Mtikila kuwaburuza mawaziri wa JK mahakamani


P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Messages
40,019
Likes
8,875
Points
280
P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2007
40,019 8,875 280
MWENYEKITI wa chama kidemokrasia (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, anaandaa utaratibu wa kuwafungulia mashtaka Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Philip Marmo kwa kuidharau Katiba.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Mchungaji Mtikila alisema kitendo cha viongozi hao wawili kwa nyakati tofauti kueleza kuwa suala la mgombea binafsi haliwezekani na linahitaji lipelekwe kwa wananchi kwa ajili ya kura za maoni ni kuvunja Katiba.
“Utaratibu wa kuwasimamisha kizimbani Marmo na Membe kwa kuvunja Katiba na sheria kwa kuthubutu kuifanyia jeuri na dharau mahakama ya nchi uko palepale,” Mtikila alisema.
Mwenyekiti huyo wa DP alisema kwa sasa wanasheria wake wanashughulikia kesi nyingine zipatazo tisa za Kikatiba lakini suala hilo litashughulikiwa hadi haki hiyo kwa Watanzania ipatikane.
Alisema hoja ambazo zimekwishatolewa na mawaziri hao pamoja na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Rajab Kiravu, ni porojo na haziwezi kuathiri utendaji wa mahakama.
Aliukosoa utetezi wa Waziri Marmo kwamba muda hautoshi kwa kuandaa mazingira ya mgombea binafsi kwa vile suala hilo linahitaji umma kushirikishwa na kusema hiyo ni haki ya Kikatiba, haihitaji umma kuulizwa iwapo wanaitaka.
Mtikila alisema amri ya mahakama kuruhusu mgombea binafsi ilitolewa Mei 5, 2006 na kuwatuhumu watendaji wa serikali akiwemo mwanasheria mkuu kufanya njama za kutotekeleza amri hiyo kwa miaka minne sasa.
“Pili, hakuna mabadiliko kufanywa katika Katiba wala mahakama haiamuru hivyo kwa sababu Katiba ndiyo inayotoa haki hii kwa kila raia hasa Ibara ya 21 (2)...mahakama tu ndiyo inayotoa haki nchini ya kutafsiri sheria pamoja na Katiba ...siyo Marmo, Membe wala Rais Jakaya Kikwete,” alisema.
Akinukuu maneno ya Waziri Membe aliyoyatoa kwa mabalozi baada ya kukutana nao katika viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mchungaji Mtilila alisema hatua ya kuwataka mabalozi wavute subira juu ya suala la mgombea binafsi ni kuliuza taifa.
Katika hilo, mwanasiasa huyo anayeongoza kwa kufungua kesi nyingi dhidi ya serikali, alisema waziri huyo ameuza uhuru wa taifa kwa kitendo chake cha kuwanyima Watanzania haki yao huku akijadiliana na wanadiplomasia hao.
“Membe amethibitisha tabia inayowachukiza wananchi kwamba wanaotawala nchi yetu hawana ridhaa ya wenye nchi, bali wanajisalimisha kwa mataifa makubwa,” alisema.
Alisisitiza kwamba suala la kugombea uongozi ndani ya nchi ni nyeti na ni la utaifa ambalo kulitafutia uhalali kwa mataifa mengine ni kuuza uhuru wa nchi, kosa alilolifananisha sawa na uhaini.
Aliushutumu uongozi wa Rais Kikwete kwa kutaka kuhujumu haki hiyo na kutabiri kutokea machafuko yatakayoifanya Tanzania kutengwa na jumuiya za kimataifa.
Alisema mbinu ya kuzima suala la mgombea binafsi inayofanywa na watendaji wa Rais Kikwete inatokana na hofu ya kumpata mgombea atakayechuana naye katika kinyang’anyiro cha urais Oktoba.
“Rais Kikwete hata akifaulu kuzima ushindani ndani ya chama chake, ataibuka mgombea binafsi na wanachama wote watamfuata na kuiacha CCM inamfia mikononi,” alisema. Aliongeza kwamba baada ya usajili wa Chama cha Jamii (CCJ), hatma ya CCM ilianza kuwa mashakani kutokana na ukweli kwamba
 
Ben Saanane

Ben Saanane

Verified Member
Joined
Jan 18, 2007
Messages
14,602
Likes
3,913
Points
280
Ben Saanane

Ben Saanane

Verified Member
Joined Jan 18, 2007
14,602 3,913 280
Hold on,tafadhali naomba rekebisha kichwa cha habari kwanza.

Mkuu,kichwa cha habari kinapotosha.

Ungeweza kuweka Mtikila kuwaburuza mawaziri wa JK mahakamani

au

Mtikila awageukia mawaziri wa JK

au

Mtikila kuwashtaki mawaziri wawili wa JK.
 
BelindaJacob

BelindaJacob

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2008
Messages
6,109
Likes
600
Points
280
BelindaJacob

BelindaJacob

JF-Expert Member
Joined Nov 24, 2008
6,109 600 280
Pdidy nilijua wako mbaroni kweli, heading inachanganya!.lol!!
 
Ndibalema

Ndibalema

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2008
Messages
10,945
Likes
240
Points
160
Ndibalema

Ndibalema

JF-Expert Member
Joined Apr 26, 2008
10,945 240 160
Kaka MBARONI ninavyoelewa mimi ni kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi lakini kushtakiwa sio kutiwa mbaroni.
Labda ungerekebisha kichwa cha habari.
By the way thanks a lot.
 
B

ByaseL

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Messages
2,224
Likes
25
Points
145
B

ByaseL

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2007
2,224 25 145
You know, the recent statement by the Chief Justice on the Independent Candidates has really rattled the JK regime out of its hole. Walifikiri kuchelewesha rufaa hadi 2010 (tangu 2006) ingewasaidia lakini it has cought them with pants down! Wanatapatapa. Anachosema Mtikila ni kitu cha maana kwa vile Mahakama inasema kugombea madaraka ni haki ya msingi kabisa kama ilivyokula, kulala na kwenda msalani. Huwezi kusema tuwaulize wananachi kama tule au la. Vile vile huwezi kuwauliza watu kama wanataka kugombea madaraka kupitia vyama vya siasa au la. That is the point and the regime is scared stiff!
 
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
45,945
Likes
32,759
Points
280
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
45,945 32,759 280
Mtikila anapata wapi hela za kuwalipa mawakili?
 
P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Messages
40,019
Likes
8,875
Points
280
P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2007
40,019 8,875 280
ni kweli byasel ila kwa serikali yetu unafikiri watakubali br
tutaishia kununua magazeti kama sijakosea
 
Jayfour_King

Jayfour_King

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2009
Messages
1,141
Likes
12
Points
0
Jayfour_King

Jayfour_King

JF-Expert Member
Joined Nov 15, 2009
1,141 12 0
Kichwa cha habari kimekaa ki udaku nakubaliana na wanaosema kibadilishwe mara moja.
 
Mateso

Mateso

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2008
Messages
259
Likes
13
Points
35
Mateso

Mateso

JF-Expert Member
Joined Aug 6, 2008
259 13 35
Kimsingi Mtikila ana point kwa sababu mahakama ikishatoa maamuzi ya namna hii ilikuwa kazi ya wizara husika kutengeneza draft bill ya mabadiliko ya sheria zote husika ikiwemo katiba ambayo ni sheria mama na kuzipitisha kwa vyombo husika kuzipitia kabla ya kupeleka final draft bungeni. Sasa serikali imekalia swala hili tangu 2006 hadi leo ili waanze kuja kubabaisha watu mwaka huu wa uchaguzi. Is this a good governance or mere politics? A justice delayed is not a justice at all, we needto see the justice be done. Lawyers, kindly assist Mchungaji on this matter so that the justice can be done as soon as it deem fit. Naona Serikali inaleta madharau kwa muhimili mwingine wa dola.
 
M

MpendaTz

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2009
Messages
1,693
Likes
175
Points
160
M

MpendaTz

JF-Expert Member
Joined May 15, 2009
1,693 175 160
Ama kweli hapa mchungaji amekua mwiba! Napenda mambo kama haya, yanazidi kudhihirisha kuwa ufisadi unaleweshaaa!! na umelaaniwa na Mnyazi Mungu!
 
Kiranja Mkuu

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2010
Messages
2,100
Likes
41
Points
0
Kiranja Mkuu

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Joined Feb 18, 2010
2,100 41 0
Kweli shuzi limepamta mjambaji
 
Ngongo

Ngongo

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2008
Messages
12,494
Likes
4,259
Points
280
Ngongo

Ngongo

JF-Expert Member
Joined Sep 20, 2008
12,494 4,259 280
Serekali inatakiwa kuheshimu uamuzi wa mahakama sasa inapotokea mawaziri ambao ni washauri wakuu wa Rais wanapotosha umma kwa maksudi au kwa faida za kisiasa nchi inaweza kutumbukia kwenye migogoro isiyo na sababu.
 
ELNIN0

ELNIN0

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2009
Messages
3,874
Likes
314
Points
180
ELNIN0

ELNIN0

JF-Expert Member
Joined Nov 26, 2009
3,874 314 180
Mtikila ukimaliza hiyo - buruza na nyingine ya kudai Tume Huru ya Uchaguzi - Bara. hii iliyopo ni ya CCM.
 

Forum statistics

Threads 1,251,743
Members 481,857
Posts 29,783,065