa ufisadi humu nchini......................Bunge lilisema Hosea afutwe kazi jk alimlinda hadi muda wake utakapokwisha hivi karibuni..............................

  Wikileaks zimetufumbua macho kumbe JK ndiye anawazuia Takukuru wasipambane na rushwa kubwa kubwa kwa masilahi ya nani/

  let us read between the lines....................JK must go and Tanzania without him is very possible................
   
 16. chobu

  chobu JF-Expert Member

  #16
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mimi nadhani JK sio kwamba hasikii au haoni hali ilivyo; yeye ni mwepesi sana wa kusoma nyakati. Tuvute subira kidogo ataongea tu!!!!!!!!
   
 17. M

  Mopalmo JF-Expert Member

  #17
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  heri huyo alitumia busara akaachia hapa kwetu tungekufa wote na asingeachia mtu madaraka,naomba yasitokee hapa kwetu maana thamani ya utu wetu isingeonekana mbele ya madaraka
   
 18. m

  mapambano JF-Expert Member

  #18
  Jan 21, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukiingia ikulu kwa mizengwe utatoka kwa mizengwe......Alipofika JK its unrecoverable....He has to pave the way, it is that simple or else the army will be left with no alternative but to take over
   
 19. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #19
  Jan 21, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,936
  Likes Received: 673
  Trophy Points: 280
  akabeba na tani moja na nusu ya dhahabu......
   
 20. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #20
  Jan 21, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,936
  Likes Received: 673
  Trophy Points: 280
  huyu jamaa hachoki...... ni kichwa twenty four seven
   
Loading...